Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Hon. Charles Muhangwa Kitwanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kutoa shukrani kwa nafasi hii. Nianze tu kwanza kwa kutoa shukrani angalau safari hii nimeona hela katika kusaidia kupata maji katika Jimbo langu la Misungwi. Kwa masikitiko makubwa sana vilevile lile swali nililouliza la nyongeza kwamba, pale Ihelele ambapo ndipo chanzo cha maji hata leo hii pamesahaulika. Sasa safari hii patachimbika na mimi sitatoa shilingi, nitakachofanya nitakwenda ku-mobilize wananchi wa Misungwi kama 10,000 tukazime ule mtambo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tangu mwaka 2008 tunaendelea kusubiri, tunaendelea kusubiri na leo mmethubutu kuandika huku kijiji cha Nyanhomango kimepata maji wakati hakina. It’s so disgusting kwamba World Bank walikuja pale wakasema this is inhuman, halafu sisi tunaona ni human. World Bank wamefika pale wakaona kwamba hawa watu ambapo maji yanatoka hawana maji, wakasema this is inhuman, lakini wafanyakazi waliokuwa nao wameendelea kuona huo ni ubinadamu. Siwezi kukubali na sitakubali na hili lazima libadilike, kwa sababu hii nchi ni yetu wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia huku pesa nyingi zimepelekwa sehemu ambazo siwezi kuzitaja na maji labda yapo, ni vema tukatendeana haki. Inanipa shida zaidi kuona kwamba hata mahala ambapo Mheshimiwa Rais aliahidi maji pale Usagara hamna senti iliyowekwa humo, kama imo mnionyeshe. Ninachowaomba jamani tutendeane haki. Huwezi kuwa na mradi wa kwenda mpaka Tabora unatumia bilioni 600 unashindwa kuwapa hawa watu wa pale ambapo maji yanatoka hata bilioni kumi? Very unfair, ninazungumza hili likitoka moyoni mwangu kabisa. Nakipenda sana chama changu, naipenda sana Serikali yangu, nampenda sana Mheshimiwa Magufuli lakini ninyi watu wa Wizara lazima mtende haki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi ya hapo hata ile barabara inapokwenda chanzo cha maji sasa hivi haipitiki kwa sababu ile ni ya tani 10, lakini yale malori yanayobeba yale madawa ni 28 tons, 40 tons, sasa Halmashauri kila ikijaribu kutengeneza inashindikana. Nashukuru Wizara ya Ujenzi angalau wameweza kui-upgrade ile barabara kuwa ya TANROADS. Niseme tu kwamba haki haijatendeka hapa na mimi sitatoa shilingi wala nini dawa yenu ni kwenda kuzima ule mtambo, eeh. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, dawa yenu ni kwenda kuzima ule mtambo wote tukose, eeh! Kwa sababu gani, kama tunasema na mmeniahidi hapa kwamba na mimi nimekwenda nimeongea na watu wa KASHWASA wakaniambia it is 4.2 billion, ziko wapi? nimeona hapa bilioni
3.9 najua ni za kutoka Mbalika kuja Misasi. Halafu sasa tutakuwa tunapoteza hata hela, kwa sababu kutoka Mbalika kuja mpaka Misasi tayari mabomba yamewekwa, kutoka kwenye chanzo cha maji kuja hapa Mbalika, hamjaweka, hata common sense jamani hatuna? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati mwingine inanishangaza sana, yaani mnishukuru tu nilikuwa Waziri zamani nilikuwa siwezi kusema, sasa nimetoka tutapambana. Ninachosema ni lazima tuwe good planner, lazima tuwe na mipango mizuri, tuwe na mikakati mizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mbona kwenye REA tume- perform vizuri tu, kwa nini tusi-perform vizuri hata kwenye maji vijijini, tuna matatizo hapo kidogo. Sasa mpaka nashangaa wakati mwingine, niliomba mradi kwa rafiki zangu kutoka Austria nikawa nimepewa, baadae nikapigwa figisu figisu eti kwamba wewe una-interest, ndiyo nina interest! Kwa sababu watu wangu wa Kolomije wanahitaji maji! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wangu wa Bukumbi wanahitaji na tulipokuwa Bukumbi na Mheshimiwa Rais akawambia wananchi huyu ana marafiki zake wengi nchi za nje. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikawa nimetafuta kule mara ya kwanza wakasema kwanza Tanzania ichangie 20 percent kwenye design hela kidogo, sasa hivi wamesema hivi hata hiyo 20 percent tunawasamehe kamilisheni hiyo miradi awamu ya kwanza ili nami Bukumbi wapate maji, Kolomije wapate maji, Ibongoya wapate maji. Kwa sababu waliishaniahidi kwamba tukiishamaliza tu hiyo awamu ya kwanza na wewe utapata. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa namuuliza mmojawapo ya wakubwa hapo kwamba hebu vipi huu mradi wa Austria ananiambia achana na huo mradi wa Austria. Sasa hatuwezi kutajana majina, I was a little bit disappointed. Niombe tu huo mradi na wenyewe tuupe, kwa sababu sasa hivi wameshakubali, kinachotakiwa ni sisi ku- respond kwa Serikali ya Austria kusema kwamba go ahead, halafu wakishamaliza hapo wanachosema pelekeni ombi lingine sasa la hivyo vijiji vyangu ambavyo nimevitaja. Hamia huko kama unataka, ni pazuri sana. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo ndugu zangu wapendwa sitajihangaisha kutoa shilingi, lakini mjue mtajua sasa maharage ni mboga au ni zao la biashara. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.