Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza naungana na wote waliotoa rambirambi na naungana na wote waliopongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze haraka mambo matatu, katika kifungu ambacho kinahusiana na umeme, mafuta na redio Zanzibar ni tatizo. Fedha zilizotengwa hazitoshi katika Mkoa wa Mjini Magharibi. Mkoa wa Mjini Magharibi una Wilaya tatu na una jumla ya vituo 14, Askari wanachangishana wenyewe katika vituo hivi. Kwa hiyo, hapa namwomba Mheshimiwa Waziri aangalie vizuri.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miradi ya maendeleo, niliahidiwa ukarabati wa nyumba za Polisi, ukarabati wa Makao Makuu ya Polisi na niliahidiwa uzio pamoja na nyumba mpya za Polisi lakini bado hayajafanyika. Hapa kuna kituo kimoja cha Mkokotoni hicho ambacho kimetajwa.Kwa hiyo, hiyo naomba katika miradi ya maendeleo waje watuangalie vizuri.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo hapa lilizungumzwa naona kwamba bora na mimi nigusie, haiwezekani ugomvi wa nyumbani kwako ukaenda ukamtumpia jirani yako. Wewe umeachia ushuzi katika nyumba yako, harufu ya ushuzi ule unamsingizia jirani, jitazameni ninyi wenyewe, CCM haishiriki katika mgogoro waCUF na ndiyo maana tunasema la kuvunda halina ubani. Hiyo nisakaratul maut, mtu anapokuwa katika sakaratul maut anakuwa mara nyingi hajitambui, kwa hiyo, hiyo mtambue ni sakaratul maut hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ni muhimu mlijue kilichowaponza ni tamaa zenu wenyewe.

Mlihisi mnakuja kupokea mapesa kumbe ndiyo mmekwenda kukiua Chama. Kwa hiyo, ni ninyi wenyewe, mgogoro wenu wenyewe kwa tamaa zenu wenyewe, msisingizie Chama cha Mapinduzi hata siku moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu jambo lingine ambalo ni muhimu mzingatie kwamba hayo mambo mliaza ninyi wenyewe ukaribishaji, utoaji, kumuingiza huyu kwenye Chama, kumtoa huyu mlifanya wenyewe, CCM imehusika wapi? Mjiangalie vizuri.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende katika hoja moja ambayo alizungumza hapa mtu haki za binadamu katika Magereza. Haki za binadamu katika Magereza ni lazima ziangaliwe pamoja na usalama ndani ya Magereza. Ndiyo maana hapa ikasemwa kwamba watu wanapekuliwa mabanda ya uwani, mabanda ya uwani lazima watu watapekuliwa, anaweza mtu akaingia na shazia ikahatarisha usalama, akaingia na msumari, anaweza mtu akaingia na silaha yoyote. Kwa hiyo, nimpe pole au kama nimpe hongera Mheshimiwa Lema kama na yeye yalimkuta haya ya kupekuliwa mabanda ya uwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ubaya wenyewe unaweza ukaja ukamkuta mwanaume mwenzako anakuvalia gloves halafu anaanza kusema mashallah, lazima utakuja kusema hivyo hapa...(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na hili nalizungumza maksudi ili watu waache kuota ndoto za kipuuzi na kutangaza hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.