Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja hii kwa asilimia mia moja na nachangia kwenye maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, Kituo chetu cha TBC naomba kiimarishwe, hususan maeneo ya vijijini. Aidha, Redio ya Taifa na TV – TBC hazisikiki kabisa na TV za TBC muono wake sio mzuri. Kwa mfano, maeneo ya Tarafa ya Amani, Muheza yenye Kata za Mbomole, Misanai, Zirai, Kwezitu, Kweningoji na kadhalika Redio ya Taifa, TBC, haisikiki kabisa. Naomba mipango ifanyike kuimarisha sehemu hizo ili vyombo hivyo visikike na kuonekana.

Mheshimiwa Spika, wasanii wanafanya kazi kubwa lakini inaonekana haki zao (copyright) hawazipati kama inavyostahili; ni vizuri kuweka mikakati madhubuti ya kuwasaidia kupata haki zao. Aidha, wote wanaofanya uhalifu huu wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kutungwa Sheria hivi karibuni ya Vyombo vya Habari, lakini maslahi ya waandishi wa habari hawapewi. Wapo waandishi wengi hawalipwi mishahara na wanaendelea kuwa vibarua. Suala hili liangaliwe kwa umakini mkubwa.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Timu yetu ya Serengeti Boys, ni vizuri timu hii ikaangaliwa vizuri na isipoteze wachezaji hao ili baadaye wawe Taifa Stars. Taifa Stars imeshindwa kabisa kutuletea sifa katika nchi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na kocha bora na wacheaji wengi wa Taifa wana umri mkubwa.