Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

MHE. BALOZI ADADI RAJABU: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuunga hoja mkono na kuwapongeza wote; Mheshimiwa Waziri, Naibu, Katibu Mkuu na Watendaji wote kwa kazi kubwa wanayoifanya. Naomba kuchangia kwenye maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi ya NIMR ni muhimu sana na ina sifa kubwa kwa tafiti mbalimbali za magonjwa ya binadamu Afrika na dunia kwa ujumla. Taasisi hii tawi lake lipo Muheza na lina mpango mahususi kabisa wa kuanzisha Chuo Kikuu kwa msisitizo wa masomo haya ya Tafiti za Binadamu, masomo ambayo hayapo hapa Afrika. Majengo yapo ila yanahitaji ukarabati kidogo huko Amani, Muheza. Sasa ni kwa nini Wizara haikutoa umuhimu wa kutenga fedha kwa ajili hiyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshatenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza. Tunaomba Wizara iangalie uwezekano wa kusaidia ujenzi wa hospitali ili isaidiane na Hospitali Teule ya Muheza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tunaomba Mheshimiwa Waziri aangalie uwezekano wa kupeleka CT- Scan na utengenezaji wa lift katika Hospitali yake ya Bombo, Tanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, magari ambayo yametolewa Kanda ya Ziwa, uwezekano wa magari hayo kutolewa kwenye Vituo vya Afya vya Muheza uangaliwe, maana kuna matatizo makubwa ya usafiri wa kuwapeleka wagonjwa kwa haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Chuo cha Mafunzo mbalimbali ambacho kipo maeneo ya Kiwanda, Muheza. Chuo hiki kipo chini ya Mheshimiwa Waziri lakini kimedharaulika kabisa, ni kama hakipo. Idara ya Ustawi wa Jamii imekisahau kabisa. Kina matatizo mengi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri atume wataalam wake ili tushirikiane tuweze kukubaliana tutakisaidia vipi Chuo hiki kisife?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa juhudi zao wote Wizarani.