Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Katiba na Sheria

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Katiba na Sheria

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipatia fursa hii ya kutoa mchango kwa njia ya maandishi. Napenda kumpongeza Waziri wa Katiba na Sheria yeye pamoja na wataalam wake kwa kuandaa hotuba hii yenye kuonesha ubora na utaalam mkubwa. Katika kuchangia hotuba hii, napenda kuchangia maeneo yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, urejeshwaji wa wahalifu na ushirikiano na Mataifa kwenye makosa ya jinai, hili ni jambo zuri ambalo linaongeza ushirikiano na mahusiano mazuri kwa Mataifa ya nje. Uhalifu ni jambo baya ambalo linahitaji kupigwa vita kwa nguvu zote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika suala hili, Serikali iwe makini katika utekelezaji wake. Inapotokelezea ulazima wa kuwapeleka wananchi wetu (wahalifu) ni vyema tukaangalia usalama wa nchi tunayotaka kuwapeleka. Kwa mfano; juzi imetokezea wahalifu wa biashara ya unga ambao wanafika kupelekwa Marekani lakini hivi sasa katika nchi ya Marekani kuna vita ya maneno kati ya Marekani na Korea ya Kaskazini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hali hii inatisha na ni vyema tukachukulia tahadhari kubwa. Korea ya Kaskazini wametishia na wanaendeleza vitisho la kuipiga Marekani kwa silaha za nuclear, hii ni hatari kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maendeleo ya rasilimali watu, rasilimali watu ni jambo jema katika sehemu zote za maendeleo. Ushauri wangu katika jambo hili ni kwamba, Serikali ni vyema ikawatayarisha kwa kuwasomesha na kuwapatia elimu juu ya masuala ya kisheria ili kuendeleza ufanisi katika Wizara hii nyeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.