Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante namshukuru Mungu na nashukuru kwa yote na wote waliofanya vizuri. Kule kwetu kulikuwa kuna bomba/mfereji ambao unatoa maji safi. Sasa kuna mtu alienda akafunga koki kwa sababu yeye ana kisima chake huko yale maji ya kisima chake yanazidi kupanda bei. Katika hii kesi ya pesa za machinga huku nje tunasikia kuna kausha damu wanakopesha kwa riba kubwa lakini kwa nini hizi pesa za wamachinga kwa miaka miwili zilipangwa shilingi bilioni 22 hazikutoka na sasa zimepangwa shilingi bilioni 18 hazikutoka au inafanana na hii kesi ya huyu aliyekwenda kulifunga bomba na huku ana kisima chake ili apandishe maji kwenye kisima, tulitizame vizuri sana hili suala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaambiwa utaratibu wa benki, ni sawa utaratibu wa benki hivi hiyo Serikali imeshindwa kuwasiliana mpaka leo pesa zikafika hapo. Mwenyekiti alitoa hii hoja kwamba hizi fedha zitolewe kwa haraka na riba ipungue lakini na utaratibu wa kupatikana vitambulisho uende vizuri. Kwa hiyo, hii tunahofia katika suala hili kwa sababu ni mwaka wa pili pesa hizi hazijatoka na mna component tatu, kuna other charges hazijatoka pia kuna fedha ambazo zikajenge zile ofisi amabazo amezizungumzia Mheshimiwa Furaha pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala jingine na kwenda katika Wizara ya Kazi na Ajira, huku tumesema kuna programme ya kukuza ujuzi lakini tumepata poromoko tumetoka kutoka watu 42,000 mpaka 12,000, tumeanguka kwa 71%. Isitoshe kuna mpango wetu wa Taifa tumeuweka kwamba kwa miaka mitano tufikie watu 600,000,081 ambapo kila mwaka ni watu 136,000,000. Hivyo, sisi tunakwenda tunapata watu wachache zaidi. Fedha zilizopangwa zilikuwa zitumike kwa mwaka shilingi bilioni 109 lakini tunatumia shilingi bilioni 9, maana yake tunafikia kwa 8% tu peke yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo je, ipo haja ya kuwa na hii programu? Hii programu ilipaangwa kwa kulenga one third ya skills development levy ndiyo maana ukaja ukaona kwamba hatuendi sanjari. Sasa je, skills development levy hatupeleki kwa one third. Hapa Mheshimiwa Waziri wa Fedha alileta sheria lakini akaja akaiondosha kwamba ku-ring fence ile one third, aliiondosha. Sasa tutizame je, tunaweza kufikia hili lengo, kama hatufikii tunajidanganyia nini? 8% mwanafunzi au mtoto huwezi ukasema umefaulu kwa 8%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine tuna mifuko yetu ya hifadhi ya jamii, hapa Mwenyekiti ametoa hoja kwamba wastaafu wanaomba kuongezewa pensheni zao. Huku Wizara imesema inataka kufanya actuarial study utafanyaje actuarial study wakati Serikali yenyewe ina deni la shilingi trilioni 2.45 la PSSSF. Kule kwenye NSSF pia 1.39 trillion shillings Serikali wanadaiwa Serikali. Ukitaka kufanya actuarial ina maana kwamba ni lazima uingize na uwezkezaji wa hizi taasisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, uwekezaji hizi fedha zitakuwa ziko nje. Sasa tukisema tunafanya actuarial study ina maana hata tukienda tukataka kuwalipa tutawapunja. Kwa hiyo, Serikali ijaribu kuangalia hivi vitu kwa maana hiyo kweli tuongeze lakini tujaribu kuangalia hilo suala. Jingine alizungumza hapa Babu Tale ameondoka na nilimtania pale kidogo kutokana na hii…

MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ali Hassan King kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Taletale.

TAARIFA

MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampa taarifa muongeaji kwa neno la Hayyakum dhanna amedhani kama nimeondoka wakati nipo, ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa King endelea na mchango wako.

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, alikusudia iyyakum wadhanna (Jiepusheni na kudhani). Mimi sikumuona pale alipo kwa hiyo nilikuwa niko sahihi macho yangu ndiyo yaliyosema hivyo. Babu tale alisema hapa kwamba ingawaje hii sports betting ni haramu lakini kwa nini isitoke? Kule kwetu kuna usemi, Mshairi mmja anaseama “Ingawa haramu, malipo yake ni moto, msaidie mwenzako.” Kwa hiyo, namuunga mkono kwamba hili fungu la sports ambalo tumesema ni 5% liende kule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, si kweli kwamba Bunge lako hili unajua kwamba pesa za sports betting kwamba hazijulikani, zinajulikana hata na mimi ninazo. Mtu atakayezitaka hizo hata na mimi nnazo naweza nikazileta za mwaka juzi, mwaka jana na mwaka wa leo kwa sababu zipo lakini kwa nini hazitoki? Nashauri tu-ring fence hii 5%, tu-ring fence Serikali iki-fence tu hapa moja kwa moja zinakwenda zake Wizara ya michezo. Kama hatukufanya hivyo bila ku-ring fence ina maana kwamba matumizi yake bado yatabakiwa kuwepo katika Wizara ya Fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina mengi ya kuzungumza, nashukuru sana kwa kupata nafas, naunga mkono hoja. (Makofi)