Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge kuhusu Wakala wa Kimataifa wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (International Renewable Energy Agency - IRENA) na Azimio la Bunge kuhusu mapendekezo ya kuridhia Mkataba wa Kuanzisha Taasisi ya Dawa ya Afrika wa Mwaka 2019 (Treaty for the Establishment of the African Medicine Agency - AMA)

Hon. Ummy Ally Mwalimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tanga Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge kuhusu Wakala wa Kimataifa wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (International Renewable Energy Agency - IRENA) na Azimio la Bunge kuhusu mapendekezo ya kuridhia Mkataba wa Kuanzisha Taasisi ya Dawa ya Afrika wa Mwaka 2019 (Treaty for the Establishment of the African Medicine Agency - AMA)

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, niwashukuru wachangiaji wote ambao wamechangia hoja yangu ya kuomba Bunge lako lipitishe Azimio kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Mkataba wa Kuanzisha Taasisi ya Dawa ya Afrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli maoni yote ambayo yametolewa yanaunga mkono Azimio. Niseme kubwa, sisi kama Serikali tunaamini kwamba kuridhiwa kwa mkataba huu wa AMA, itakuwa ni moja ya nyenzo muhimu katika kupambana na bidhaa tiba duni na bandia, kukuza soko la bidhaa tiba ambazo zinaweza kuzalishwa na nchi nyingine. Kwa hiyo, kubwa tunaamini tutanufaika zaidi na Azimio hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati imeunga mkono jambo kubwa ambalo Kamati imesema na Mheshimiwa Christina Mnzava, ni kwa nini tumechelewa? Ndiyo taratibu zetu za Serikali, lakini naamini maazimio mengine ambayo yana maslahi makubwa kwa nchi tutajitahidi kuyaleta kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, Askofu Josephat Gwajima kwa kweli ameongea jambo kubwa sana zuri na inaonekana amefanya research kwenye masuala ya teknolojia ya genetics. Ni kweli ndiyo tiba sasa hivi, hata kwenye masuala ya stem cell therapy, masuala sasa hivi ndiyo yanajitokeza. Kwa hiyo, Azimio hili pia linakwenda kudhibiti, maana sasa hivi hatuna sheria ya kudhibiti masuala kama hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalize kwa kusema kama walivyosema Dkt. Ndugulile, Askofu Gwajima na Mheshimiwa Christina Mnzava na Kamati ya Mheshimiwa Nyongo. Kweli dawa ni maisha, biashara na siasa. kwenye biashara ukiangalia baada ya biashara haramu ya silaha, dawa za kulevya, dawa ni moja pia ya biashara tatu kubwa ambazo zina-generate mapato makubwa sana. Kwa hiyo ni lazima pia tuimarishe mifumo na uwezo wa nchi katika kudhibiti dawa, vifaa tiba vitendanishi pamoja na bidhaa nyingine za afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, angalizo ambalo limetolewa na Mheshimiwa Dkt. Ndugulile tumelipokea, kuhusu masuala ya udhibiti wa chakula tutaendelea kujadiliana ndani ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, angalizo lingine ambalo tunaenda nalo ni kuimarisha uzalishaji wa ndani wa dawa. Sasa hivi kwa mfano katika maji tiba (drip) tunavyo viwanda viwili ambayo vinazalisha Maji tiba na kukidhi soko la nchi. Tunayo Kairuki Pharmaceuticals na Alfa Pharmaceuticals, wana uwezo wa kuzalisha chupa 98,000,000 za maji tiba wakati mahitaji ya nchi ni chupa 24,000,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tunaamini kabisa tukipitisha Azimio hili pia as long as nchi nyingine zimeridhia Mkataba wa AMA tuna uwezo wa kwenda kuuza ziada katika chi nyingine za Afrika. Pia kubwa tumepata maoni kuna wawekezaji wako tayari kuja nchini, lakini wananiambia Minister, when we come to Tanzania, we can’t sell for Tanzanian market. We have also to sell for SADC and EAC. What are the requirements? Kwamba, do we need also to register our products in Kenya, Rwanda, Burundi?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tukipitisha mkataba huu na kama Kenya ameridhia, Zambia, Rwanda, Burundi, Zimbabwe, maana yake wawekezaji pia watavutika kuja kuwekeza Tanzania na hivyo bidhaa zao kuuzwa katika nchi nyingine za Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge, kama Serikali tutaendelea kutoa kipaumbele kwa bidhaa za afya, bidhaa tiba zinazozalishwa ndani ya nchi. Mwaka jana tulinunua bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi zenye thamani ya shilingi 14,000,000,000. Mwaka 2023 tumenunua bidhaa za afya zinazozalishwa ndani ya nchi zenye thamani ya shilingi 36,000,000,000. Kutoka shilingi 14,000,000,000 mpaka shilingi 36,000,000,000. Kwa hiyo naiona commitment ya Serikali katika kuimarisha uzalishaji wa ndani wa bidhaa tiba. Tunaamini kabisa mkataba huu pia utatuwezesha kufikia lengo la Serikali la kupunguza uagizaji bidhaa tiba kutoka nje ya nchi angalau kwa 50% ifikapo mwaka 2030.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa Bunge lako lipitishe Azimio kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Mkataba wa Kuanzisha Taasisi ya Dawa ya Afrika (Treaty for the Establishment of the African Medicines Agency - AMA).

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.