Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa ruhusa ya kusimama leo, kwanza nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amenipa kibali na pumzi yake ya bure na kuweza kuchangia katika masuala ya ulinzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Samia Suluhu Hassan na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, amefanya kazi kubwa tumetembelea vikosi tumekuta amefanya kazi kama alivyoahidi kwamba kazi inaendelea, lakini sisi tulikuja tuliona kazi zinaendelea maana ni nyingi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara hii ya Ulinzi kwa kazi kubwa pia wanayoifanya. Lakini kipekee nimpongeze Mkuu wa Majeshi Jenerali Mabeho, Mnadhimu Mkuu, Makamanda wote kwa kazi nzuri na njema wanayoifanya katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumeona mara nyingi panapotokea maafa wanajeshi wamekuwa mstari wa mbele katika kwenda kusaidia wananchi. Lakini pia tulipata simanzi mwaka jana kwa kuondokewa na Rais wetu mpendwa wa Awamu ya Tano Dkt. John Magufuli, lakini Jeshi la Wananchi lilisimama imara likahakikisha nchi imetulia na mpaka sasa wananchi wana amani katika nchi yao, hongereni sana majeshi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nalipongeza tena Jeshi tumetembelea Makao Makuu ya Ulinzi pale Kikombo tumekuta vitu vya ajabu, hatukutegemea kuona kama kuna wakandarasi wa kiwango cha juu cha aina ile. Ukipata nafasi nenda katembelee. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi tulikuwa tunauliza hili jengo limejengwa na Mchina, Mjapani kama tulivyozoea, lakini jengo lile limejengwa na wataalam wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Lakini limetumia fedha kidogo lakini kwa ubora na hadhi ya hali ya juu, limeokoa shilingi bilioni 69; nani kama Jeshi la Wananchi wa Tanzania? (Makofi)

WABUNGE FULANI: Hamna.

MHE. JANETH M. MASABURI: Hongereni sana makamanda. Hawa ni wazalendo, ni waadilifu iwapo Serikali itawajengea uwezo wataweza kufanya vitu vikubwa sana katika nchi hii. Kuna mambo mengine ambayo tunaweza kuyasema kuna mengine hayasemeki, wanahitaji fedha. Kuna mazao ya kila aina ambayo wakipata kiwango kikubwa cha fedha, tutaweza kuuza katika nchi za jirani, tutaweza kuwaongezea uwezo Jeshi letu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, naomba niongelee kuhusu suala la…

SPIKA: Kengele imeshagonga Mheshimiwa.

MHE. JANETH M. MASABURI: Mama yangu weee. (Kicheko)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Spika, leo hunipi kidogo dakika moja basi niongee kimoja tu. Leo nihurumie, najua umenikubalia.

Mheshimiwa Spika, ninaomba barabara zilizopo pembezoni za Mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya doria ya ulinzi ziwekewe lami zitengenezwe, kwa sababu nchi jirani wana barabara lakini huku wanajeshi wetu wanapata ugumu sana kwa sababu hatuna barabara ambazo zitasaidia doria katika mambo ya ulinzi. (Makofi)

Mwisho naomba bajeti iongezwe, bajeti ya ulinzi ni ndogo bajeti ya vyombo vya ulinzi vyote ziongezwe. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nakushukuru sana. (Makofi)