Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja Kuhusu Bei ya Kuuza na Kununulia Mahindi

Hon. Aeshi Khalfan Hilaly

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sumbawanga Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hoja Kuhusu Bei ya Kuuza na Kununulia Mahindi

MHE. AESHI K. HILALY: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza, naomba ku–declare interest kwamba na mimi ni mkulima, lakini ni mfanyabiashara.

Mheshimiwa Spika, naungana na hoja za Wabunge waliokuwa wanaomba Serikali kwamba, hili jambo sasa hivi liahirishwe na haya masharti mengine yawekwe wakati wa msimu ujao. Nasema hivyo kwa sababu moja tu, haya masharti ambayo yamewekwa sasa hivi, yangewekwa kabla, nafikiri wakulima na wafanyabiashara wangejiandaa, lakini yamekuja katikati ya msimu, wafanyabiashara wameshaanza kununua mazao na wengine wamesafirisha.

Mheshimiwa Spika, pamoja na nia njema ya Mheshimiwa Waziri, ni rafiki yangu lakini tulikaa naye hapa, ni muumini wa kutofunga mipaka. Juzi Mheshimiwa Waziri aliruhusu magari yaliyozuiliwa mipakani yaende Kenya na mengine yaende Rwanda. Pamoja na nia nzuri ya Mheshimiwa Waziri ya kuruhusu, lakini imetokea wale wote waliokuwa na magari wamepigwa faini ya shilingi milioni moja moja kwa kila mtu.

Mheshimiwa Spika, sasa inawezekana Mheshimiwa Waziri aliruhusu bila kuwapa maelekezo. Hata hivyo, Wakuu wa Mikoa wameamrisha magari yote walipe faini ya shilingi milioni moja moja bila kosa, laiti wangelijua wangelijiandaa mapema.

Mheshimiwa Spika, sio kazi ya mkulima kuhakikisha kwamba mwananchi wa Tanzania hafi na njaa. Ni kazi ya Serikali kuhakikisha kwamba mwananchi anapata chakula, lakini vile vile anapata huduma nyingine. Hatujawahi kuona Serikali ikimsaidia mkulima kwa asilimia 100. Hata hivyo, mkulima huyu anajitahidi mwenyewe anafanya kazi mwenyewe, analima mwenyewe…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)