Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

Hon. Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi na mimi nitoe mchango wangu kwenye Bajeti Kuu ya Serikali. Nianze kwanza kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya katika Taifa hili lakini kipekee kwa miradi mikubwa anayoifanya ndani ya Jimbo langu la Kwela na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla sisi tunampongeza na tunamuombea maisha marefu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Naibu na timu yote ya wataalamu niwape pongezi kubwa kwa kazi kubwa mnayofanya ya kumsaidia Mheshimiwa Rais. Leo pamoja na mambo mazuri yaliyosemwa katika Speech yako ya Bajeti Mheshimiwa Waziri nina mambo machache ya kushauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo moja ambalo nililifurahia ni kati ya Wabunge waliosimama kuchangia juu ya hali ya mtaji kwenye Benki zetu za Serikali kwa maana ya TCB (Tanzania Agricultural Development Bank) pamoja na TID Development. Nimeona katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri mmetenga kiasi cha shilingi bilioni 235 kwenda kuziwezesha benki hizi ili walau kuzinusuru katika hali ya mtaji lakini kwa namna ambayo nimeona plan yenu ya kutenga shilingi trilioni moja ndani ya miaka 10 ili kila benki hizi tatu ambazo ni benki za kimkakati za Serikali ziwe na fedha au mtaji wa shilingi trilioni moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jambo jema lakini muda mliojiwekea miaka 10 ni muda mrefu sana. Ninachoomba mfanye kwa TCB mmetanguliza fedha shilingi bilioni 30 na hivi karibuni mnaenda kupeleka shilingi bilioni 101. Jambo hili nawapongeza kwa fedha hizi mnaenda kuinusuru hii Benki inakaa vizuri kimtaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo deficit ambayo tunatakiwa kuweka pale ni shilingi bilioni 700. Katika Bajeti hii mnapeleka shilingi bilioni 100. Niwaombe ndani ya muda mfupi mfikishe hii shilingi trilioni moja kwenye Benki hii ya Kilimo ili kusiwe gap kubwa kwa maana huu mtaji mnaoweka shilingi bilioni 100 msipokaa vizuri mkasubiri hiyo miaka 10, nao utamezwa kutakuwa ni kazi bure.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halikadhalika Benki ya TID Development (Benki ya TID Maendeleo). Ile pale ina deficit ya mtaji karibia shilingi bilioni 370. Napo pale mnapeleka shilingi bilioni 100, kutabaki deficit karibia ya shilingi bilioni 270. Naomba nazo hizi mzitengee muda mfupi mkakamilishe, mkishindwa kufanya hivyo maana yake hata shilingi bilioni 100 hii itamezwa kutakuwa ni kazi bure. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkifanya hivyo wazo la kuja na shilingi trilioni moja litafuata baadaye wakati tayari mme-stabilize vitabu katika Benki hizi hizi tatu za Serikali. Ni jambo muhimu sana nililotaka kushauri Mheshimiwa Waziri na ulichukulie kwa maanani makubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo limepigiwa kelele ni suala la ununuzi wa mazao nitaongelea zao la mahindi na Mheshimiwa Waziri Bashe kwenye bajeti hii umesimama zaidi ya mara nne, mara tano umetoa maelezo mazuri kabisa sina mashaka naye. Umetoa maelezo na ulivyosema kauli yako unasema kwamba hatufungi mipaka lakini mnataka m-regulate export ya mahindi mkuze wigo wa kodi (tax base) ili tayari export ya mahindi iwe reflected kwenye mapato ya Taifa ni jambo zuri lakini mnapofanya hiyo approach muangalie pia stabilization ya price kwenye zao hili la mahindi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndani ya wiki mbili hizi ambapo mko kwenye transition period hapa mahindi yalikuwa kilo moja shilingi 800, hivi ninavyoongea ndani ya wiki mbili hapo ambapo mnakuja na hizo measures za ku-control export ime-drop kwenye Mkoa wa Rukwa kutoka shilingi 800 mpaka shilingi 450. Maana yake gunia la shilingi 80,000 lime-drop mpaka shilingi 45,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni nini? Chochote unachowaza kufanya, control measure yoyote unayofanya iwe ya kudhibiti export ya mahindi ili nayo ichangie kwenye kodi ya Serikali siyo jambo baya, hakikisha stabilization ya price ya mahindi isiyumbe kwenye measures unazochukua. Kufanya hivyo hakutakuwa unachofanya, madhara yake yako kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaenda huko mtaweka hizo sijui control, sijui hivi masharti mengi mengi, mta-discourage hawa wanaotaka kununua mahindi yetu. Mkisha-discourage, competitor wetu wa zao la mahindi mkubwa ambaye anafanya vizuri katika viwango vya juu ni nchi jirani ya Zambia. Ita-capitalize masoko hayo na baadaye hata tuje tufungue mipaka, tupunguze nini hatutaweza kupata wateja wa mahindi yetu yatakuwa tayari zao la mahindi lime-collapse. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii siyo kwamba ni mara ya kwanza itatokea, hapana. Mwaka 2017, 2018, 2019 tulifanya jambo hili hili tukafunga mipaka kwa nia tu moja tu ya usalama wa chakula nchini kwa gharama ya mkulima yaani tunataka tuwe na food security kwa expense ya mkulima. Tukafunga mipaka, tulipofunga mipaka Zambia ika-take over masoko yote ya mahindi. Soko la mahindi likaanguka, tulikuja Bungeni hapa tukapiga kelele Wabunge wote wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini tukajenga hoja hapa ikalazimika twende tukachukue overdraft ya shilingi bilioni 50 CRDB tukanunua na bado Serikali haikuwa na capacity ya kununua kwa sababu mazao yalikuwa yamezagaa hakuna kwa kupeleka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, measures zote mnazochukua we must be very sensitive. Tuwe tuna balance, tuna balance hicho tunachosema food security ya nchi lakini tunaangalia mkulima tusimuumize kwa sababu unakuta tunafanya haya yote 45, wakulima wameshindwa kukopesheka mahindi mwaka huu. Hamna benki iliyojitolea, commercial bank zote hata Benki ya Kilimo ilikataa. Unakopeshaje zao la aina hii ambalo lenyewe halitabiriki? Benki gani inataka kupata hasara? Hamna benki inayomweza kukubali mambo ya namna hii kwa sababu hata ukiangalia Ripoti ya BOT, performance kwenye Sekta ya Kilimo mikopo imekuwa ikiyumba sana kwa sababu ya sera zisizotabirika kwenye mazao yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, alizeti Wabunge wengi wamesema wa Singida na wengine ilikuwa ni zao ambalo tulili-encourage wakulima walime na ukienda kwenye portfolio ya Benki ya Kilimo walitoa viwanda shilingi milioni 700, 800. Leo hii mikopo ile hailipiki tayari tunaenda kupeleka non-performing loan nyingi kwenye Benki ya Kilimo kwa sababu ya sera hizi zisizotabirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kodi zetu tuanvyo-set hizi kodi hizi Mheshimiwa Waziri umesema aah tunapunguza mafuta ghafi ya kuingia nchini mjue huko huko benki zetu mnazopeleka huu mtaji mlikopesha wakulima. Tutarudi mwakani benki mitaji ime-collapse kwa sababu hakuna repayment kwenye Sekta ya Kilimo tumei-paralyze. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hili jambo mliangalie kwa umakini mkubwa muende mkaangalie tu-balance mazao hasa mahindi tusikubali wananchi kwa mara ya kwanza wanavuna wakiwa na shilingi 80,000 leo hii shilingi 45,000. Niombe tu utakachofanya chochote Mheshimiwa Bashe iwe between shilingi 75,000 na wewe mwenyewe unasema NFRA nimeona kwenye Hotuba ya Waziri mnaenda kununua tani laki nne lakini kwenye mfumo tu wa NFRA una ambiguity na una anomalies nyingi sana ambazo zinakwanza kwenye manunuzi yake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza moja, hamna infrastructure za kutosha, vituo tu vya kutosha vya kukusanya mazao ya wakulima havitoshi kwa sababu inabidi mkulima asafiri kilometa nyingi kuja kufuata NFRA ilipo. Jimbo langu la Kwela unajua kwa mfano mtu anatakiwa asafiri kilometa 100 na zaidi kufuata kuuza unakuta anaenda kuuza tena anaondoka pale anakuta tena pale kuna bureaucracy nyingi. Watu wenye nguvu za fedha wanateka masoko, wao ndiyo wanakuwa wa kwanza kupima. Mkulima anayepeleka mahindi kwenye toroli kamwe hawezi ku-access NFRA kwa hiyo, niombe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia bado wananchi wamekuwa wana complain hata vipimo vinavyotumika pale sehemu nyingi tuna analogia. Wakulima wanakuwa wananung’unika tuna punjwa. Nendeni hata NFRA na CPB taasisi zako mtakazoenda muende na mizani ya digital ili mkulima asiibiwe mazao yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu kwa sababu tumeona zao la mahindi ni tija, kwa nini tusiendelee ku-pump hela nyingi? Siyo lazima tuchukue huko, twendeni kaongezeni overdraft na nyie mnunue kwenye competitive price mahindi kuliko haya mambo mengi tunayoongea ni mazuri tu ni lugha very cosmetic lakini implication yake kule siyo hivyo Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimekwambia very frankly na hiyo measure tukachukue tuhakikishe mkulima wa mahindi hatumuumizi tukanunue bei ya kuanzia shilingi 75,000 na kupanda. Chini ya hapo ni maumivu. Tuli-subsidize mbolea maana yake nini?

MHE. EDWIN E. SWALLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Sangu, taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Swalle.

TAARIFA

MHE. EDWIN E. SWALLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kumpa taarifa Mheshimiwa Deus Sangu kwamba hii bei ya mazao ya wakulima wameuza bei nzuri ya shilingi 800, 700 kwa kilo shambani na yako mashamba yako umbali wa kilometa zaidi ya 150 kwenye masoko ya NFRA kwa hiyo, tukisema wakapeleke huko sokoni watapata hasara. Hili Mheshimiwa Waziri wa Kilimo alizingatie sana, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Deus taarifa unaipokea?

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipokea ni msisitizo wa jambo hili. Hili tunalo Mheshimiwa Bashe tunaendelea nalo mpaka tufikie consensus mahali ambapo kutakuwa win win, Serikali i-win na mkulima a-win. Nihame hapo nadhani message itakuwa imefika vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nililokuwa nataka kuchangia Mheshimiwa Waziri wa Fedha, ifikapo nyakati kama hizi tunapoelekea mwisho wa mwaka wa fedha mifumo yote halmashauri ina paralyze haifanyi kazi. Mfano kwenye halmashauri yangu siku 20 sasa hamna business yoyote inayo-transact. Wanasema mifumo imekwisha. Tumefika mahali tulikuwa tunachukua hata kwa wazabuni mafuta, sasa hivi hata ambulance zinaenda kukosa mafuta ya kujaza pale kuhudumia wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naombeni kama inafikia hatua mnapofuga mwaka wa fedha kuna shida kwenye mifumo yenu, muwe na alternative ya ku-attend emergencies za Serikali kwa sababu hatuwezi tukasema mifumo imekufa, kwa hiyo, watu wafe mahospitalini? Kwa hiyo mambo yale basic ya muhimu yasiende? Lazima mtafute alternative ya kuwa na namna ya ku-rescue yale mambo ya dharura ili sasa isiwe kwamba mifumo ime-paralyze nchi nzima hamna kinachoenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ni mbaya kwenye halmashauri tayari kuna wazabuni, wazabuni ambao walifanya kazi. Maturity obligation zao kwa maana ya wanahitaji kulipwa sasa mifumo imefungwa tutakuja tuletewe riba ya kucheleweshewa malipo tunaingiza hasara Serikali, kwa hiyo niwaombe jambo hili utakapokuwa una wind up utueleze vizuri limekaaje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante nashukuru naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)