Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Hon. Mohammed Maulid Ali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiembesamaki

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

MHE. MOHAMMED MAULID ALI: Mheshimiwa Spika, naomba na mimi kutoa mchango wangu kwa maandishi kuhusu bajeti ya Wizara hii kwa mwaka 2023/2024.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote naomba nimshukuru Mungu kwa kunijaalia nafasi ya kuchangia bajeti hii ya Wizara ya Mawasiliano na Ujenzi kwa mwaka 2023/2024.

Mheshimiwa Spika, pili naomba nimshukuru Rais wetu kwa kupeleka fedha nyingi kwenye Wizara hii kwa lengo la kuhakikisha miradi yote iliyotengwa inakamilika.

Mheshimiwa Spika, mchango wangu utajikita zaidi kwenye eneo la mamlaka ya bandari kuhusu uwekezaji unaokwenda kufanywa na Serikali kwenye gati na 8, 9 na 10.

Mheshimiwa Spika, napenda kuwatoa hofu Wabunge wenzangu na wananchi wote kwamba kinachokwenda kufanyika pale ni ubia kati ya Serikali yetu na wawekezaji hawa kwa lengo la kuongeza ufanisi. Kazi tutafanya sote na mapato ni yetu sote. Sambamba na hilo ni vizuri tukaelewa kwamba management pamoja na operations za bandari yetu zitaendelea kubaki kama zilivyo hasa kwa vile Serikali imeboresha gati na 5, 6 na 7 kwa ajili ya general cargo na makontena.

Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia mchango wangu napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mbarawa na timu yake yote kwa kazi nzuri inayofanywa na Wizara hii kwenye maeneo yote yakiwemo ya barabara, reli na anga.

Mheshimiwa Spika, ahsante na naunga mkono hoja.