Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru wewe kwa kinipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya Makadirio na Mapato ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024, hii ni miongoni mwa Wizara muhimu sana katika nchi yetu na kwa uchumi wa nchi yetu.

Pili, napenda kumpongeza Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoongoza nchi yetu kwa umakini mkubwa sana na kuiweka nchi yetu katika hali ya usalama, amani na utulivu.

Tatu, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa namna walivyotayarisha hotuba hii kwa ubora wa hali ya juu na hatimaye kuiwakilisha hotuba hii katika Bunge lako tukufu kwa ufasaha mkubwa sana.

Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo; kwanza ni kuhusu huduma za ndege.

Mheshimiwa Spika, napenda kuipongeza Serikali yetu kwa namna inavyojitahidi kutaka kurahisisha usafiri wa ndege katika nchi yetu. Huu ni ujasiri mkubwa uliochukuliwa na Serikali yetu ya kuimarisha usafiri wa ndege nchini. Lakini bado bei za ndege za ndani (domestic flights) ni kubwa sana kwa wananchi wetu. Wananchi wanashindwa kumudu bei hizo na kushindwa kufaidi matunda ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu katika jambo hili kwa Serikali ni kuangalia uwezekano wa kupunguza bei za ndege za ndani kwa manufaa ya wananchi wa nchi hii.

Pili ni kuhusu huduma za bandari, napenda kuipongeza Serikali yetu kwa namna inavyoonesha nia ya kutaka kuboresha bandari zetu kwa nia ya kutaka kuongeza uchumi wa nchi hii kupitia bandari. Bandari katika nchi zote duniani inakuwa ni moja kati ya vyanzo vya mapato.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu katika jambo hili kwa Serikali ni kwenda na azma yake ya kutafuta wawekazaji ambao wataweza kuendesha bandari zetu hasa ile ya Dar es Salaam ambayo iko kiuchumi zaidi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.