Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Hon. Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia kwenye Wizara hii ya Ujenzi na Uchukuzi. Kwanza niseme, naipongeza Serikali kwa kuona umuhimu ambao tumekuwa tukiipigia kelele sana, ingawa bado ni asilimia 47 tu kwenye ukarabati wa ujenzi wa Kiwanja cha Musoma. Tunaomba sana ukamilike kwa haraka kwa sababu pale ndipo anapotoka Baba wa Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuchangia kuhusiana na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Serengeti. Tulizungumza hapa na tukaonesha jinsi gani uwanja ule ukijengwa utaenda kufungua fursa za kiuchumi kwa sababu una multiplier effect na Serikali hapa ikatuhakikishia, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara yenu ya Ujenzi na Wizara ya Fedha, mlikaa mkasema kabisa kwamba ule Uwanja wa Serengeti unaenda kujengwa na umetengewa shilingi bilioni 147. Nimepitia hotuba yako yote, sijaona sehemu yoyote ambapo umeainisha. Baada ya kusema vile, wananchi na wawekezaji mbalimbali walikuja Serengeti wakanunua maeneo mbalimbali ya ujenzi wa hoteli na vitu vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hivi ilivyo, watalii wakitoka huko kwenye mataifa mengine, wanaopita route ya huku, wanashukia Nairobi then wana-drive na magari kuja Serengeti. Sasa kuna wengine wanakuwa disgusted, tunapoteza mapato. Tunaiomba sana Serikali, ili kuweza kukuza utalii wa nchi yetu, ili kuweza kukuza uchumi wa Tanzania, mtujengee uwanja wa Serengeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli tokea iende re- allocation, basi Wizara iweze kuchukua hatua kuhakikisha kwamba wanaanza angalau kwa mwaka huu wa fedha wanatenga fungu kidogo kuelekeza hapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kipekee kabisa niwapongeze madada ma-pilot ambao wapo kwenye Air Tanzania, walikuja hapa jana, walikuwa 10 kati ya 106, bado idadi ni ndogo sana, tunatamani wafike 50/50, lakini ni hatua nzuri kuelekea hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mchango wangu zaidi nitajielekeza ATCL na muda ukitosha nitaenda na kwenye TPA. Ni dhahiri kabisa kwamba mashirika ya ndege ili yaweze kuwa endelevu na yajiendeshe kwa tija zaidi, kuna some components ambazo zinahitajika. Kwanza inahitaji uwekezaji mkubwa sana, mtaji mkubwa kwenye uwekezaji (capital intensive). Pili, lazima tuwe na udhibiti wa gharama za uendeshaji. Usipokuwa na udhibiti na gharama za uendeshaji hata ununue ndege ngapi sijui, lazima utakuwa unaona hasara zikijitokeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa viwango vya Kimataifa vya gharama za uendeshaji ambazo ni standard zinajulikana, tunajua kwa upande labda wa mafuta ni asilimia 30. Utakuta kwenye maintenance cost inakuwa labda asilimia 20, kuna rasilimaliwatu kati ya asilimia 10 mpaka 15 na kuna vikosi vingine vidogo, hivyo ni kwa mashirika yote hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ili shirika letu la ATCL liweze kuwa shindani, ukitoa hizo component za gharama ambazo nimesema, tumeipa burden tena kwa hizi fedha za kukodi ndege kutoka TGFA. Mkataba huu wa kukodisha ndege, na huu nitauongea very bitterly, tumezungumza mara nyingi hapa, mpaka hata Katibu Mkuu Kiongozi wa Ikulu aliongea kuhusu kuhakikisha kwamba ndege zinarudi ATCL. Ni mzigo mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, basi Serikali ikasema imeweka huo mkataba kama caveat ya ndege zisikamatwe. Ndege zinakamatwa sana, zinashindwa hata kuruka kwenda kwenye vituo vya nje ambavyo ni vya kimkakati. Mathalani, ndege zetu zinashindwa kwenda Johannesburg ambapo zilikuwa zinatengeneza fedha nyingi sana. Kuanzia 2018 August kila mwaka tunapoteza takribani 37 billion kwa sababu haturushi ndege kwenda Johannesburg. Kwa nini? Tunaogopa zitakamatwa? Sasa huu mkataba ambao tumeweka ambao ni mzigo unasaidia nini? Ukiangalia pia tunakataa kupeleka ndege Landon au Ulaya, tunaogopa zitakamatwa. We are losing a lot of money, 13 billion zinapotea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndege za kukodi, kwa mfano hii tu ya kwenda South Africa Machi, 2022 mpaka Machi, 2023 tumepoteza 17.3 billion, halafu tunaendelea kukumbatia huu mkataba ambao it is a burden. Sasa ukiangalia ripoti ya CAG ikitoka, wanasema shirika linajiendesha kihasara. Kwa mfano, huu mwaka 2021/2022 imerekodi kwamba imejiendesha kihasara kwa 35 billion, lakini ukiangalia kiuhalisia, direct cost ambazo zinatokana na ukodishaji wa ndege ni 85 billion, ukitoa hiyo hasara, unajikuta shirika in fact lingeweza kuwa na faida over all most 50 billion, kama ingekuwa hatujaweka huu mkataba wa kukodisha ambao hauna tija. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mlikuwa mnataka mweke mkataba kuzilinda ndege, mngeweka tu hata shilingi milioni 100 au shilingi milioni 200, si mnataka mwoneshe kama TGFA inakodisha kwa ATCL? Kwa nini mweke burden kubwa hivyo? Hela nyingi za kukodi, bado sijui una-reserve maintenance, process zenyewe za procurement ni ndefu, unakuta wanachukua hela zao nyingine wanakarabati, kunakuwa kuna double count.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ni direct cost. Ukichukua tu direct cost uka-oversight na hiyo hasara uliyosema, una profit ya 50 billion. Sasa ukiongeza kwa mfano huo mwaka wa 2022 ambao nimesema, fedha ambazo tumepoteza, 37 billion ndege ya abiria kwenda South Africa, uongeze 17.3 billion uje uongeze na hii ya kwenda Landon 13 billion unapata all most 37 billion. 37 billion ukijumlisha 50 billion hili shirika lingekuwa linajiendesha kwa faida kubwa, all most 117 billion. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii haihitaji kukodi wataalaam sijui uunde tume kutoka nje kuja kutushauri juu ya uendeshaji wa shirika letu na umiliki. It is just a mere wastage wa fedha za walipakodi masikini. It is just a common sense, yaani ukifikiria tu, is just a mere common sense, hauhitaji kuunda timu ya wataalam eti kushauri ni jinsi gani uweze kuwa na muundo ATCL, ni jinsi gani uweze kumiliki ndege. Are we serious real kama Taifa, and yet tunatumia hela za walipakodi masikini kulipa hao the so called wataalam kuja kutushauri sisi. Serikali tunaomba, huu mkataba ufe, ATCL ikabidhiwe hizi ndege, after all ndege hazitakamatika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kwenye hotuba yako Mheshimiwa Waziri umeandika Ibara ya 260 kwamba unaboresha Shirika of which I agree, unanunua ndege unaleta, unasema unaboresha uendeshaji kupunguza gharama. Component namba moja kupunguza gharama ya uendeshaji, ondoa huo mkataba feki kati ya TGFA na ATCL.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge lako Tukufu ningependa sana katika kupitisha hii bajeti tuazimie Serikali ivunje huu mkataba ambao ni burden kwa Taifa. Tunapoteza fedha kwa mfano kutokurusha ndege, hizo fedha, shilingi bilioni 67, zingeweza kuja Serikalini na zikajenga madarasa ya kutosha, vituo vya afya vya kutosha, but we are wasting them. Hizo ni forgone revenue kwa uzembe tu wa kuona kama umekodisha ndege. Haikubaliki kabisa. Lazima huo mkataba ufe. Haikubaliki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, Mheshimiwa Waziri ukitaka kweli shirika letu likue, tukishaondoa huo mzigo sasa, kwa sababu huo mzigo upo, lakini unaandika kwamba unataka iwe competitive labda na mashirika mengine…

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

TAARIFA

MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Festo Sanga.

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na mchango ambao anatoa dada yangu, Mheshimiwa Esther, tayari Mheshimiwa Rais alishaunda tume ambayo inashughulikia kuondoa ndege kutoka TGFA kwenda kwenye Shirika la ATCL ili kuondoa hizo burdens ambazo anazizungumza. Kwa hiyo, tume tayari ilishaundwa na Serikali ilishachukua hatua. Kwa hiyo, hili Mheshimiwa Rais aliliona kwa jicho la karibu sana, ndiyo maana ameshaunda tume tayari kwa ajili ya kuondoa hicho anachokizungumza, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther, taarifa unaipokea?

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, siipokei, kwa sababu hata wanaomshauri Mheshimiwa Rais, hawaitendei haki nchi hii. Kwa sababu hii tume imeundwa kitambo, halafu kwanza hata walifikiaje kumshauri Mheshimiwa Rais waunde tume wakati this thing was obvious? Sidhani hata wakati wanaunda hiyo tume kuleta mkataba huu waliunda hizo tume ambazo zinatumia fedha. Ndiyo maana nasema, tusipoteze at a time fedha, unaunda tume, unaleta watu sijui kutoka nje, they are using money ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ATCL ukilinganisha na Ethiopian Airlines kutoka Afrika tu hapa hapa, wenzetu wale kwanza Ethiopian Airline wenyewe ni kampuni ambazo zinajiendesha zikiwa sanjari na kampuni nyingine hodhi, ambapo kwa mfano kwenye uendeshaji wa viwanja, sijui mambo ya inflight catering na mambo mengine mengi…

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Deo Sanga.

TAARIFA

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisema wanaomshauri Rais wanamshauri vibaya, Rais huyo huyo ndio wamemshauri, amefanya maridhiano na ndiyo maana mambo yanakwenda vizuri. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Esther, taarifa unaipokea?

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, namheshimu sana mzee pale, lakini kuna ushauri wenye tija na ushauri mwingine hauna tija. Hatujakataa ushauri wote wanaoushauri kwa Rais yanaenda vibaya, lakini in particular this one wamemshauri Rais vibaya na kweli hao wataalam wanapoteza fedha za Watanzania…

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa hili narudia kusema it is a mere common sense.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilindie muda wangu kwa hizi taarifa.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Kuna taarifa.

TAARIFA

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mchangiaji anasema kuna ushauri wenye tija na usiokuwa tija. Ningetamani atuambie wenye tija ni upi na usiokuwa na tija ni upi?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther, malizia mchango wako.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania wanawasikia, kwa sababu wanaweza tu wakatumia their common sense. Katibu Mkuu Ikulu mwaka 2022, a year now, alisema kabisa kwamba hili la mikataba limeshaisha. ATCL wanarudishiwa ndege na mkataba una…, mwaka jana 2022 Katibu Mkuu Ikulu said that, and then… (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama Wabunge, tumetumwa humu ndani kuishauri na kuisimamia Serikali.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatakiwa kuhakikisha kwamba rasilimali za nchi yetu zinatumika vizuri. Tunashauri kwa nia njema kabisa, soberly.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu.

TAARIFA

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaheshimu sana mchango wa Mheshimiwa Mbunge. Wabunge kadhaa na mimi naomba kuungana nao, tunachokisema ni kwamba ni mapema sana. Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani, kati ya mambo ambayo aliyaona ni mambo ya kuyafanyia kazi kwa haraka ni pamoja na mkataba huo wa ATCL na akaagiza ni lazima tupate ushauri wa kitaalam, kwa sababu, tunaposema ushauri wa kitaalam, maamuzi tutakayoyafikia yatutoe moja kwa moja na yasitupeleke tena kwenye hasara ambayo imejitokeza huko nyuma. Kwa hiyo, sioni kama ni sahihi kuendelea kutumia maneno ambayo yanadhalilisha kazi hiyo nzuri, mawazo na maamuzi mazuri aliyoyafanya Mheshimiwa Rais kupitia watendaji wake kuhakikisha jambo hili tunalimaliza salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu nimpe taarifa Mheshimiwa Esther, Serikali jambo hili imelipa kipaumbele na baada ya muda siyo mrefu, tutakuwa tumefikia conclusion na shirika hili kila mmoja anatamani liweze kufanya kazi yake vizuri. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Esther, taarifa hiyo unaipokea?

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri anajaribu kupita pale pale tu, anarembaremba mambo. Mimi nakubali, nasema hivi, na Kamati yako ya Bunge ya Miundombinu ilishasema hili jambo hapa, TGFA warudishe hizi ndege kwa ATCL. Mheshimiwa Rais ana dhamira hiyo nzuri kwa sababu hizi forgone revenue zinazopotea zingeweza hata kusaidia, mama anazunguka kutafuta fedha while mnapoteza fedha hizi hapa, why are you doing that, guys? hamlioni hili? It is just a simple logic.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana. Mheshimiwa Waziri na timu yako na watendaji, tuone hili ni la muhimu sana. Hapa naongea tu, kama unaweza ukaleta ndege kwa mfano hiyo unayoleta ya mizigo, itaruka kwenda wapi? Ulaya si tumefungiwa, hatuwezi kupeleka ndege zinakamatwa. Hiyo ndege ya mizigo inayokuja, tunaipeleka wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, tunahitaji kupata mapato. Ndege mmeileta sawa, baada ya wiki mbili inakuja. Mmeirusha wapi? Hata wa East Africa mkienda Nigeria nasikia mtakamatwa. Mtairusha wapi? South Africa hampeleki, mnapeleka wapi?

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Esther.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, let us be sincere. (Makofi)

MWENYEKITI: Muda wako umeisha, nashukuru sana.