Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia katika bajeti hii ya Wizara ya Kilimo. Baada ya Mheshimiwa Halima kuongea, sauti yangu itaonekana imepwaya sana, lakini mnisikilize tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nami niungane na Wabunge wenzangu kwa kumpongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ambayo ameifanya ya kuipaisha nchi yetu mpaka sasa hivi hata Kimataifa tunajulikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, maana najua nina muda mfupi sana, nimwambie tu Waziri Bashe, kweli tunapenda mambo ya block farming, lakini isiwe to the expense ya wakulima wadogo. That is one. But two, tujue kwamba block farming inahitaji umwagiliaji sana, na umwagiliaji huo uwe wa drip au wa system gani, ambao hautaleta siltation. Tuangalie basi tume yetu ya umwagiliji kama ina capacity hiyo ya kuchukua hii role ya kufanya hii block farming na hii programme ya BBT kufanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia ripoti ya CAG ya ukaguzi wa kiufundi, 2018/2019 mpaka Januari 2019/2020 – 2022/2023, inaonesha upungufu mwingi ambao uko kwenye tume yetu hii ya umwagiliaji. Nitasema machache tu ambayo ni key kwa ajili ya argument yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, tume hii haifanyi upembuzi yakinifu kabla ya kuanza ujenzi wa miradi ya umwagiliaji. Hii tunaweza kusema kwamba tangu mradi ukianza umeshakufa kabla hata haujasimama. Pili, kuna udhaifu mkubwa kwenye kuzingatia Sheria ya Manunuzi. Maana yake ni nini? Fedha ya umma itatumika vibaya sana kama Sheria ya Manunuzi haifuatwi. Tatu, hii Tume ya Umwagiliaji haifanyi uhakiki wa viwango vya ubora wa miradi, na hivyo miradi mingi imeonekana ina kasoro sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu kuna miradi ambayo imekuwa ikichelewa sana kukabidhiwa, na hivyo inaongeza gharama katika kuendelea kutekeleza. Haya yote yanafanya tujiulize, hivi tunapoenda kwenye kufanya block farming na kama tume yenyewe ndiyo hii hii, na jinsi inavyo-operate ni hivi hivi, kweli tunategemea mafanikio? Kama Mheshimiwa Halima alivyosema, kwamba hizi fedha nyingi ambazo zinaenda kwenye miradi hii ambayo tunaona kuna upungufu sana katika hii tume ambayo ndiyo tunaitegemea, zingekwenda kusaidia wakulima wadogo wenye skimu zao kutengeneza vizuri, nafikiri tungefanya mazuri zaidi, maana naona hatujajipanga vizuri kuhusu block farming. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, linalonisikitisha kubwa zaidi, tukiangalia pia upungufu huo, kwenye bajeti ya Tume ya Umwagiliaji kwa mwaka wa fedha 2022/2023 iliidhinishwa shilingi bilioni 257.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji, lakini hadi kufikia Februari, 2023 ilikuwa imetolewa asilimia 18 tu ya fedha iliyotakiwa, yaani katika miezi minane ni shilingi bilioni 46.68 tu zilizokuwa zimetolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiingii akilini kwamba katika kipindi hiki cha robo mwaka kilichokuwa kimebaki, tume itaweza kutumia shilingi bilioni 210 wakati kwa miezi minane ilitumia tu shilingi bilioni 47. Kama hivyo ndivyo, hata huu mradi wa block farming nina mashaka sana kama utafanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua kwamba kweli wakulima wadogo wanahitaji kusadiwa sana, ukichukulia mfano kama alivyosema Mbunge wa Same Mashariki. Kule kwetu miradi mingi ya mpunga ambayo ilisaidia sana kulisha Mkoa Tanga, Kilimanjaro na Arusha ilikuwa ni ya kilimo cha umwagiliaji. Ukiangalia kilimo cha umwagiliaji cha skimu ya Ndungu, mfereji wa fidia, Kalinga Maore na hizo za Kihurio zilizosemwa zote zilikuwa zinalisha mikoa hiyo mitatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu miradi hii imejengwa tangu mwaka 1999 imetelekezwa. Kwa mfano, mradi wa fidia wa Ndungu, sasa hivi mvua ikinyesha kubwa inakuwa ni shida kwa wakulima hao. Mradi uliojengwa kwa msaada wa kutoka Japani ambao hatukuweza hata kuuhudumia, leo mvua ikija ni mafuriko kwa kwenda mbele, mashamba yanaharibika, zile barabara zilizotengenezwa za kuingia mashambani zinaharibika. Matokeo yake, badala ya kuwa baraka, mvua inakuwa laana kwa wakulima wale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wameomba wafanyiwe kitu kinaitwa kudebua mifereji ile. Nilishangaa kwamba kweli tume ilipeleka mitambo ile ya kudebua, lakini bila tume kuwasiliana na Halmashauri, ikitegemea Halmashauri itatoa Shilingi milioni 80 ikapeleka mashine ile, equipments zile, zikakaa mwezi mmoja na kitu bila kufanya kazi yoyote. Mwisho zikaondolewa. Kwa hiyo, ukiangalia usimamizi wa vyombo vyetu ni hafifu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiingii akilini kwamba unawezaje kutoa mitambo Dodoma uipeleke Ndungu ikae mwezi mzima na zaidi, machine iko pale yame ku tide up, wafanyakazi wako pale hawalipwi au watalipwa na hela ya Serikali, lakini kazi haifanyiki. Maana Shilingi milioni 80 Halmashauri haijatoa. Sasa hapo tunajiuliza, hivi kweli are we serious? Are we serious kwamba tunataka kulima kilimo kikubwa, lakini cha hawa wadogo ambao miaka yote hii ndiyo wametubeba, tumeshindwa kukilima!

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia shirika letu la NFRA haliweki akiba ya mpunga au maharage au mbegu za alizeti, at most inaweka tu mahindi na nafaka nyingine inaitwa mtama. Sasa ukiangalia wananchi wengi wanakula wali, halafu NFRA haiweki hiyo kama akiba. Pamoja na upungufu uliyooneshwa jana, juu ya kwamba NFRA inakuwa na akiba ya kama siku tatu na nusu, hata huo mpunga haupo kwenye list. Sasa unajiuliza, hivi nchi yetu tunakwenda wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri kwamba Mheshimiwa Waziri hebu u-rethink kwamba hivi hii BBT kweli itafanikiwa kwa approach hii tunayokwendanayo? Tuko too theoretical in the sense that BBT au block farming inahitaji a lot of mechanization. Sasa hivi ukimchukua tu kijana uliyemchukua mtaani umfundishe miezi minne halafu umpe kazi kubwa kama hii I don’t think kama tutafanikiwa. I wish tungechukua mashamba karibu na wenyeji wenyewe tukawa-identify wale vijana ambapo maeneo yale wanajihusisha na kilimo, wakapewa hiyo kazi, wakafundishwa, because at least wana A, B, C ya kilimo na itakuwa kwenye Mkoa ule au Wilaya ile. Kwa hiyo, hata kijana aki-abscond, wapo watakaoendeleza. Sasa tunawatoa Mikoa mingine, tunawapeleka mikoa mingine. Kesho hali yake ya kifedha imekuwa nzuri, anaamua kuacha lile shamba, unamfanya nini? Unamfanya nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, yangu ni hayo machache kwamba hebu tu-rethink approach ya hii block farming kwamba tumejiandaa vipi? Kwa gharama hizi zilizotajwa, kwa kweli sidhani kama ni sustainable, ahsante sana.