Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Afya

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Afya

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, napenda kutoa pongezi za dhati kwako kwa kunipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya makadirio na mapato ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na hatimae kuiwasilisha hotuba hii katika Bunge lako tukufu kwa ufasaha na umakini mkubwa.

Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo; nikianza na upungufu wa dawa nchini.

Mheshimiwa Spika, napenda kuipongeza Serikali yetu inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoongoza nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, matatizo ya upungufu wa dawa katika nchi yetu ni ya kusikitisha sana. Tatizo hili ni kubwa na linakera sana. Serikali inajitahidi sana kutoa pesa kwa madhumuni ya ununuzi wa dawa lakini bado ufumbuzi wa suala hili ni kubwa. Ushauri wangu katika jambo hili kwa Serikali ni kuweka mikakati madhubuti ya kuwadhibiti maafisa wetu wanaohusika na manunuzi ya dawa ili kuwachulia hatua za kinidhamu na kisheria ili kukomesha kabisa suala hili.

Mheshimiwa Spika, pili ni kuhusu chanjo; naipongeza Serikali yetu kwa kuendelea kuratibu upatikanaji wa chanjo pamoja na kuhakikisha chanjo na vifaa vya kutolea chanjo vinapatikana katika mikoa yetu yote. Hili ni jambo zuri sana katika nchi yetu. Naomba Serikali yetu iendeleze suali hili.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu katika jambo hili kwa Serikali ni kueneza elimu ya faida ya chanjo hizi katika jamii hasa wananchi wa vijijini.

Mheshimiwa Spika, tatu ni upungufu wa wafanyakazi katika vitu vyetu vya afya. Napenda kuipongeza Serikali yetu kwa jitihada kubwa inayochukua kwa kueneza huduma za afya nchini kwa kujenga vituo vya afya maeneo yote nchini. Hudumu ya afya ni miongoni mwa huduma muhimu sana kwa binadamu. Vituo vingi vimejengwa lakini bado inaonekana kuna upungufu wa wafanyakzi katika maeneo kadhaa nchini.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu katika jambo hili kwa Serikali ni ujenzi wa vituo hivi ni vema ukaenda sambamba na kuongeza wafanyakazi ili kuboresha huduma hii. Wafanyakazi wa sehemu zote (idara) pamoja na madaktari ni vyema wakawa wa kutosha kabisa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.