Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Afya

Hon. Janejelly Ntate James

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Afya

MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Spika, nami namshukuru Mwenyezi Mungu kupata fursa ya kuchangia kwa maandishi katika Wizara ya Afya. Nimshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi za makusudi anazofanya kwa ajili ya kuimarisha huduma ya afya hasa afya ya mama na mtoto.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Ummy Mwalimu ambaye amekuwa mwalimu kama jina lake lilivyo hasa kwa masuala ya afya, tunakuamini endelea kumsaidia Mheshimiwa Rais. Pia nimpongeze Naibu Waziri Mheshimiwa Dkt. Mollel kwa jinsi anamsaidia pamoja na wataalam wote wa Wizara.

Mheshimiwa Spika, niombe sasa nijikite kwenye mchango wangu katika Kiwanda cha Viuadudu kilichopo Kibaha, Pwani. Suala kubwa katika kiwanda hicho ni soko na mnunuzi mkuu ni Wizara ya Afya. Kwa msingi huo naomba kushauri yafuatayo; Wizara ya Afya na TAMISEMI wasukumwe kusaini mikataba wa manunuzi; ili mkataba utekelezwe Wizara ya Afya itenge bajeti kuendana na mahitaji na Wizara ya Fedha itoe fedha kwa mchanganuo utakaoianishwa kwa manunuzi ya kila mwezi; na fedha ya ithibati itolewe ili kiwanda hiki kiweze kupata soko la nje;

Mheshimiwa Spika, haya yakifanyika lengo la kiwanda hiki na nia ya kujengwa itaonekana.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja.