Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Afya

Hon. Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Afya

MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Awali ya yote kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kunijaalia kuwa na hali ya uzima na afya, kufika hapa leo katika ukumbi wako huu Tukufu na kwamba hivi sasa naweza kuchangia Wizara ya Afya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru mwanangu Mheshimiwa Ummy Mwalimu anafanyakazi vizuri, anaupiga mwingi, usemaji wa vijana anaupiga mwingi Waziri wangu Ummy Mwalimu, Mwenyezi Mungu akujaalie pamoja na Naibu wako anafanyakazi naye vizuri mpaka anawasaidia na watu wengine ili kupata matibatu katika hospitali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninamshukuru na Mama yangu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ndugu yangu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yeye kwa kuupiga mwingi, kila pembe, kila rika, kila mahali ameingia. Mwenyezi Mungu amjaalie kheri na baraka, ampe uzima, amuondolee nuksi, amuondolee kila dhiki ili ampe uzima aweze kuendelea mbele. Ahsante sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuendelea kuna baadhi ya Vituo vya Afya vinafanyakazi vizuri sana, lakini kuna baadhi ya Vituo vya Afya ukiingia katika vituo vile kwenda kutafuta huduma wahudumu wanakuwa wanajisikia sijui kama mtanielewa. Wanajisikia sana mtu unamkuta unakwenda una muulie ile hali kukuitikia hawezi. Mheshimiwa Waziri hawa watu wapo, bado juu ya utekelezaji mkubwa wa Serikali yangu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini hawa watu wapo wanajisikia, mtu anaweka miguu juu ya meza anataka ahudumiwe tena kwa kipimo tu cha presha, namuuliza wewe mfanyakazi, ana niambia ndiyo, sasa kwa nini umeweka miguu juu kama hivyo? Wapo watu kama hao leo nasema katika Wizara katika wizara hiyo Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie kuhusu suala la presha, sukari pamoja shinikizo la damu. Hili suala lipo siku nyingi sana mimi nataka kulingumzia. Walengwa wengine tupo humu humu katika masuala hayo. Nasema haya kwamba shuhuda ninayo, kwamba kuugua ugonjwa wa sukari pamoja na presha unaua na unaumiza na hasa kwa wanyonge wale waliokuwa hawana fedha. Wanakwenda kupima sukari, wanapata maradhi ya sukari, lakini huduma kujihudumia hawana. Ukiingia kwenye masuala la bima, ukienda ukitaka dawa unaambiwa uongeze fedha ili uweze kupata dawa uende ukahudumiwe, hapo mgonjwa mnyonge atapona kweli? Hatapona. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo, naomba Wizara hii au naomba Wizara yangu ya Afya nchini ifanye kazi kwa wanawake hasa tunaoathirika na masuala ya presha, sukari pamoja na shinikizo la damu. Maana ukiingia kwenye masuala ya sukari na presha kwa wanaume ndiyo yanaumiza nguvu kabisa, kwa wanawake ndiyo wanaleta ugomvi ndani ya nyumba hawawezi kwenye masuala la ndoa. Sukari inaumiza, inaharibu huwezi kulifanya tendo la ndoa wakati wewe binadamu umeumbwa ukae na mwenzio ili uweze kulifanya lile, hamu iko wapi kutokana na sukari? Hamna. Tujitahidi jamani suala la sukari na shinikizo la damu linaumiza na litatuumiza kwa sana hata sisi wanawake. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la saratani. Suala la saratani lipo nalo vilevile linaumiza kwa wanawake hasa kwenye kizazi cha wanawake. Hili mimi limenigusa mwenyewe ndani kwangu yupo mgonjwa huyo, lakini nashukuru Serikali hili suala linaweza kufanya na mtu akapona akawa mzima wala asijue hasa kama mimi nilipata maradhi ya saratani. Kwa hiyo, naomba Wizara hii ichukue jitihada kubwa sana ya kuweza kuwahudumia wagonjwa wa saratani kwa hali na mali ili waweze kufanyakazi vizuri na kuweza kujihudumia. Maana magonjwa ya saratani, kuna mtu katibiwa mzima na kaolewa na mumewe hivi sasa anakwenda na shughuli zake na pilika zake. Kwa hiyo, mimi Wizara hii niishukuru sana na niipongeze sana, inafanyakazi vizuri bila wasiwawasi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwenye Wizara hii ya Afya. Ahsante sana. (Makofi)