Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji

Hon. Dr. Alfred James Kimea

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na mimi kunipa nafasi hii kabla sijaongea vitu vyangu vya jimboni naona Mheshimiwa Esther mchango wake uliopita amegusia kidogo kitu ambacho nilitaka kushauri Wizara. Waheshimiwa Wabunge wengi wamesisitiza na wakaonesha kama upo uwezekano wa kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka Dodoma; kwa ajili gani tusifikirie kuchukuwa maji kwenye vyanzo vyote vikubwa nchi hii tukavisambaza nchi nzima? Kwa ajili gani tuendelee na vyanzo vidogo vidogo ambavyo havina uhakika nilikaa chini nyumbani mwenyewe nikaanza kufirika na kupiga mahesabu? Nikahisi tufanye kitu kimoja.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri naomba hili ulichukuwe Katibu Mkuu wetu yupo aandike hiki kitu ninachotaka kukishauri Serikali Mheshimiwa Waziri naomba uandike kaka yangu tukae chini tutengeneza business proposal kiasi gani kitatu-cost kuchukuwa maji kutoka vyanzo vyote vikubwa nchi hii, kusambaza nchi nzima kiasi gani kitatutosha kutengeneza treatment plant ambazo zitatosha nchi nzima na kiwango gani cha pesa kitaweza kusambaza mabomba nchi nzima kumaliza ili tatizo kwa wakati mmoja (at once)?

Mheshimiwa Spika, nafahamu hatuna fedha hizo, lakini business proposal hiyo i-identify source of fund, twende tukakope. Nina imani kabisa tukikopa fedha hizo namba moja tutaweza ku-repay ule mkopo kwa kuwa watu watakuwa nchi nzima wanalipa bili za maji na revenue kutoka kwenye maji zitaongezeka, nimepiga mahesabu zitaongezeka mara tano.

Mheshimiwa Spika, tumeambiwa hapa kuna upotevu wa maji asilimia 30 mpaka 45. Kwenye huo mfumo mpya ninaamini kabisa tutakuwa na upotevu wa maji chini ya asilimia 10, kana kwamba tutaweza kuokoa revenue tutaweza kulipa mkopo huo.

Mheshimiwa Spika, nimepiga mahesabu, kwa mfano mwaka huu tumetenga milioni 700. Nina imini bajeti ya Wizara ya Maji kuanzia kipindi hicho ambacho kila Mtanzania atakuwa na maji tutatumia sasa hiyo bajeti ya maji kulipa mkopo na tutakuwa tumeondoa tatizo la maji kabisa nchi hii, na inawezekana Mheshimiwa Waziri. Mimi niko tayari kama utanihitaji. Unafahamu mimi ni mtalaam wa masuala ya fedha, nitashirikiana na wewe au wataalam wengine wa Wizara yako tuweze kutengeneza hiyo business proposal, tuiuze ili tutatue tatizo la maji nchi nzima kwa wakati mmoja. Nakushukuru sana.

Mheshimiwa Spika, naomba nirudi jimboni kwangu. Ninamshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa miradi mikubwa ambayo ameileta jimboni kwangu. nimshukuru Mama yetu Samia Suluhu Hassan, kwa kipindi kifupi ambacho ni Mbunge umenipatia milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa maji kwenye Kata ya Bagamoyo, umenipatia fedha kwa ajili ya kumalizia ule mradi ambao unaitwa chechefu wa Longela Relini na Darajani na mwezi huu maji yatatoka. Pia mradi ambao una thamani wa 1.6 bilion uko kwenye hatua za manunuzi tunakushukuru sana.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo bado zipo changamoto chache kwenye Kata ya Kwamsisi, maji yapo lakini ya chumvi Kata ya Manundu Majengo mabomba ni chakavu sana ni yale mabomba ya chuma ambayo yametengezwa tangu mwaka 70; ni chakavu yanavujisha maji sana mjini watu wanakosa maji. Kwenye Kata za Masuguru, Magunga, Mtonga Road Korogwe Mgombezi na kwa Mndolwa wanapata maji kwa shida sana.

Mheshimiwa Spika, lakini ninafahamu, ni imani yangu, na ni imani ya watu wote wa Korogwe kwamba huu Mradi wa Miji 28 ambao ulioasisiwa miaka nane iliyopita nakumbuka kwenye jimbo langu Mbunge alikuwa kaka yangu Nasri; lakini leo baada ya miaka nane tunaenda kuufanyia kazi mradi huo. Nimpongeze Mheshimiwa Waziri, pia nimshukuru Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kutuhakikisha mradi huo unafanyika.

Mheshimiwa Spika, imani yetu, imani ya watu wa Korogwe, tunaamini mradi huo utaleta maji Korogwe, utaenda kutengeneza matenki sehemu zote zinazohitajika kupelekwa maji, utasambaza mabomba kwenye kata zote na vitongozji vyote na mitaa ya mji wetu. Ninaamini pia mradi huu utatengeneza vizimba vya kuchotea maji kwa wale wananchi wetu ambao hawana uwezo wa kuvuta maji nyumbani mwao.

Mheshimiwa Spika, tulikuwa tumeambiwa mradi huu utatuletea tu maji kusambaza tutajua wenyewe lakini ndugu yangu juzi umenihakikishia, kwamba mdogo wangu si kweli mradi utaleta maji Korogwe na utasambaza na kihistoria ya changamoto ya maji Korogwe itakuwa imeishia hapo. Mheshimiwa Waziri nakushukuru sana, nilikuwa na hayo mawili machache nataka kuunga mkono hoja, Mungu akubariki sana endelea kuchapa kazi na kupambana sisi ndugu zako tuko nyuma yako. Ahsante sana. (Makofi)