Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji

Hon. Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii ili na mimi niweze kutoa mawazo yangu na mchango wangu kwenye Wizara hii muhimu sana, Wizara ya Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri na Naibu wake kwa kazi nzuri wanayofanya, lakini culture waliyonayo, kwa maana hierarchy ya Wizara yao yote ni wasikivu, Katibu Mkuu, Meneja wangu wa Mkoa ndugu yangu Boaz, unafanya kazi nzuri na Meneja wa SUWASA ndugu yangu Nzoa na Meneja wangu wa Wilaya, Maganga. Kwa kweli kazi yao ni nzuri, wanatupa ushirikiano mzuri kiasi kwamba, tunafurahia sana huduma katika Wizara yako hii ya Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitaanza kwa shukrani kubwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwanza kwa mile stone tuliyopiga kwenye miradi ya maji. Kwa muda mfupi nimeingia kama Mbunge nimeweza kushuhudia maajabu. Ajabu ya kwanza ambalo nitalisema kwako na kwa moyo mkunjufu ni mradi ule wa Ziwa Dogo la Kwela ambako sasahivi mko kwenye final stage ya kusaini mkataba wa bilioni tano. Utahudumia Kata za Kalambanzite, Lusaka, Laela, Nyangalua na Mnokola. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuombe sana Mheshimiwa Waziri tumepata fedha hizi bilioni tano ni za mwanzo tu, lakini umuhimu wa mradu huu uta-justify na investment hii kwa sababu return ya hii investment ni pale tutakapofikisha maji haya katika Mji Mdogo wa Laela, Mnokola na Miandalua. Sasabu hii ya kusema ni nini, tuna chanzo kile kimeishiwa nguvu, ambacho Serikali iliwekeza bilioni 2.6 pale kwenye Mji Mdogo wa Laela umefika mara nyingi na badaye kukatokea mgogoro mkubwa umechukua miaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pale kuna shida nyingine. Ule mradi mwanzo ulikuwa unatumia system ya solar; mliwekeza kama shilingi milioni mia moja na kidogo kwa ajili ya kununua solar. Solar ziko pale ziko redundant na mara nyingine sisi tunapata shida kupata maji kwenye Mji Mdogo wa Laela kwa sababu moja tu kwamba, umeme tunaotegemea ni wa Zambia. Wakati mwingine inapita hadi wiki mbili hatujapata umeme kwa hiyo, tunakuwa hatuwezi kupata maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nikuombe kwa kauli yao Mheshimiwa Waziri turudi, zile solar zinakaa pale zitakuwa obsolete. Tuzitumie ili zitusaidie ili zitusaidie pale tunapopata shida ya umeme zisaidie ku-pump maji ili wananchi wa Mji Mdogo wa Laela waweze kupata maji. Lakini chanzo cha Kwela ndio kitaenda kumaliza matatizo ya kudumu kabisa kwa sababu ukifika mwezi wa saba na wa nane maji yanakuwa ndoo moja shingi elfu moja mpaka elfu mbili katika Mji Mdogo wa Laela.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pili nishukuru sana Serikali kwa mradi mkubwa wa kihistoria utakaotekelezwa ambao unaitwa Kaoze Group kule Bonde la Ziwa Rukwa. Mradi ule utaleta manufaa makubwa. Nashukuru mmetangaza kuanza na Kata ya Kaoze kwa bilioni moja na milioni 500.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimuombe Waziri, kwa mradi ule wa mamu, ule wa Marekani, ambao umekuja, muweze kupeleka mpaka vijiji vingine 13, kwa maana ya Kata za Kipeta na Kilangawani, ili wananchi wale ambao tangu ulimwengu huu kuumbwa hawajawahi kupata maji safi na salama na hawajawahi kuona maji kutoka kwenye bomba. Nikuombe ndugu yangu Waziri umekuwa ukinipa ushirikiano mzuri na Naibu wako, twendeni tukafanye jambo kubwa kwenye mradi huu wa Kaoze Group ili wale wananchi waweze kuandika historia kwamba, alipita Mheshimiwa Aweso, kama Waziri, alitufanyia miujiza mikubwa ambayo hawajawahi huona. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekee kuna ule mradi wa Bwawa la Ikozi, unalifahamu sana una miana zaidi ya minne bilioni 1.5 tumewekeza pale. Shida iliyopo pale kuna mambo mawili; kwanza kuna mgogoro ule na wale wananchi waliotoa yale mashamba. Nikuombe Waziri kuna mambo waeleweshwe tu wale wananchi, miaka minne hawajaeleweshwa kama kuna fidia au hakuna. Ni kuwaweka tu wapate clarity ya mradi ule utakavyokuwa, wakishajua hawana shida, maana wameshindwa kupata jibu kamili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, twendeni tukawaambie ili pesa ulizoleta hizi karibuni tumesaini mkataba wa bilioni mbili wakaone faida ya hela ya mama bilioni mbili, sio ikatokea bilioni mbili imewekezwa pale muda mfupi tuanze kupata sabotage ya wananchi kwa sababu wana complain kwamba kuna mgogoro kwenye eneo lile la Ikoze. Najua ni jambo dogo kwako utaenda kuli-address ndani ya muda mfupi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nishukuru pia kwa mradi mkubwa sana ambao unaenda kuhudumia Mkunda Group, Kijiji cha Kaengesa, Kianda pamoja na Kijiji cha Itela.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe jambo moja. Kuna vijiji viwili katika mradi huu vimesahaulika na viko njiani; Kijiji cha Katonto na Kijiji cha Kazi. Naomba tunapofanya huu mradi ambao tayari nao umesaini mkataba viwe included ili waweze kao kunufaika nah ii pesa bilioni moja na milioni 700 ambayo mama amewaletea wananchi wa Kata ya Lyangalile na wa Kata ya Kaengesa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa namna kubwa kabisa na Wabunge wenzangu wa Kigoma, Katavi, Rukwa na Songwe wameongea. Mradi ambao utakuwa tiba ya kudumu ya tatizo la maji katika mikoa hii minne ni mradi kutoka Ziwa Tanganyika. Tuombe sana; investment ni kubwa tunakubali, lakini return ya investment hiyo na economies ya scale ambayo itapatikana kulingana na huu mradi itaenda kumaliza tatizo hili na hii miradi midogo ambayo life span yake ni miaka 20 tutaachananayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana pia kwa CSR uliyotoa pale kizungu ndani ya Kata yangu Muze, nakushukuru. Umekuwa kati ya Mawaziri waaminifu; ukipita ukaahidi jambo unatenda, maana kuna jamaa zangu walipita jimboni kwangu wakaahidi CSR miaka mitano, wengine mpaka wameondoka kwenye uwaziri nimesahau kabisa, ila wewe uliahidi ndani ya mwezi mmoja na muda mfupi ukaleta ile CSR. Nikupongeze ndugu yangu Mheshimiwa Aweso kazi yako imetukuka hakika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini mwisho nishukuru pia kwa mradi ule unaoendelea wa Uviko pale Mwadui, Kata ya Mwadui, lakini pesa tuliyotenga kwa ajili ya Kata ya Kasekela. Halikadhalika Ilemba pale kwa mara ya kwanza nao watapata maji ya kutosheleza. Nikupongeze sana Waziri, kwa kweli mimi hayo niliyoyasema ndio nakuomba sana, Lake Tanganyika ndicho kilio chetu, ndio suluhu ya matatizo katika mikoa yetu hiyo minne. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo naomba kuunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)