Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Spika, napongeza sana Wizara kwa kazi nzuri ya kuboresha mitaala; ushauri wangu ni kuhusu kuzingatia na kutafuta njia nzuri ya udhibiti ubora kwa shule zilizopo nchini lakini zinatumia mitaala ya nchi nyingine. Shule hizi zinazidi kuongezeka lakini udhibiti wake ni mdogo na kuna dalili za uholela katika uanzishwaji na usimamizi wake hivyo kuathiri ubora katika utoaji wa elimu katika shule hizo. Mfano ni shule zinazotumia mtaala wa Cambridge.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili naomba sana Wizara isikie kilio chetu cha Jimbo la Kilolo kujengewa Chuo cha VETA. Tayari eneo tunalo na wananchi na halmashauri tupo tayari kushirikiana katika kuhakikisha chuo hicho kinajengwa.