Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Abdi Hija Mkasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Micheweni

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. HIJA ABDI: Mheshimiwa Spika, mimi naomba nijikite kwa kuchangia katika eneo zima la usalama wa nchi yetu kiujumla hususan maeneo ya Zanzibar, maeneo ya Pemba kwa muktada huo naishauri Serikali ione umuhimu wa kununua boti ya kufanyia doria katika upande wa bahari ya Hindi kwa upande wa maeneo yale na boti hii ihusishe askari wa Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Uhamiaji kwa pamoja kwa lengo la kuhahikisha usalama katika maeneo yale umedumishwa.

Mheshimiwa Spika, la pili kuna malalamiko makubwa juu ya haki za askari wetu wanaofariki dunia au wakati mwingine kustaafu, naiomba Serikali ihakikishe kama hawa marehemu basi angalau iwaone hawa warithi wake ili waweze kupata hii haki ya mzazi wao na wao wajue kama mzazi wao alikuwa ni mtumishi sahihi wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, lingine ni kuboresha miundombinu ya majengo pamoja na vitendea kazi; kiujumla kwa majeshi yetu yaliopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani mtihani sana maana unaenda katika Kituo cha Polisi hata kompyuta ya kuwekea kumbukumbu hamna sasa na hili ni tatizo hasa ukiangalia na dunia ilivyo sasa.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali ichukue juhudi za makusudi ilione hili ili angalau hawa askari wetu waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki angalau.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.