Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja ya Dharura (Changamoto ya Kupanda kwa bei za Mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa)

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hoja ya Dharura (Changamoto ya Kupanda kwa bei za Mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa)

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami pia. Ni-declare tu kwamba naunga mkono hoja na ninampongeza sana mtoa hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nadhani kwa sababu mengi yameshaongelewa, nitaongea kwenye mambo kama mawili au matatu. Cha kwanza ni tozo. Nimejaribu kupitia huku na hoja yangu ilikuwa tozo zisifutwe, lakini tujaribu kuona jinsi ya kuzipunguza, kwa sababu haiwezekani nchi iko kwenye crisis, mwezi wa Kumi na Moja mwaka 2021 au mwezi wa Kumi au wherever huko nyuma TBS walikuwa wanapata Shilingi moja au Shilingi mbili na sasa wanaendelea kupata pesa ile ile. Kwa hiyo, nilikuwa naomba kwanza tupunguze even by 50%. Tukiweza ku-cut down by 50% watu waelewe kwamba nchi iko kwenye crisis, wananchi wanaumia, nchi inaumia, Mheshimiwa Rais naye anahangaika; kwa hiyo, tukiweza kushusha even by 50% kwenye zile tozo, zitaweza kutusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, nimejaribu kupitia ile calculation; najua hata Taifa limepitia wakati mgumu sana. Tunatoka kwenye post impact ya Corona, leo tunakuja kwenye mafuta pia. Hawa wanaotuletea mafuta hapa in bulk procurement wana fixed profit, kwamba wakati wa Corona, kipindi dunia imefungwa watu wamejifungia, wao waliendelea kupata faida kwenye nchi hii kwa sababu shughuli zetu zliendelea, leo dunia inahangaika mafuta yanapanda bei, yeye bado anapata fixed profit ile ile. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kuna haja ya ku-revisit hizi profit zao, kwa sababu kuna financial overhead hapa, kwa sababu kulikuwa na financial cost. Yeye kama amekopa, financial cost imekuwa calculated hapa. Kwa hiyo, tunachohitaji, tuongeenao pia, kwamba wewe mwaka 2021 umepata faida ya Shilingi 123 kwa lita, sasa hivi hata wewe kubali kushuka kwa sababu Taifa hili haliwezi kuendelea kuangamia huku wewe ukiwa unatengeneza faida ile ile. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, turudi hata kwao hawa, kipindi tunayaangalia haya, kurudi kwa hawa wafanyabisahara pia, twende sasa kwenye upande wa Serikali. Najua iko miradi ambayo tunakusanya, tunalipa, tunakusanya tunalipa. Kama tutaogopa kugusa kwenye sehemu kama za REA, tutaogopa kugusa kwenye sehemu za maji; hivi vitu vitapanda bei, kwa sababu mafuta yanapopanda bei, costs zikianza kubadilika, tutakuwa na variation kubwa. Serikali itaenda kuwalipa tena wafanyabiashara…

MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Chiwelesa, kuna Taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Godwin Kunambi.

T A A R I F A

MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tozo zinaathiri moja kwa moja bei ya kupanda kwa mafuta, lakini kuna ushindani wa soko. Ushindani wa soko pia unaathiri moja kwa moja kwenye kushuka kwa bei. Hivyo, nadhani ni vyema sasa Serikali ikaruhusu kuwe na uhuru wa kuagiza mafuta na bila ya shaka naamini bei itashuka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Ezra Chiwelesa, unaipokea taarifa hiyo?

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, tumesimamisha Bunge kwa hoja ya dharura. Hayo mambo ni ya baadaye, we are talking about now. Hizo idea tutazitoa baadaye huko, mambo ya kuanza kuagiza; hii ni dharura. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapoongea leo, mimi kwangu Biharamulo mafuta ni shilingi 3,370. Naongelea Biharamulo mjini. Kutoka Biharamulo Mjini kuna wananchi wako kwenye kata ambazo zinaenda kilometa 70 kutoka mjini, yule mwananchi leo mafuta yako shilingi 4,000 yanaelekea shilingi 5,000; bodaboda ndiyo ambulance yao, bodaboda ndiyo usafiri wao. Tunapoongea hapa, tuongee hili jambo kama dharura. Hizo ideas Serikali itupe nafasi tutatoa mawazo huko baadaye jinsi ya kufanya, lakini for now it is an emergency.

Mheshimiwa Spika, tunapoongelea emergency, yaani tunataka Serikali isikie leo, kesho jioni au leo jioni tuje na majibu, kwamba tumesikia na tumeondoa shilingi 200 mafuta yashuke leo. Tukitaka kwenda mwisho wa mwezi, it won’t help us, huenda huko vita itakuwa imeisha, mafuta yatakuwa yameshuka pia. Hicho ndiyo tunachoendeleanacho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninachosema ni kwamba, twende kwenye hali ya udharura, tuone tunafinya wapi, bei zishuke, wananchi wakiamka kesho waamke na tabasamu.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naunga mkono hoja. (Makofi)