Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Madini

Hon. Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Madini

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangia. Kwanza nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma, lakini pia nimpongeze Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ambayo anaendelea kuifanyia nchi hii. Lakini pia nimpongeze Waziri wa Madini Mheshimiwa Doto Biteko pamoja na timu yote.

Mheshimiwa Spika, baada ya pongezi hizo, kutokana na muda nataka nitoe ushauri kidogo kwenye Wizara hii, ushauri wangu wa kwanza ni pamoja na kwamba plants nyingi nchini zinaliingizia Pato la Taifa, plants nyingi za VAT reaching zinalipatia Taifa mapato makubwa sana; ikiwemo Nyangh’wale ambayo tuna plant zaidi ya 100. Uchenjuaji huu una sababisha uharibifu wa mazingira. Ushauri wangu kwamba plant zote nchini ikiwemo na plant za Nyangh’wale Serikali ielekeze kwamba kila plant ipande miti zaidi ya 200 ili kuepusha majanga ya uharibifu wa mazingira.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu wa pili Mheshimiwa Waziri Doto Biteko, uunde tume ili iweze kwenda kwenye mgodi wetu wa Bulyanhulu kufanya uchunguzi wa uchimbaji unaoendelea kule chini. Inasemekana kwamba uchimbaji huu umeelekea zaidi kwenye upande wa Nyangh’wale na siyo Kahama. Watakapobaini kwamba ni kweli uchimbaji huu unaelekea Wilaya ya Nyangh’wale basi tukae chini ili tuweze kurekebisha ushuru ambao tulikuwa tukipata. Kutoka kwenye asilimia 100 Msalala walikuwa wakipata 67 na Nyangh’wale tulikuwa tunapata asilimia 33. Iwapo sasa hivi uelekeo huo utakuwa unaelekea Wilaya ya Nyang’wale itabidi tubadilishe. kwamba sisi tuchukue 67 na Msalala wachukue asilimia 33.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu mwingine ni kwamba, Wizara imeruhusu uchimbaji unaoitwa uchimbaji wa rash maeneo mbalimbali nchini. Sasa kwenye uchimbaji huu wa rash pamejitokeza vikundi ambavyo vinasimamia kukusanya mapato yanayopatikana pale. Kumejitokeza pia vijana ama wananchi fulani wachimbaji wanaojiita wababe wachimbaji ambao wamekuwa wakizivamia zile ofisi za rash ambazo zinakusanya mrahaba wa mawe. Kwa mfano kikundi cha akina mama wachimbaji wadogo wadogo wa Nyangh’wale walivamiwa na kufanyiwa usumbufu mkubwa sana na vijana hawa. Kwa sababu Serikali imeruhusu ofisi hizi zisimamie rash, ninakuomba Mheshimiwa Waziri utoe tamko utundu huo na ujeuri huo unaofanywa na hao vijana uachwe kabisa.

Mheshimiwa Spika, lakini pia nashukuru kwamba hawa akina mama baada ya kuvamiwa namshukuru sana DC wangu pamoja na RMO wamelishughulikia jambo hili na limekaa vizuri wale akinamama wanaendelea na shughuli zao. Hongera sana Mheshimiwa DC kwa kulimaliza tatizo hili. Mheshimiwa Spika, ushauri wangu mwingine, ni kwamba kuna wachimbaji ambao wanapeleka carbon zao kutoka Nyangh’wale kwenda kuchomea Geita mji carbon hizo zinapochomwa Geita na dhahabu inapopatikana, imekuwa kodi zote zinachukuliwa na Geita mji ikiwa mrahaba wa Serikali lakini pia service levy, Wilaya ya Nyangh’wale tunakuwa hatupati service levy kwa sababu wametoka Nyang’wale wameenda kuchomea carbon zao Geita. Takriban zaidi ya milioni 800 zimeng’ang’aniwa na Mji wa Geita. Tunakuomba Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko lisimamie hili ili tuweze kurudishiwa hizo milioni 800 ziweze kuleta maendeleo katika Halmashauri yangu ya Wilaya ya Nyang’wale.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Doto Waziri wa Madini, mwisho kabisa, pesa hizi zimekuwa zikiombwa na zimeleta mgogoro sana. Ni kwanini wanaenda kuchomea Geita? Ni kwa sababu wale wachimbaji wanakuwa hawana uwezo wa kuendesha shughuli zao, wanakwenda kukopa kwa wale matajiri walioko Geita, sasa badala ya kuchomea mzigo huu Wilayani Nyangh’wale, wanabeba ule mzigo kuupeleka Geita wanapochomea. Geita kule kwa wale matajiri wanalipa zile…

SPIKA: Mheshimiwa Hussein Amar kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Kanyasu.

T A A R I F A

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Spika, namheshimu sana Mheshimiwa Hussein na natambua mchango wake. Lakini, kwa mujibu wa sheria ya service levy inalipwa pale ambapo mfanyabiashara anafanyia biashara yake na kwamba Halmashauri ya Mji wamekuwa wakitoza hivyo kwa sababu sisi hatukuwafata Nyangh’wale wanakuja wenyewe nakushukuru sana.

SPIKA: Mheshimiwa Hussein Amar unapokea taarifa hiyo?

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, taarifa hii siipokei. Namheshimu sana mdogo wangu Kanyasu. Wale wanapochukua carbon zao Wilayani Nyangh’wale kwenda kuchomea Geita ni kwa sababu wanapewa mikopo na wale matajiri waliopo Geita. Lakini kwa sababu address ni kwamba ametoka Nyangh’wale tunaomba ile service levy irudi kwetu Nyangh’wale vinginevyo Mheshimiwa Waziri basi uweke zuio la watu kubeba carbon kutoka Nyangh’wale ziende Geita zisiende Geita hizo carbon kwa hiyo tunaomba utusaidie hilo; kwa sababu wachenjuaji wengi wanapeleka Geita kwa sababu wanaenda kukopa kule. Iwapo Mheshimiwa anasema kwamba ni sheria basi hebu kuiangalia hii sheria, tuweke zuio ili carbon isitoke Nyangh’wale ichomewe pale pale Nyangh’wale na isiende Geita.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru, ahsante.