Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Hon. Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza sana Serikali chini Rais Mama yetu shupavu Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea Watanzania maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Waziri wa TAMISEMI, Naibu Mawaziri TAMISEMI pamoja na uongozi wote wa Wizara kwa kufanya kazi nzuri kuhakikisha maendeleo na huduma inasogezwa karibu na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jitihada hizo bado kuna changamoto kwa upande wa afya, elimu, mikopo ya asilimia 10 kwa makundi maalumu. Katika afya bado mkoa wetu wa Manyara tuna jiografia ngumu mno kutoka kata moja kwenda makao makuu ya Wilaya ni umbali zaidi ya kilometa zaidi ya 100 hivyo kuwa na kituo kimoja katika Tarafa bado ni changamoto kubwa mno, mfano katika mkoa wetu kuna tarafa kubwa zaidi ya baadhi ya Wilaya hivyo ombi langu ni kuwa angalau kituo kimoja kila kata, hii itasaidia kupunguza vifo vingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika Wilaya ya Simanjiro hakuna gari la wagonjwa hivyo wananchi wetu wanateseka sana na wengi kupoteza maisha. Tunaomba kupatiwa gari la wagonjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la asilimia 10 ya kina mama, vijana na watu wenye ulemavu nashukuru Serikali kwa kuendelea kuwapatia makundi haya ili kujikwamua kiuchumi, lakini bado asilimia nne kwa kina mama haitoshi ukizingatia kina mama ndiyo wana majukumu makubwa kwenye familia na vigezo vinavyotumika kupewa mikopo inatakiwa kufanyika marekebisho.

Ushauri wangu ni kuongeza asilimia 10 iwe kwa kina mama tu na vigezo vya mikopo isiwe lazima kukopa mpaka vikundi, akinamama wapewe mikopo hata mtu mmoja badala ya vikundi, hii itasaidia kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na urahisi wa marejesho.

Kwa upande wa elimu bado tuna changamoto, ukosefu wa madawati bado kuna watoto wanakaa chini hasa shule za misingi, elimu bora ni pamoja na mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.