Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022

Hon. Dr. Joseph Kizito Mhagama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Madaba

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwa unyeknyekevu kabisa na kwa niaba ya Kamati ya Katiba na Sheria tunawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote na Mawaziri walioweza kuchangia hoja hizi ambazo tumezileta mbele yako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jumla ya Waheshimiwa Wabunge kumi na Mawaziri watano wamepata fursa ya kuchangia moja kwa moja kwa njia ya kuzungumza kwenye maeneo muhimu ambayo Kamati iliyaleta mbele ya kiti chako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maslahi ya muda nisingependa kuwatamka hapa, lakini tulikuwa na mambo kadhaa ambayo yamewekewa mkazo kwa Waheshimiwa Wabunge na nisingepende niende kuyaeleza yote, lakini niweke mkazo katika maeneo machache ambayo yameelezwa; moja, ni Mfuko wa Maendeleo ya Vijana umepata ufafanuzi wa kutosha sana kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge, lakini pia kwa Mheshimiwa Waziri Ndalichako mwenye dhamana katika eneo hilo tunatambua na tunaelewa mabadiliko ya taarifa kwa maana ya kwamba utekelezaji umefanyika baada ya sisi kupita kukagua. Kwa hiyo, tunashukuru kwamba mapendekezo ya Kamati yamefanyiwa kazi kwenye eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja ya lugha ya uandishi; imepewa ufafanuzi mzuri na tunashukuru kwa wadau kuliwekea msisitizo Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali, lakini eneo la nne ni kazi na ajira.

Mheshimiwa Mwneyekiti, hili jambo limepata ufafanuzi mzuri kutoka kwa Mheshimiwa Jenista Mhagama, Waziri mwenye dhamana katika eneo hili, lakini pia wadau upande wa Serikali Mawaziri mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja kubwa ya Kamati na hoja kubwa ya Wabunge tunapotoa ajira za Serikali, ajira ambazo tunaenda kulipa kwa kutumia fedha ya umma tusimlinganishe mtoto aliyemeliza Madaba Day Secondary School na mtoto aliyemaliza Feza Boys na wote tukawashindanisha kwa viwango vinavyofanana na baadae tukajikuta kwamba ajira zote zinaelemea kwa watu wa aina fulani, watu wa aina moja, hiyo ndio hoja ya kamati na ndio hoja ya Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapotoa ajira tufanye allocation kadri ya mikoa, tufanye allocation kadri ya wilaya. Tuna ajira 200; je, mkoa wa Ruvuma ziende ajira ngapi? Mkoa wa Morogoro ziende ajira ngapi ili watoto wa mkoa wa Ruvuma wapimwe kwa viwango vya mkoa wa Ruvuma, la sivyo tutakuja kujenga taifa lenye changamoto kubwa sana na hiyo ndio hoja ya Kamati na hiyo ndio hoja ya Wabunge na nakuomba ikikupendeza Waheshimiwa Wabunge waipitishe hoja hii kama ambavyo imewasilishwa na Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na hoja ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ya Uendeshaji wa Mashauri ya Jinai; Waheshimiwa Mawaziri wamefafanua pia na Waheshimiwa Wabunge wamesema, lakini hoja kubwa ya Kamati ni kuitaka Ofisi hii iheshimu maamuzi ya Mahakama hasa pale ambapo mahakama inatoa maamuzi juu ya watuhumiwa warudishiwe mali zao. Ofisi hii ihakikishe hayo yanafanyika na hiyo ndio hoja ya Kamati na ninaomba Bunge lako liipitishe kama ilivyopendekezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine zimepewa msisitizo mzuri ikiwemo hoja ambayo aliifafanua vizuri sana Mheshimiwa Khadija Taya inayohusu watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya naomba sasa Bunge lako likubali kupitisha taarifa pamoja na maazimio yote ya Kamati ya Katiba na Sheria kama yalivyowasilishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja. (Makofi)

MHE. EDWIN E. SWALLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.