Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022

Hon. Jacquline Andrew Kainja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022

MHE. JACQUELINE K. ANDREA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia taarifa hii ya CAG katika Kamati ya Hesabu za Serikali PAC. Moja kwa moja niweze kuchangia kuhusu ukaguzi wa kiufundi katika ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Kanda na Hospitali za Rufaa za Mikoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa ya CAG inaonesha kwamba hakukuwa na mawasiliano mazuri kati ya Wizara ya TAMISEMI pamoja na ya Afya, ina maana pesa zimeenda Wizara ya TAMISEMI kwenda kujenga yale majengo kwa ajili ya hospitali za rufaa lakini hawajawashirikisha wataalam ambao wako Wizara ya Afya ili waweze kuwapa michoro na ramani nzuri ambazo wanaona kwamba zinafaa na zina sifa za kuwa hospitali. Matokeo yake taarifa hii ya CAG inatuonesha kwamba yale majengo hayana sifa ya kuwa hospitali kwa maana kwamba pesa za umma hazijaenda kuwa na tija, kwa sababu tayari moja kwa moja yale majengo inavyoonekana wataalam watashindwa kuyatumia kwa sababu michoro ile na ramani ile haijaenda sawa pamoja na Wizara ya Afya wanavyotaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile katika eneo hilo hilo, pesa zilizoenda kwa mfano katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ambayo imekwenda kujengwa ni pesa zaidi ya bilioni tano, lakini sasa majengo yale kwa taarifa ya CAG na sisi kama Wanakamati tumeona, beam za majengo tayari zimepinda, lakini vile vile mabati yamepinda, nyufa tayari zimeshatokea. Sasa unaanza kujiuliza, kama pesa imeenda bilioni tano na zaidi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na tayari umepeleka mkandarasi pale, walitumia vigezo gani mpaka yule mkandarasi anajenga vitu ambavyo havieleweke yaani hata kwa mwonekano, hata nyumba ya mwananchi hawezi kujenga beams zimepinda, mabati yamekaa shaghala baghala, kuta tayari zina nyufa. Hizi ni pesa za wananchi ambao ni walipakodi, wananchi wanyonge, Serikali tunakaa hapa tunapitisha bajeti, Wizara inachukua pesa, inaenda site kutuletea matokeo ambayo yanasikitisha na yanatia uchungu kwa matumizi mabovu ya pesa za wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nihamie katika suala hilo hilo katika kipengele cha ukiukwaji wa sheria za manunuzi. Kwa mfano, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambayo imejengwa Consultant hakuleta performance security bond. Sasa kama Consultant hajapeleka performance security bond, maana yake ni kwamba yule consultant asipoweza kufanya ile kazi, wewe Serikali unaweza ukambana kwa kupitia kitu gani? Utarudisha vipi zile pesa? Tayari tutakuwa tumeshapoteza hizo pesa na kama wamekiuka kifungu cha Sheria 58(1) cha Sheria ya Manunuzi ina maana wale watu hawako serious na kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba watu hawa wanaofanya business as usual katika pesa za wananchi kutuletea hasara, kutupigisha mark time hapa, kila siku tutakaa hapa tunapitisha pesa, watu waende site, matokeo yanayokuja, CAG anakuja na mambo ambayo hayaeleweki, mwisho wa siku wanaoumia ni wananchi. Kwa haya yaliyofanyika katika Hospitali hizi za Rufaa za Kanda ambazo CAG ameweza kukagua na kuona kwamba ufanisi wa majengo haya haukidhi vigezo, basi sasa wale Wakandarasi au watu ambao wamechukua mkataba huu wa kutujengea zile gharama ziwe juu yao. Majengo yale yabomolewe, wajenge kwa gharama zao wao wenyewe, sio tena kesho na keshokutwa tukae hapa tuambiwe tunapitisha bajeti ya ukarabati wa majengo ambayo tayari tulishapitisha, tunategemea kazi nzuri ije mikononi mwetu, inakuja kazi ambayo haina viwango. Kwa hiyo gharama iwe juu yao na sio juu ya wananchi wanyonge, wanalipa kodi, biashara zenyewe ni ngumu, watu wanahangaika kutafuta ada za watoto wao, kodi zinakatwa kila kukicha, kodi nazo ni nyingi, leo tena tuna kazi ya kujenga hospitali kila kukicha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hayo machache, naomba kuishia hapo kwa sababu ya muda. Ahsante. (Makofi)