Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022

Hon. Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, nami nikushukuru sana kwa kunipa nafasi. Nianze kwa kusema, hili suala la ukosefu wa ajira kwa vijana wetu limekuwa ni changamoto. Sasa kutokana na hilo, naipongeza sana sana Wizara ya Kilimo kwa kuanza mpango wa kupokea vijana wanatuma application, wanawa-enroll ili baadaye hao vijana wote wawapatie skills au mafunzo ya kilimo, nafikiri ni kilimo cha umwagiliaji, halafu baadaye wawape vifaa, yaani matrekta na pembejeo ili waanze vile vitu mnavyoita block farms.

Mheshimiwa Spika, sasa naiomba Wizara, hii link mnayoituma ili hao wanafunzi au hao vijana watume application, nafikiri vijana waliopo mijini watafaidika sana. Sasa nilikuwa nawaza kwamba ni vizuri ili vijana wote walioko katika wilaya zetu wapate hii taarifa, basi hizi taarifa au link ipelekwe mawilayani. Wakuu wa Wilaya au Wakurugenzi wajue kuzituma katika Wilaya zao ili vijana wote wafanye hiyo application. Kwa sababu idadi hii mliyoipata ya karibu wanafunzi 16,000 inaweza ikaongezeka. Kwa hiyo, hilo litasaidia sana pia kupunguza hilo tulilosema la ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, niseme hivi, kama Wizara ya Kilimo imeweza kufanya hilo jambo, kwa nini Wizara nyingine hizi mbili ambazo nazo zinafanya kazi ya production wasifanye kama Wizara ya Kilimo? Mfano, hii Wizara ya Mifugo, kwa nini na ninyi msifanye hivyo ili tuwe na hizo blocks za mifugo? Wizara ya Viwanda na Biashara kwa nini na ninyi msifanye hivyo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Viwanda na Biashara mkichukua wanafunzi 10,000, Wizara ya Mifugo nayo ikachukua wanafunzi 10,000, kwa kufanya hivyo Wizara hizi tatu zinaweza zikasaidia sana sana kupunguza hili wimbi au manung’uniko ya changamoto ya ajira. Kwa hiyo, naomba hizi Wizara mbili zifanye kama wanavyofanya hawa Wizara ya Kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni kuhusu mbolea. Kuna wakati nimesikia kwamba mbolea hizo zitakwenda kwenye maeneo, na centers za kusaidia kupeleka mbolea zitaongezeka. Niseme tu, hata mkiweka hizo centers Wizara ya Kilimo kwa sababu tunaleta Kilimo cha Umwagiliaji, naomba sana hiyo mbolea ipatikane throughout. Tukisubiri tu wakati wa msimu ule wa mvua, ndiyo maana kunakuwa na changamoto ya wakulima kunyanyasika, kuibiwa pesa zao na mbolea yenyewe kuuzwa kwa namna ambayo haipendezi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni vizuri sasa mbolea ikawa inapatikana wakati wote, tusisubiri tu wakati wa msimu wa kilimo. Kwa sababu tunatengemea kuanzisha Kilimo cha umwagiliagi, basi hiyo mbolea ipatikane wakati wote na hiyo itapunguza sana changamoto za upatikanaji wa mbolea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)