Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

Hon. Janejelly Ntate James

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuchangia siku ya leo.

Nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai na afya, nitakuwa mwizi wa fadhila nisipomshukuru Mheshimiwa Rais, kwa niaba ya Vyama vya Wafanyakazi kwa jambo alilolifanya la wenzetu waliyopata ajali ya kughushi vyeti kuruhusu walipwe akiba yao waliyokuwa wakichangia wao wenyewe ni jambo la kiungwana sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile najikita kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha, kuhusu Mpango na Maendeleo aya ya 33 kipengele cha Nne, wanasema watachochea maendeleo ya watu hasa kwenye elimu, afya, maji na ardhi. Leo naenda na elimu na afya. Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ameonyesha nia thabiti ya kupigana na umaskini, ujinga na maradhi na ndiyo maana sasa hivi nchi nzima tuna zahanati 5,123, vituo vya afya 650, shule za msingi 17,181 na sekondari 4,211, hizo zinamilikiwa na Serikali tu. Hata hivyo hivi vyote havitakuwa na maana kama hatuna rasilimali watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mahitaji ya wataamu wa afya ni 126,294 waliopo ni 61,304 pungufu ni 64,960, sawasawa na asilimia 52. Lakini upande wa walimu shule za msingi mahitaji ni 299,210, waliopo ni 167,245 pungufu ni 131,965 sawa na asilimia 44 hizo ni shule za msingi. Vilevile walimu wa sekondari wanahitajika 174,632, waliopo ni 84,700 pungufu ni 89,332 sawasawa na asilimia 51.1.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila kuwa na rasilimali watu hii hakuna tutakachofanya na ninaona huruma kwa hela tulizoweka kwenye zahanati na shule hasa tulizojenga na COVID. Kama hakuna walimu shule zile zitageuka magofu, zile zahanati zitakuwa magofu. Haiwezi kuwa zahanati kama haina wataalamu na wale wanaoenda kutibiwa pale na bila kukazania hivi vitu adui umasikini hatutomtoa Tanzania. Naomba na nimeangalia mpango mnasema mtawaboresha watumishi lakini hamjasema mkakati thabiti wa kuajiri walimu na watalaam wa afya na hawa ndiyo wakuhudumia hivi vitu nilivyovitaja. Ninaomba huu mpango uoneshe mwaka huu kuna mkakati gani wa kuongeza kada hizi za watalaamu wa afya na walimu wetu ili hayo majengo yasije yakageuka magofu na hela tuliyoweka huko ikapotea kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe bajeti hii ituonyeshe ajira, itoke tu tutoe bajeti ya mwaka mmoja tuseme mkakati ni kuajiri walimu na watalaamu wa afya tu ili tuweze kupunguza hii asilimia hamsini na mbili na asilimia arobaini na moja. Nilikuwa na ushauri tu, ushauri wa kwanza ni hiyo Serikali kuweka mkakati wa namna ya kuajiri hizi kada mbili ili tuweze kufikia malengo tuliyoyaweka, pendekezo la pili Halmashauri zinazo vyanzo vya ndani vya mapato waruhusiwe watalaam wako wengi mtaani, waajiri kwa mkataba ili kuziba pengo hili ili tuweze kumsaidia Mama Samia Suluhu Hassani kufikia nia yake yakufuta masikini, ujinga na maradhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu ni huo leo, ahsante sana. (Makofi)