Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii jioni hii ili nami nitoe mchango wangu katika Kamati hizi tatu za PAC, PIC na LAAC. Aidha, napenda kuwapongeza Wenyeviti wote wa Kamati tatu hizi pamoja na wajumbe wao wote kwa namna walivyotayarisha na hatimaye kuwasilisha ripoti zao katika Bunge lako Tukufu kwa ufasaha wa hali ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mengi yamezungumzwa. Mimi katika mchango wangu wa leo nitachangia kuhusu ukiukwaji wa taratibu za uendeshaji kazi katika wizara, idara na mashirika yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli, ni jambo la kusikitisha sana kuona kwamba, baada ya miaka 60 yetu ya uhuru bado kuna idara zetu na mashirika yetu yanafanya kazi kwa kukiuka taratibu. Hasa inasikitisha zaidi unapoona kwamba yanayofanyika na wanaofanya haya ni wale ambao wanatakiwa wasimamie utaratibu ule; ni jambo la kusikitisha sana.

Mheshimiwa Spika, katika Ripoti ya CAG imeonekana kwamba Lindi Regional Police Commander walimkodia OCD wao ofisi kutoka National Housing kwa malipo ya 1,770,000/=. Katika hili polisi walikuwa wanalipa pungufu; 1,770,000/= wao walikuwa wanalipa 1,500,000/=. Kwa hiyo kulikuwa kuna bakaa ya kama 200,000/= kila mwezi. Hii ime-accumulate fedha jumla ya milioni 37 ambazo mpaka sasahivi hawajalipa.

Mheshimiwa Spika, lakini issue si hiyo, issue ni kwamba hakukuwa na mkataba baina ya Polisi na National Housing, mambo yalikuwa yanakwenda kihivihivi tu. Ndipo pale ninaposema kwamba inasikitisha zaidi kuona kwamba wale wasimamizi wa sheria ndio ambao wanavuruga sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mchango wangu wa pili utakwenda kwenye kutekeleza hoja za ukaguzi. Asubuhi hii kuna mjumbe mmoja, Mheshimiwa Tarimba, alisimama akaeleza namna ya dharau watendaji wetu wanavyodharau. Katika Ripoti ya CAG imeonekana kwamba, katika kipindi cha 2019 Jeshi la Polisi walipewa hoja 13 na CAG, lakini mpaka kufikia hii leo hapa tulipo wametekeleza hoja tatu tu. Kwa hiyo, hii ni ile dharau, kwamba wao wanadharau maelekezo hata ya CAG. Wamepewa hoja 13 wametekeleza tatu tu mpaka hii leo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu na la mwisho ni kuhusu kutokutekeleza hata ile mipango yao wanayopanga. Katika uchunguzi wa CAG imeonekana kwamba National Housing katika mipango yao ya 2015/2016, katika strategy planning yao, walijipangia wenyewe watengeneze kampuni tanzu ambayo itawasaidia kwenye mambo yao ya uendeshaji, lakini mpaka hii leo tuko hapa kampuni tanzu hii hawajafanya na zoezi hili bado linasuasua.

Mheshimiwa Spika, mimi kwa haya yangu matatu niliyochangia naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)