Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Mkataba wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Ugaidi ya Mwaka 2004

Hon Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Mkataba wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Ugaidi ya Mwaka 2004

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nikushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia hoja ya Itifaki iliyowasilishwa na Mheshimiwa Waziri wangu Engineer Masauni mchana huu, lakini nianze pia kwa kuwashukuru katika vitu ambavyo vimetupa unafuu sana leo tunapojadili Itifaki hii karibu wasemaji wote wamekuwa-positive wameunga mkono hoja nasi kwa kweli tunawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi tunaridhika na yote yaliyotolewa kwa maana ya kuunga mkono hoja yetu, zaidi na ushauri mbalimbali uliotolewa. Kuna maangalizo kadhaa yametolewa ningetamani kugusia machache kadri ya muda ulionipangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wachangiaji wengi wamerejea manufaa, ambapo wazungumzaji karibu wote wamerejea manufaa kama yalivyoainishwa na mtoa hoja kwenye ukurasa wa 10, ukurasa wa Nane aya ya 10 ambapo amechambua hoja karibu 11 zinazosema manufaa ya kuunga mkono ama kuridhia Itifaki hii. Kwa hivyo, tunashukuru nimeona Mwenyekiti wa Kamati pia amerejea manufaa haya, kwa hiyo manufaa kwa kweli ni makubwa kwa sababu, tayari kama nchi tunayo Sheria ya Kuzuia Ugaidi lakini tulikuwa tumesimama nchi kama nchi, lakini kama wasemaji wengi walivyozungumza masuala ya ugaidi huvuka nchi moja kwenda nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania watakuwa wanakumbuka na Waheshimiwa Wabunge mtakuwa mnakumbuka kwamba, hivi karibuni kumekuwa na matukio yametokea karibu na mpaka wetu na nchi ya jirani kule Mozambique. Kwa hiyo, utaona uhalifu unafanyika Tanzania wanakimbilia kule, kwa sababu bila ushirikiano wahalifu wanaokimbia nchi jirani utawafanyaje? Kwa hiyo, ni lazima kuwa na Itifaki ya namna hii inasaidia fursa kama hizo za ushirikiano baina yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya Wabunge wametukumbusha na mimi nalipokea, lakini tuwape tu assurance ni kwamba nchi yetu ipo makini, hatuwezi kwa sababu nchi moja au mtu mmoja kasema huyu hana sifa hizi mumuondoe Tanzania na sisi tukafuata na ndiyo maana kwa kulizingatia hilo tumechukua muda kujiridhisha na hadi tunapoleta Itifaki hii Bungeni tumejiridhisha kwamba tunachokwenda kufanya ni cha uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtakumbuka Waheshimiwa Wabunge miaka kadhaa iliyopita ziko nchi zilikumbana na changamoto za vikundi na kutaka ku- blacklist vikiwemo zile zinavyotoa huduma kwenye nchi yetu, lakini Serikali ya Tanzania haikukurupuka kufunga huduma zile tu kwa sababu nchi Fulani ilisema shule fulani, zahanati fulani kwa sababu ipo hivi ifungwe! Ni kwa sababu tulifanya uchunguzi wa kujiridhisha hakuna dalili zozote za kuonesha vitendo vya ugaidi kwenye eneo hili, kwa hilo nalo litaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo nchi zilikumbana na changamoto za vikundi na kutaka ku-blacklist vikiwemo vile vinavyotoa huduma kwenye nchi yetu, lakini Serikali ya Tanzania haikukurupuka kufunga huduma zile kwa sababu tu nchi fulani ilisema shule fulani, zahanati fulani kwa sababu iko hivi ifungwe. Ni kwa sababu tulifanya uchunguzi tukajiridhisha hakuna dalili zozote za kuonesha vitendo vya ugaidi kwenye eneo hili. Kwa hiyo hilo nalo litaendelea na polisi wetu watajiepusha, kwa sababu hata Waziri alivyokuwa anaisoma alisema tutazingatia matakwa ya katiba, kuzingatia haki za binadamu ikiwemo kuepuka kubambikia watu wasiohusiana na makosa hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na hiyo inatukumbusha, mara kadhaa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, amevikumbusha vyombo vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutokubambikia watu kesi. Kwa hiyo hayo yanakwenda hadi hayo yatakayozungumzia masuala ya ugaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia naomba na mimi niunge mkono hoja hii, kwamba Bunge kwa pamoja turidhie Itifaki hii ili tuweze kuungana na nchi nyingine 21 ambazo zimeweza kuridhia kwenye nchi zao ili tunufaike na uwepo wa Itifaki hii pamoja na wanachama wenzetu wa OAU.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)