Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

Hon. Bakar Hamad Bakar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii ya kuweza kunipa fursa nami kuweza kuchangia kwenye hoja ya Kamati yetu ya PAC.

Mheshimiwa Spika, kabla ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa neema yake ya uzima na uhai ambao anaendelea kutujalia hadi sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikupongeze wewe binafsi pamoja na Naibu Spika kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi za kishindo na kuweza kushika nafasi ambazo mko nazo. Nikuombeeni kwa Mwenyezi Mungu afya njema lakini busara na hekima ziendelee kuwaongoza katika uongozi wenu.

Mheshimiwa Spika, pia niipongeza Kamati yetu ya PAC lakini kipekee nimpongeza Mheshimiwa Mwenyekiti mama Kaboyoka kwa namna ambavyo ameweza kuiwasilisha ripoti hii kwa ufasaha sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye ripoti hii, nitaelekeza michango yangu kwenye kuanzia ukurasa wa 20–24 kwenye ripoti ya Kamati ya PAC. Ukurasa huo unaelezea namna ya ukaguzi uliofanyika kwenye Mamlaka ya Mapato ya TRA. Kwa kweli ukusanyaji wa mapato ndiyo jambo ambalo linaiwezesha Serikali kuweza kutimiza mipango ambayo Bunge lako Tukufu inaipitisha kila mwaka. Lakini bila kukusanya mapato na mapato hata kama hayatatosheleza maana yake ni kwamba mipango ambayo tunaipanga ndani ya Bunge hili Tukufu haitoweza kutekelezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika ukaguzi wa CAG wa mwaka 2019/2020 umebaini mambo kadhaa kwenye mamlaka hii ya mapato ambayo sisi kama Kamati tumeona kwamba tuishauri Serikali kuweza kuyachukulia hatua za haraka ili kuongeza mapato ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na trend ya kutokutimia malengo ya ukusanyaji wa mapato, kwa mfano; mwaka 2019/2020 mapato ambayo yalikadiriwa ni trilioni 19.6 lakini ambayo yamekusanywa ni trilioni 17.1. Kutokutimia malengo ya ukusanyaji mapato kwa TRA kuna sababishwa na mambo kadhaa; moja wapo ni mifumo ambayo TRA wanaitumia kwenye kukusanya mapato haya. Kwa mfano; kuna mfumo wa ITAX, mfumo huu unaiwezesha Mamlaka ya Mapato kuweza kukusanya mapato ya wafanyabishara mmoja mmoja. Lakini mfumo huo umegundulika na dosari kadhaa zikiwemo zinazosababisha upotevu mkubwa wa mapato au kutokukusanya mapato inavyopaswa. Kwa hiyo, tunaiomba sana Serikali uupitie upya mfumo huu wa ITAX ili kuongeza mapato yanayotokana na wafanyabiashara kila mwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, CIMIS pia ni mfumo mwingine ambao unamilikiwa na TRA. Mfumo huu unalengo la kutatua changamoto za mashauri ya kodi ambayo yanaendelea kurundikana mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, mwaka 2018/ 2019 mashauri haya yalikuwa 770 lakini hadi kufika 2019/2020 mashauri haya yameongezeka licha ya kuwa na mfumo huu wa kuwasaidia utatuzi wa makosa haya na kufikia makosa 1097. Kiukweli tulitegemea sana kwamba kuwepo kwa mfumo huu ungeweza kusaidia kutatua mashauri haya lakini tunaendelea kuona trend ya ongezeko ya makosa haya ya kikodi.

Mheshmiwa Spika, mfumo huu pamoja na kusababisha ongezeko hilo la makosa lakini pia kuna trilioni 360 mpaka sasa ambazo zinasubiria kutatuliwa kwenye mashauri haya. Lakini endapo mashauri haya yataweza kutatuliwa Serikali inaweza ikaingiza fedha nyingi sana. Mbali na tatizo hili la mfumo huu, pia kuna udhaifu mkubwa kwenye mfumo huu ambao nimezungumza wa CIMIS ambao unamuwezesha Meneja wa Kanda moja kuweza kuingia mashauri ya kanda nyingine. Kwa kweli kama tutaweza au kama kutakuwepo maafisa ambao siyo waaminifu wanaweza wakabadilisha nyaraka za Ushahidi na kuweza kuisababishia hasara kubwa Serikali yetu. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshmiwa Spika, naunga mkono hoja hiyo. (Makofi)