Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza nikupongeze kwa kupata uteuzi huo wa Naibu Spika, nakupongeza sana. Pia tunakupongeza kwa kuwa mgeni juzi siku ya Jumapili pale, na tukaona kwamba ile kutoa mkono wako kama Mgeni rasmi ilisaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nijikite katika hoja moja, nayo ni bandari, Kamati ya Bajeti wameizungumzia Bandari, lakini pia Kamati ya Mitaji ya Umma nao wameisemea. Kwa hiyo, nijikite moja kwa moja katika upakuaji wa mafuta bandarini. Tunafahamu mafuta yanapakuliwa pale bandarini na anayeshughulikia hili pale ni TPDC. Lakini pia kuna PURA naye huwa anasaidia. Sasa, tunapakua mafuta kwa ajili ya nchi tofauti. Yako yanayokwenda Rwanda, Burundi, Malawi pamoja na Congo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa bahati mbaya kuna tozo. TPDC na PURA wanaitoza ZPDC na ZURA tozo ambayo hizi nchi nyingine hawatozwi. Sasa hii tozo imegeuka wakati mwingine inaweza kuwa deni; Sasa nielezee nini athari yake? Athari za tozo hizi ni mbili. Moja, ZPDC na ZURA yaani wanakaa kama watalipa hiki kitu, inamaana kwamba kule Zanzibar bei ya mafuta itakuwa imebaki ileile, lakini TPDC yeye ataandika kama ni deni, lakini litakuwa ni deni hewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, na athari nyingine, ZPDC na ZURA walikilipa tozo hii moja kwa moja itakuwa kwamba TPDC na PURA wamepata pesa lakini kule Zanzibar bei ya mafuta itaongezeka. Sasa haya yote mawili yanaweza yakatokea. Ninalizungumzia hili katika muktadha kwamba Serikali iliangalie na walete sheria iliyompa mamlaka hayo TPDC kwamba yeye awe anawatoza kodi watu wote. Kwa hiyo kitu hicho angalau kidogo kitakuwa kimekaa vizuri; kwa hiyo walete sheria hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, na tukibadilisha sheria hiyo ina maana kwamba ZPDC na ZURA hawatatozwa tozo na TPDC kwa sababu hawatozi tozo Rwanda, Burundi wala Malawi, na haya mafuta yanapita hapa kama ni transit.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna msemo unasema kwmaba ajizi ni nyumba ya njaa, na chelewa chelewa utamkuta mtoto si wako. Tumelizungumzia hili, Tanzania sasa hivi miundombinu ya upakuaji mizigo ni mizuri, lakini kasoro moja iliyopo ni kwamba hatuna mfumo mmoja kwa taasisi zote zinazoshughulika na pale bandarini. Pale pana TPA, TRA, wako na regulators tofauti ambao wanafika mpaka 12. Hawa regulators mpaka wakimaliza documentation ule mzigo kutoka pale unachelewa, na sisi uchumi wetu tunapitia Bandari ya Dar es Salaam. Tukisema kwamba tunachelewa kutoa mzigo ina maana tunaipunguzia ushindani bandari yetu. Kwa sababu tumezungukwa na bandari nyingine za nchi Jirani, kwa hiyo ili bandari yetu iwe competitive ina maana kwamba tuwe na mfumo mmoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeeleza kwenye Kamati ya Bajeti kwamba tulikwenda kutembelea bandari ambako walisema kwamba wanatengeneza mfumo wa pamoja. Hata hivyo ni mwaka sasa mfumo huu wa pamoja haujafanya, ndipo nikasema kwamba ajizi ni nyumba ya njaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kingine, kuna kitu kinaitwa TICTS ambao wameingia mkataba na Serikali juu ya kutoa mizigo pale bandarini. Hata hivyo wakati mwingine kila ukiitazama hii TICS tunaona kama vile kuna vituu kidogo havielekei. Tunaiomba Serikali, TICS wana mkataba ambao wana automatic renew. Kwamba watakapokuwa wametekeleza kigezo fulani mkataba ule unajirudia tena. Lakini bandari sasa hivi inaelekea kujitegemea na inafanya mapinduzi makubwa. Kuwa na TICS pale, na hivi vigezo tunavyompa, akifika kwenye asilimia ile ina maana kwamba bandari haweze kumuingilia TICS.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaiomba Serikali huu mkataba utenguliwe, kwa sababu mkataba huu ni kama umewalenga watu kuwa na maisha yao yote pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, niipongeze Serikali kwenye mambo matatu. Bajeti, kwa utekelezaji wake kwenye makudanyo, kwenye sheria ya fedha kulisikiliza Buunge, lakini pia katika kupeleka fedha kwenye miradi ya maendeleo kwa zaidi ya asilimia 80.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru, naunga mkono hoja zote mbili.