Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

Hon. Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

MHE. KWAGILWA R. NHAMILO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana niungane na wenzangu kukupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge letu la Jamhuri ya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka jana kamati yako ya bajeti pamoja na Bunge kwa ujumla tulifanya Amendment of the Road and Fuel Tolls Act Cap. 220. Marekebisho haya yalilenga kuipatia TARURA fedha kwa ajili ya barabara zetu za vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nitoe taswira ndogo sana ya TARURA tunapozungumza TARURA ili angalau tufanye mapinduzi kwenye eneo hili la barabara zetu za vijijini. Handeni hususan Jimbo la Handeni mjini barabara zetu za TARURA barabara za vumbi ni 88%. Kwa Mkoa wa Tanga barabara zetu za TARURA, barabara za vumbi ni 79% na kwa Tanzania nzima TARURA ina mtandao wa barabara unaofika kilometa 144,429 zinahudumiwa na TARURA. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hizo 76% ni barabara za vumbi kwa maana ya kilometa 111,197, TANROADS inahudumia barabara zote kilometa 36,000 na katika hizo zenye lami ni kilometa 11,000 what is the myth ni kitu gani cha ajabu kwenye hiki ninachojaribu kukizungumza tumeipa TARURA jukumu kubwa sana lakini hatujaweka juhudi kubwa za kibajeti na za kitaasisi za kiteknolojia na kwa nguvu zote kujaribu kuibadilisha ili iweze kuhudumia barabara zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa takwimu hizi nilizotoa hapa ndiyo kusema kwamba barabara nyingi mtandao mkubwa wa barabara Tanzania uko chini ya TARURA. Sasa the opposite ndiyo tunachokifanya tunapeleka nguvu kubwa sana TANROADS na natambua kwamba barabara wanazohudumia ni za lami, lakini haiondoi fact kwamba kilometa hizi 144,429 ndiko ambako Tanzania waliko na ndiko ambako uchumi uliko. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninachotaka kusema ni nini ninachotaka kusema ni kwamba lazima tufanye mapinduzi ya namna ya approach ya kutengeneza barabara zetu kuanzia kwenye bajeti yetu inayokuja lazima tufikirie kwa namna ya tofauti. Tathmini ya dharura iliyofanywa juzi kwa uharibifu unaofanywa na mvua uliosababishwa na mvua tathmini iliyofanywa ya haraka inahitajika bilioni 120 kufanya tu marekebisho .(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukichukulia sasa ile amendment tuliyofanya ya kutoka bilioni 322 na hizo kwa hakika hatutaweza kuzikusanya zote, 120 yote inaenda kufanya marekebisho yaliyosababishwa na mvua. Which means tunakwenda ku-miss target yetu ambayo tulijiwekea kufungua barabara zetu za vijijini ninachotaka kusisitiza kama ambavyo tumefanya jitihada za makusudi kwenye SGR, jitihada za makusudi kwenye bwawa la Mwalimu Nyerere, vivyo hivyo moyo wa uchumi wa nchi yetu ni hizi barabara hizi kilometa 144,000 ambazo ziko chini ya TARURA. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo lazima tufanye mapinduzi ya namna ya kufikiri na lazima tufanye mapinduzi ya namna ya kutenga bajeti yetu. Tusii-treat TARURA kama kachombo kadhaifu dhaifu hivi ambako kako chini ya Wizara ya TAMISEMI ambako hata hivyo hata kwenye hiyo Wizara yenyewe tuna Waziri wa TAMISEMI na Manaibu Waziri wawili mmoja anajulikana ni wa afya na mwingine anajulikana ni wa elimu. Yaani hata hiyo TARURA pale huioni. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa dhati kabisa ni lazima tufanye mapinduzi bajeti inayokuja tutenge fedha nyingi lakini zienda angalau zikabadilishe barabara zetu zitoke kuwa za vumbi ziende kwenda kuwa changarawe. Lakini na siku za usoni siku za baadae tujifunze teknolojia kwa wenzetu tutengeneze barabara zetu kwa teknolojia ambayo ni cheap.

NAIBU SPIKA: Malizia.

MHE. KWAGILWA R. NHAMILO: Kama ambavyo alishauri Mheshimiwa Rais barabara zetu tuzifanyie mapinduzi tuende kwenye teknolojia ya kati ambayo siyo gharama sana lakini barabara tuzijenge ziweze ku-survive na ku-sustain kwa muda mrefu.