Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuanzia Januari, 2021 hadi Februari, 2022 pamoja na Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa Kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022

Hon. Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuanzia Januari, 2021 hadi Februari, 2022 pamoja na Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa Kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote naomba nikupongeze sana, wewe unaweza sana, hongera sana mkubwa wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi hapa leo kazi yetu ni kuchangia Kamati. Naomba niipongeze Kamati yetu ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kazi kuwa wanayoifanya ya kutushauri; na kwa ufupi ni kwamba sisi kama Serikali tutachukua mapendekezo yote ya Kamati kwa ajili ya kuyafanyia kazi, hilo ndilo jukumu letu kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina hakika Waheshimiwa Wabunge wanafahamu kuwa ajenda ya mazingira nip ana, na tuna kila sababu kwa kila mmoja wetu kuhakikisha kwamba tunashirikiana vizuri katika mpango wa mazingira. Tumeshuhudia wazi hivi karibuni kwamba Taifa letu liliingia katika changamoto kubwa sana ya mgao wa maji, ni changamoto ya kimazingira. Ukiachia hapa Dodoma, ukienda pale Morogoro watu wa Morogoro walikuwa katika hali mbaya sana. Ukienda Dar es Salaam hali ni ile ile. Changamoto yam aji iliathiri sana vilevile hata upatikanaji wa nishati ya umeme ambapo naamini hata baadhi ya viwanda vilishindwa kufanya kazi vizuri na hatima yake, hata hatuwezi kujua, inawezekana pengine wakapoteza ajira. Hiyo yote ni chain ya mazingira. Kwa hiyo tuna kila sababu kuhakikisha kwamba tunalinda mazingira. Wenzetu wa kule Kiteto na Simanjiro hali ilikuwa mbaya sana kiasi cha mifugo kufa, yote ni changamoto ya kimazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini niwashukuru sana wadau wote kwa pamoja. Hivi sasa Serikali tuko katika ajenda ya kuhakikisha tunapambana na mazingira, na tumeshuhudia kwamba katika utekelezaji wa miti, na niwapongeze sana Wabunge wote katika maeneo yenu; na kwa kweli hali ya upandaji wa miti ni nzuri na hamasa imekuwa kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, na kwa sababu kesho tunazindua Sera yetu ya Mazingira ya mwaka 2021, ni Imani yangu kwamba Waheshimiwa Wabunge wote pamoja na wadau wengine tutashirikiana kwa pamoja katika suala la utekelezaji wa seria hiyo. Lakini pia nishukuru kwa sababu hapa Mwenyekiti ndiye atatoa response kwa michango yote, niwashukuru sana Wabunge katika Kamati mbalimbali, hasa Kamati yetu ya Mazingira kwa kutoa ushauri mbalimbali na hasa kwa upande wa Wabunge waliotoka Zanzibar tunafahamu kwamba katika Wizara yetu tuna-deal na mambo ya Muungano kwa upande wa Muungano lakini pia mazingira upande wa Tanzania Bara. Kule Zanzibar ni Wizara iliyo Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. Dada yangu Saada ndiye anayehusika eneo lile.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo kuna miradi mingine ambayo tuna-scale up mpaka maeneo ya Zanzibar, kwa mfano Kaskazini A; nishukuru sana, lakini bahati mbaya miradi hii tukiwa tunafanya sisi huku kule Zanzibar maana yake hatuna mkono wa moja kwa moja. Mheshimiwa Mbunge unafahamu, mradi wako ule ndio unaotekelezwa kwa Mheshimiwa Comrade Ole-Sendeka pale. Ukienda kwa Ole- Sendeka zaidi ya ng’ombe 10,000 wanakunywa maji kupitia mradi ule.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa pesa hizi zinashuka kwenye Halmashauri ambazo ndizo zinazosimamia. Katika Halmashauri ya Mheshimiwa Ole-Sendeka (Simanjiro) mradi umekwenda vizuri 100% na wananchi watasema huyu mwaka 2025 kitaleweka vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini bahati mbaya na fedha hizi zilienda katika Halmashauri ya Kaskazini A, kwa hiyo, Mkurugenzi na timu yake ndio wanaoratibu mambo hayo. Mmeshauri mambo ya uratibu, tutauangalia ushauri wenu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile nishauri; kule nako tuna wawakilishi ambao pia wanaingia kwenye vikao vya ndani na Mkurugenzi yuko pale. Niwaomba Mheshimiwa Mbunge wakati mwingine tuwashauri wenzetu katika vile vikavyo wanavyokaa, maana kuna Kamati inayoendeshwa katika Halmashauri husika, basi tushauri kwamba zile fedha zikifika, kwa mfano ununuzi wa boti au uchimbaji wa visima; ni kweli, lakini Ofisi ya Makamu wa Rais huku yeye kazi yake inahakikisha inatoa zile fedha halafu uratibu ni wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, mmeshauri hapa kwamba suala la uratibu tulifanye vizuri. Tunaomba kuchukua ushauri huu kwa ajili ya kuona namna ya kufanya, miradi hii, kama ya mafanikio yaliyopatikana kule Kishapu, Mpwapwa, Simanjiro pamoja na Mvomero basi halikadhalika Halmashauri ya Kaskazini A ifanye vilevile utekelezaji kwa haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme ushauri huu ni mzuri; na kwa kweli suala la mazingira sasa hivi limekuwa changamoto kubwa na ndiyo maana tuna jukumu la kujitahidi sana kwa kushirikiana na upande wa pili kule, japo suala la mazingira lipo upande huu, kwa ajili ya kuvinusuru visiwa vyetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimekwenda pale Nungwi kwa rafiki yangu comrade pale, hali ni mbaya, maeneo mengine yanalika kabisa. Ukienda kwa dada yangu pale, Mbunge wa Pandani hali ni changamoto kubwa kule kwake, ukienda Chakechake kule hali ni mbaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tuseme kwamba suala la mazingira kwa sasa hivi ni suala gumu sana. Naomba niwaambie kwamba ofisi yetu itajitahidi kufanya kila liwezekanalo ili fursa za kimataifa zinazoweza kupatikana,tuzitafute kwa nguvu zote kwa kushirikiana, kwa sababu suala la mazingira halina mipaka na linaenda mbali zaidi; tutashirikiana upande wa Bara na Zanzibar, mimi na dada yangu Saada Mkuya tutafanya kazi kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, licha ya kushirikiana, ninabeba ajenda moja ya Wabunge, suala la uratibu liwe vizuri, hili ninalichukua. Kwa sababu kama tusipoweka misingi mizuri ya uratibu, hata fedha ikitoka huku ikienda kule kama mambo hayataenda vizuri itakuwa ni changamoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nishukuru sana, tutatekeleza maelekezo ya Bunge. Ahsante sana. (Makofi)