Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuanzia Januari, 2021 hadi Februari, 2022 pamoja na Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa Kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022

Hon. Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuanzia Januari, 2021 hadi Februari, 2022 pamoja na Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa Kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia kuhusiana na hotuba ya Kamati ya Viwanda na Bishara lakini pia Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kuna vitu tunavikosea sana, mathalani…

(Hapa Mhudumu wa Bunge alimkabidhi nyaraka zake)

MBUNGE FULANI: Hajajipanga huyo.

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, na samahani kwa hicho kilichotokea, maana ni kama nimekuwa ambushed, na pia sijawahi kuchangia kutoea upande huu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza leo tarehe 11 Februari ninachangia, itakumbukwa kwamba leo ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi. Na jana imesomwa taarifa ya Kamati ya Sayansi na Teknolojia, lakini ninyi nyote ni mashahidi kwamba sayansi, teknolojia na ubunifu, suala la ubunifu ni suala ambalo kama halitambuliwi vizuri na Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa hivi tunavyozungumza Taifa hili linatambua sayansi na teknolojia ambayo kuna Sera ya Sayansi na Teknolojia ya mwaka 1996, lakini pia kuna Wizara ya Teknolojia na Mawasiliano ambayo ina teknolojia, halafu kuna Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, zote hazina neno ubunifu, kwa maana ya innovation.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ninyi nyote ni mashahidi, nchi zote ambazo tunazitolea mfano kwenye Taifa hili, kwamba ni nchi ambazo zimefanya vizuri kwenye masuala ya viwanda na biashara, kama nchi ambazo zimefanya vizuri kwenye biashara na kwenye maendeleo, kwa maana ya nchi ambazo zimeendelea wote wamefanya vizuri katika masuala ya sayansi na teknolojia, lakini pia na ubunifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo sisi kama Taifa tuna Wizara nyingi, yaani kama kuna Wizara ambazo hazihusiani na masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu (STI) hazizidi tano, hazipo. Wizara yenyewe ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji inahitaji innovation science and technology. Pia Wizara ya Afya inahitaji science innovation and technology, Wizara ya Elimu, Wizara ya Kilimo yenyewe pia, zote zinahitaji science, technology na ubunifu kwa maana ya innovation.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hatutapiga hatua kama taifa kama hatutakuja kuharakisha na kufanikisha mchakato wa sera itakayoitwa Sera ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu. Kwa sababu mpaka sasa hivi tunavyozungumza sera hiyo ina miaka 28. Tumeanza kuipigia kelele tangu tuko nje, hatujaingia kwenye Bunge hili mpaka sasa hivi. Itakapokuja kufika hatua kwamba sera inaletwa itakuwa outdated kwa sababu tunakusanya maoni leo. Tutakaa miaka 10 ijayo ndipo tuje tulete sera ambapo maoni yamekuswanywa leo, maana yake hatutakuwa tumefanikiwa. Kwa hiyo, ili tufanikiwe tunahitaji kuwa Sera ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia kwenye viwanda na biashara Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ina miaka 19, ni ya mwaka 2003. Lakini pia Sera ya Taifa ya Biashara ina miaka 19; ni ya mwaka 2003, iko outdated. Waheshimiwa Wabunge mkumbuke kwamba life span ya sera ni miaka kumi. Kwa hiyo, tuna sera ambayo tunategemea ituletee maendeleo kama Tanzania ya Viwanda, sera ambayo ina miaka 19 hatuwezi kufanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama Taifa mpaka sasa hatuna Sera ya Taifa ya Ubora, hatuwezi kufanikiwa. Watanzania wenye biashara ndogo ndogo na biashara ndogo sana hawajui kuhusiana na blue print, sisi tunajua blueprint. Hatuwezi kufanikiwa kama Taifa, na ni lazima tuvuke hatua.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatuwezi kufanikiwa hata kama tuna Tume ya Ushindani (Fair and Competition Commission) kwa sababu hatuna innovation. Vitu vyote vinahitaji watu wafikiri, sasa sisi kama nchi hatujajipanga kuhakikisha kwamba tunasaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nitoe ushauri kwa Serikali, umefika muda sasa iundwe wizara maalum iitwe Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu. Kenya, Rwanda, Burundi, Uganda, Malaysia pamoja South Africa wamefanya hivyo na wamefanikiwa, ukiachana na China na nchi nyingine ambazo zinaonekana ni first world…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)