Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamati ya Kudumu Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu shughuli za Kamati hizo kwa Mwaka 2021

Hon. Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamati ya Kudumu Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu shughuli za Kamati hizo kwa Mwaka 2021

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa fursa hii ya kuweza kuchangia. Nianze kukupongeza wewe binafsi kwa kuweza kuchaguliwa kwa kura za kishindo, kuwa Spika wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia nichukue nafasi hii kuishukuru sana Kamati yetu chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Zungu, ambaye na yeye nimpongeze kwa kuweza kupitishwa na Chama chetu kuwa Mgombea wa Naibu Spika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kweli Kamati hii kwa muda mfupi ambao nimeweza kushirikiana nayo imetupa ushirikiano mzuri sana. Nafarijika sana kuwa ni miongoni mwa Wajumbe wa Kamati hii. Kwa hiyo nawashukuru sana, nawapongeza sana kwa kazi nzuri ambayo wanaendelea kufanya. Hata hivyo, pamoja na taarifa nzuri ambayo imewasilishwa hapa leo, nataka nijikite katika maeneo kama matatu hivi ambayo Kamati iliyazungumzia lakini na baadhi ya Wabunge waliyagusia ni kwa upande wa Jeshi la Magereza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa kuna hoja mbili kwenye Jeshi la Magereza. La kwanza, ilikuwa ni jinsi gani Jeshi la Magereza linaweza likajitosheleza na chakula, lakini na la pili, lilikuwa linahusu hoja ya kupunguza msongamano kwenye Magereza yetu. Sasa nasema hoja hizi mbili naweza nikazichangia kwa pamoja kwa sababu zinaingiliana. Kwa nini nasema zinaingiliana? Tunapozungumzia dhana nzima ya Magereza kujitosheleza na chakula ni jambo la msingi sana.

Mheshimiwa Spika, haiingii akilini kabisa kwamba Jeshi la Magereza, ambalo lina rasilimali ardhi yenye rutuba ya kutosha, lakini tunasema ina nguvu kazi pia ya kutosha, iwe inaendelea kutegemea ruzuku ya Serikali katika kuhudumia wafungwa. Imani yangu ni kwamba sio tu kwamba linaweza kujitosheleza na chakula, lakini linaweza likazalisha ziada kwa ajili ya kuweza kulipatia Jeshi la Magereza mapato yatakayosaidia kupunguza changamoto mbalimbali za Jeshi letu. Sasa ninaposema hizi hoja zinaingiliana nina maana gani? Hivi tunavyozungumza mpaka leo tuna takribani watu bilioni 32, ambao kati ya hao kama milioni 18.2 ndio wafungwa, lakini kuna milioni 13.8, hawa ni mahabusu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunapozungumzia suala la wafungwa kuwatumia kama nguvu kazi ya kulima ili tujitosheleze na chakula, kuna changamoto lazima tuje na mawazo na ubunifu mwingine wa ku-address jambo hili. Kwa sababu, hatuwezi tukasema kwamba katika karne hii tunayoendelea wakati hoja ya kutaka kupunguza wafungwa Magerezani inakuwa ina umuhimu wake mkubwa, halafu tuseme tuwa-retain wafungwa hawa kwa sababu, eti tunataka watusaidie kujitosheleza na chakula.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hapa kuna vitu lazima tuvi-address kwa kutumia ubunifu wa hali ya juu. Ndio maana tumeamua sasa hivi kuja na utaratibu ambao nataka niueleze hapa kwa ufupi. Utaratibu huu utasaidia sana kulifanya Jeshi letu la Magereza, liweze kujikita zaidi na lile jukumu lake la msingi la kurekebisha wafungwa. Kumekuwepo na baadhi ya hoja kwa baadhi ya watu wanasema, baadhi ya wafungwa wanaweza wakaachiwa sasa hivi, halafu baada ya muda mfupi wanarudi kuwa wahalifu. Nasema pengine kwa sababu labda, Jeshi la Magereza linajikita sasa katika kufanya mambo mawili kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati huo huo Jeshi la Magereza tunasema lirekebishe wafungwa ambalo ni jukumu lake la msingi, lakini tunasema wakati huo Jeshi la Magereza tunataka lijitosheleze na chakula, liweze kubuni miradi mbalimbali, viwanda na kadhalika. Basi mambo haya tunataka tuyafanye kwa pamoja, lakini kwa utaratibu ambao utatenganisha majukumu yake. Ndio maana tuna mkakati kabambe wa kuhakikisha kwamba mashirika yote ya uzalishaji mali katika Majeshi yetu, ikiwemo Jeshi la Magereza yanasimama na kujiendesha kibiashara. Ili kuliacha Jeshi la Magereza kama Jeshi kufanya kazi zake za msingi za kurekebisha wafungwa na mengineyo yaliyopo kwa mujibu wa Katiba pamoja na Sheria za Nchi yetu na Kanuni zake. Katika kufanya hivyo ni imani yetu kwamba… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Sekunde chache malizia.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kusema kwamba, kuna mambo ambayo kama Serikali yanaendelea kufanyika. Nimpongeze sana Rais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, katika sherehe za Uhuru hivi karibuni amesamehe wafungwa, zaidi ya 5,704. Hizi ni katika jitihada za kupunguza msongamano magerezani. Kana kwamba hiyo haitoshi, kuna hatua nyingi ambazo tunaendelea, kuzichukua na tunaamini hizi zitasaidia kupunguza msongamano wa wafungwa. Moja, tuna sheria zetu kuna Sheria ya Parole. Kuna Sheria ya…(Makofi)

SPIKA: Sasa, Mheshimiwa Waziri muda umetutupa mkono.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)