Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

Hon. Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipatia hii nafasi ili niweze kuchangia kuhusiana na Mwongozo wa Mapendekezo ya Mpango. Naomba nianze mchango wangu kwa kugusia eneo la kilimo ambapo Waheshimiwa Wabunge takribani wengi sana walilizungumza kwa hisia kali, ukiwemo na mwenyewe na msisitizo wako katika eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kukiri juu ya umuhimu ambao Waheshimiwa Wabunge wameuonesha wa kulitilia mkazo suala la kilimo zaidi katika Mpango wetu. Kwa hiyo, kama Serikali tumelichukua jambo hili kwa uzito wa aina yake na kwa kuwa, huu ni mwongozo basi niwaahidi Waheshimiwa Wabunge kwamba, pale ambapo Mpango utakapowasilishwa utakuwa umetilia maanani eneo hilo kwa uzito ambao unastahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati njema sana tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu sana na Wizara ya Kilimo. Tutashirikiana nao wenzetu vizuri kabisa kupanga mpango wetu mzuri, vizuri zaidi katika eneo hili kwa kuzingatia maeneo yote. Msingi wake ni kuhakikisha kwamba, kilimo chetu kinakuwa kilimo cha biashara, kwa maana gani? Kwa maana kwamba, kwa eneo moja ambalo litasaidia katika kuhakikisha kwamba, tunajitosheleza kwa chakula chetu wenyewe hapa nchini, lakini vilevile kwa kuweka mazingira mazuri ya kuweza kusafirisha chakula hiki nje ili iweze kusaidia kuipatia nchi yetu fedha za kigeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, maeneo ambayo tunakusudia kuyatilia maanani ni maeneo yote ambayo Waheshimiwa Wabunge mmeyazungumza. Kwa kuyataja machache kutokana na muda, eneo la kwanza ambalo tunadhani ni la msingi sana ni eneo la mbegu. Eneo la mbegu hili tutaliwekea mkakati mzuri katika mapana yake; kwanza kuhakikisha kwamba, tunashirikisha sekta binafsi kwa utaratibu wa PPP, lakini vilevile kwa kujengea uwezo taasisi zetu kwenye eneo la tafiti kwenye RND ili tuweze kuzalisha mbegu bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nalo vilevile ni muhimu na lenyewe tutaliangalia kwa kina ni eneo la umwagiliaji. Waheshimiwa Wabunge wamezungumza jambo hili kwa kina na hivyo tuwahakikishie kwamba, miongoni mwa miradi ya vielelezo wenye mpango wetu ujao hili eneo la umwagiliaji tutalizingatia kwa uzito unaostahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo katika eneo ambalo limekuwa na changamoto kubwa sana sasa hivi kutokana na changamoto ya UVIKO na upandaji wa bei za mbolea duniani, imesababisha kupanda kwa bei na hivyo basi, ni lazima kama Taifa tuje na mkakati wa muda mfupi wa kuweza kukabiliana na tatizo hili, lakini tuwe na muda wa kati na muda mrefu wa kudhibiti tatizo kama hili lisijitokeze tena. Maeneo ni mengi ambayo tutayazingatia kama ambavyo Waheshimiwa wameyazungumza. Kutokana na muda Waheshimiwa Wabunge naomba nisiyachambue, ikiwemo masuala ya masoko, TEHAMA, ugani na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia hata katika eneo hili ambalo Waheshimiwa Wabunge wamelizungumza kwa kina sana ikiwemo jinsi gani Benki yetu ya TADB inavyoweza kusaidia katika eneo hili. Nataka niwatoe hofu Waheshimiwa Wabunge, maelekezo ambayo Mheshimiwa Rais aliyatoa na wengi wameyazungumza kwa uchungu kuhusiana na riba; niwahakikishie kwamba, mchakato huu hasa katika eneo la kilimo kuhakikisha kwamba riba zinashuka chini ya asilimia 10, ni mkakati ambao umeshaanza na BOT kwa kutoa maeneo kama matano ya kuzingatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa tayari maombi yameshapelekwa na benki kadhaa kwa ajili ya kutumia fursa hii ili riba ziweze kushuka. Bado hatujafikia katika hatua ya kusema kama BOT imeshindwa au haijashindwa. Naomba Wabunge waipe muda Serikali, tutaisimamia BOT kuhakikisha kwamba, hizi benki ama taasisi zilizoomba zihakikishe kwamba, zinatumia fursa hiyo na kutumia fursa ya kushusha riba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi benki ambazo ni za Serikali ikiwemo TADB na benki nyingine zote, hizi tunataka ziwe ndio mfano wa kwanza wa kuhakikisha kwamba zinatekeleza maelekezo ya Serikali. Kwa hiyo, tutazisimamia, kama kuanza kupunguza riba basi ziwe zinaanza hizi benki zetu za Serikali ikiwemo Benki ya Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili ambalo nataka nilizungumzie ni eneo la mikopo. Kwenye hili eneo la mikopo wako Waheshimiwa Wabunge ambao walikuwa wana mashaka kwamba, pengine mikopo hii tunakopa sana; ni kweli, ni sahihi kabisa. Katika miaka ya karibuni tumekopa kwa kiwango kikubwa sana, hilo sio jambo ambalo ni la siri, ni jambo ambalo lipo dhahiri. Kukopa maana yake nini? Maana yake dhana nzima ya kukopa pale ambapo inakuwa matumizi na mapato hayaendi sambamba. Kwa maana kwamba, mna matumizi, mna mapato halafu mna gap katikati ambayo inahitajika izibwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, mnahitaji kufadhili miradi mingi sana mikubwa ya maendeleo ambayo itakuwa na tija katika nchi, lakini pengine mapato yakishapatikana hayakidhi kufadhili ile miradi na hili jambo sio geni kwa duniani. Nchi zote duniani zinafanya hivyo ikiwemo hata hizo nchi ambazo zimeendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nini ambacho tunafanya? Tunachokifanya kwanza ni kuhakikisha kwamba, katika eneo hili la mapato ama revenues tunafanya utaratibu wa kuwa na mikakati ya kuongeza mapato yetu kama nchi. La pili, tufanye jitihada za kupunguza matumizi ili ile gape iweze kupungua na hii hofu ya mikopo na yenyewe vilevile iweze kupungua miongoni mwetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa katika hili eneo la kuongeza mapato kuna hatua nyingi ambazo tumezichukua na tunaendelea kuzichukua kama nchi, lakini kwa harakaharaka naomba nitaje chache: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa katika chombo kikubwa ambacho tunakitegemea katika kuhakikisha kwamba kinakusanya mapato ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). TRA kuna hatua ambazo tayari wamezichukua kuhakikisha kwamba, tunakusanya mapato mengi zaidi kwa wakati mmoja kulingana na changamoto zilizopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja katika mambo ambayo Mamlaka ya Mapato inafanya ni kuhakikisha kwamba, tunaongeza vyanzo vipya vya mapato na mapato haya yako ya aina nyingi, kuna mapato ambayo yanatokana na walipakodi wakubwa. Niyapongeze sana maoni ya Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia suala la kufanya utafiti kwenye eneo hili la mawasiliano, mashirika ya sim una kadhalika. Tumepokea haya mapendekezo na tutashirikiana na Wizara husika ili tuliangalie. Tunaamini kwamba, eneo hili litatusaidia kuweza kupata vyanzo vikubwa vya mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni kwenye eneo la mitandao. Kuna hoja nyingi zimezungumzwa jinsi gani tutakusanya kodi kwenye hizi huduma za mitandao. Hili lenyewe nataka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba, tayari linafanyiwa kazi na Mamlaka ya Mapato Tanzania, lakini na hizi jitihada ambazo Serikali imekuwa ikichukua za kuhakikisha kwamba, tunafungua fursa zaidi za uwekezaji nchini ili sekta binafsi iweze kuingia na tupate wawekezaji wakubwa, zitasaidia kuongeza katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la informal sectors; hawa watu ambao wanaitwa wafanyabiashara wadogowadogo. Tuna mikakati thabiti na juzi mmeshuhudia Mheshimiwa Rais ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa soko pale Kariakoo na maeneo mengine mengi. Haya ni mambo ambayo tunafanya kama Serikali ili wale ambao wanaitwa wafanyabiashara wadogowadogo waweze kuku ana walipe kodi. Mambo mengine ni masuala ya mifumo, masuala mengi ambayo tunafanya ya kuhakikisha kwamba, TRA inafanya kazi yake vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna vyanzo vingine, mikakati ya kutafuta vyanzo mbadala vya mapato na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niende harakaharaka kwa sababu ya muda, kwenye eneo lingine hili la kupunguza matumizi. Tutakapokuwa tuna njia za kuweza kupunguza matumizi kwa maana gani? Kwa maana ya kuhakikisha kwamba, mikopo ambayo tunakopa inakuwa sio mikopo ya kibiashara mpaka pale inapobidi. Kwa hiyo, kwanza tuzingatie sheria; tuna sheria kama tatu ambazo tunazisimamia, Sheria hii ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura Namba 134, lakini pia kuna sheria nyingine mbalimbali ambazo zinatuongoza jinsi ya kukopa mikopo ya kibiashara ambayo itakwenda kuwekeza katika miradi ambayo inaleta impact kwenye uchumi wa nchi yetu, hilo ni la msingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna vipimo ambavyo vimewekwa vya kisheria kabisa vya kupima mikopo hiyo inakopwa vipi. Moja, ni kwa mfano kuangalia ratio kati ya thamani ya deni la sasa na GDP na nyingine kuangalia thamani ya sasa ya deni na export. Hayo maeneo mawili ni muhimu sana na ndio maana niungane sana na Mheshimiwa Waziri wa Nishati alivyozungumza, miradi kwa mfano ya reli (SGR), miradi hii ya umeme, hii itasaidia sana kuhakikisha kwamba, GDP yetu kama Taifa inakuwa, lakini vilevile na usafirishaji utasaidia kufanya tuweze kusafirisha nje bidhaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukifanya hivyo maana yake nini? Maana yake uhimilivu wetu kama Taifa utaongezeka. Kwa hiyo, miradi hii ya uwekezaji niwahakikishie kwamba, imezingatia sheria, lakini imeangalia miradi ambayo italeta tija kwa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ya msingi ni kuona kwamba, sasa tunaweza kufanya jitihada na hii ndio kazi ambayo Mheshimiwa Rais Samia ameifanya kwa weledi mkubwa sana, kwamba, lazima tuweze kupata kuimarisha mahusiano yetu na taasisi za kimataifa ambazo zinatoa mikopo ya riba nafuu. Mikopo hii ni muhimu sana, juzi mmeshuhudia 1.3 trillion iliyotolewa jinsi ambavyo imeleta impact kubwa sana katika nchi yetu, imeenda kuchochea shughuli za uchumi kila mahali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba hatuhangaiki kutafuta fedha zenye gharama kubwa, masharti makubwa au riba kubwa kwa ajili ya kufanya miradi, bali miradi hiyo sasa inafanywa kwa fedha ambazo masharti yake ni nafuu mno. Kwa hiyo katika eneo la kupunguza matumizi hata kama itakapofika mahali tunahitaji tulipe deni kwa mwezi, maana yake tukilipa deni ambalo lina grace period ndefu, deni ambalo riba yake ni ndogo, mzigo kwa Serikali unapungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la kupunguza matumizi hata kama itakapofika mahali tunahitaji tulipe deni kwa mwezi, maana yake tukilipa deni ambalo lina grace
period ndefu deni ambalo riba yake ni ndogo. Kwa hiyo, mzigo kwa Serikali unakuwa unapungua.

Mheshimiwa Spika, hoja ya msingi na muhimu ni kuhakikisha kwamba fedha hizi zinatumika inavyostahili na hivyo basi ile hoja ambayo Waheshimiwa Wabunge wamezungumza ni hoja ya msingi sana hoja ya kuhakikisha kwamba suala la tuliangalie kama Serikali eneo ambalo lina mapungufu na tunakiri kwamba eneo hili lina mapungufu eneo la kuangalia kuhusu eneo la sera la M & E ufuatiliaji na uthamini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati tukiandaa tukijipanga katika kulipatia ufumbuzi wa kudumu tatizo hilo kuna jitihada ambazo Serikali imefanya katika kuboresha ufuatiliaji na utathmini wa miradi ya maendeleo kwenye kuandaa hiyo sera ya Taifa ufuatiliaji wa tathmini, kwa kufanya mambo kadhaa. Moja ni kuandaa mfumo wa kitaifa wa kusimamia miradi ya maendeleo ambapo kimsingi utawezesha upatikanaji wa taarifa za miradi kuanzia uibuaji hadi utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jingine ambalo tunafanya ni kuandaa mwongozo wa ufuatiliaji wa tathmini ya miradi na program za maendeleo. Lakini kama kumbe hiyo haitoshi Waheshimiwa Wabunge walipendekeza juu ya umuhimu wa kuishirikisha sekretarieti za mikoa. Ni pendekezo zuri Waheshimiwa Wabunge pendekezo hilo tumelichukua na tutalizingatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ufupi maeneo ambayo nilikuwa nimejipanga kuchangia ni hayo nashukuru sana kwa hii fursa.