Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Viwango vya Afya ya Mimea, Wanyama na Usalama wa Chakula

Hon. Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Viwango vya Afya ya Mimea, Wanyama na Usalama wa Chakula

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Itifaki hii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Viwango vya Afya ya Mimea, Wanyama na Usalama wa Chakula. Kwanza kabla ya kuendelea naunga mkono hoja na nafanya hivyo kwa sababu kuna baadhi ya vitu vilivyomo katika Itifaki hii hata kama tulikuwa tunaogopa na hata tungeendelea kuogopa, hatuwezi kuvizuia.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano Article ya nne inazungumzia framework for managing pests na tunafahamu kwamba pests hawana mipaka, hata nadhani mwaka huu kulikuwa na nzige hawawezi kusema hawa wamesaini au hawa hawajasaini, wata-cross na kama hakuna hiyo management maana yake ni kwamba tutakuwa hatufanyi jambo lolote la maana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna mambo ya cross pollination ambalo hilo ni la kuliangalia, kwa mfano hata tunapozungumzia kwamba hatutaki GMO, lakini kuna nchi ambazo tunapakana na wanalima na wanaweza wakawa wanakubali GMO, sasa cross pollination pia hatuwezi kuzuia nyuki kuvuka mpaka kwa mfano. Kwa hiyo kuna vitu ambavyo hata kama hatutaki kwa sababu tunapakana na nchi na hatujajenga ukuta au kuzuia kwa namna yoyote ni lazima vile vitu tutavipata tu. Kwa hiyo kwa kusaini hii Itifaki inatoa room ya discussion ambayo inaweza ikasababisha hayo mambo tukaya-manage vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ili tuweze kunufaika sasa na Itifaki hii ambapo ni kweli kwamba sisi ni wazalishaji wa chakula na sisi tunaotoka kwenye maeneo tunayozalisha chakula kingi kama mahindi na hata sasa hivi wanazungumzia parachichi, kuna mambo ambayo ili tuweze kunufaika ni vizuri Serikali yetu ikajiandaa. Jambo la kwanza ni maabara na vifaa vya kupimia ubora wa hayo mazao kutoka kwenye chanzo chenyewe. Kwa mfano, mtu anaposafirisha mahindi kutoka Iringa, Sumbawanga au Mbeya halafu afike mpakani ndipo aambiwe hayana ubora wa kutosha, itakuwa ni changamoto na inaweza ikawa ni disaster kubwa zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo wakati tunapokwenda kusaini hii Itifaki, basi zile sehemu zinazohitaji maabara ya kupimia haya mazao ziwe zimeandaliwa ili wakulima waweze kunufaika. Kwa hiyo, maabara kama hizo na hata sasa hivi kwenye kilimo hiki cha parachichi zile maabara za kupima ubora ambapo sasa mtu anapokuwa na hiyo certificate tangu kwenye chanzo, kwa sababu mara nyingi processing za certificate zinaweza zikafanyiwa mahali ambapo sio kwenye chanzo cha hayo mazao. Kwa hiyo certification ikifanyika kule itakuwa rahisi zaidi kwenye kuhakikisha kwamba tunanufaika na protocol hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haiishi tu kwenye maabara zenyewe, bali pia kuwajengea uwezo wakulima kuelewa viwango, kwa sababu wafanyabiashara wapo lakini wengi hawaelewi hivi viwango. Nilifanya utafiti kidogo, kwa mfano, maandalizi yapo ya kutosha sana kwenye sekta ya chakula TBS imesha-harmonize karibu kila kitu kwenye East Africa, kama ni vyakula vilivyobaki basi ni vichache sana. Hata hivyo, pamoja na hiyo harmonization ambayo imeshafanyika, ni wakulima au wafanyabiashara wangapi wanajua au labda kuna haja ya kutengeneza manual ya standards hasa kwa vile vyakula ambavyo tuna-export sana na zikawepo kwenye sehemu ambazo watu wanaweza kuzi-access, tena zikatengenezwa kwa lugha rahisi ili kila mtu aweze kuelewa standard zetu ni zipi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nazungumza hivi kwa sababu, kwa mfano TBS waki-harmonize na ziko pale TBS kwenyewe na wakulima hawaelewi, bado watataka ku- export kitu ambacho kinaweza kisiwe competitive au kikawa haki-fit kwenye hii protocol. Hiyo inaweza ikawa ni changamoto ambayo inaweza ikasababisha hii protocol ikatupa disadvantage badala ya advantage kwenye nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hilo napenda pia liangaliwe kwamba kuna elimu kiasi gani ili tuweze kunufaika? Maana yake hofu hii inaweza ikawa hatukujiandaa, sasa tumejiandaa: Je, wananchi wa kule Iringa, Mbeya na Sumbawanga, wanaelewa maandalizi tuliyoyafanya ili waweze ku-export? Kwa sababu kweli sisi ni beneficiary wakubwa sana wa hii, lakini kama kutakuwa na maandalizi ya kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa kwa kweli ni vizuri sana kuiomba hata Serikali kuangalia, kwa sababu kama tunaendelea kuzungumza kwamba kilimo ni uti wa mgongo na ufugaji ni uti wa mgongo pia, lakini kama tusipotengeneza mazingira ya ku-export tukabakia kula wenyewe, maana yake ni kwamba haitawezekana kuweza kunufaika na baadhi ya protocol ambazo zinatufanya tuweze kufaidika zaidi. Hiyo hofu inaweza ikawa ilikuwa inatokana tu na kutokuelimisha watu ambao wanaweza wakafanya biashara vizuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine ambacho ningependa tu kukizungumzia cha mwisho ni huu urahisi wa hizi certification wakati wa kusafirisha haya mazao. Kwa sababu inazungumzia, wakati unapotaka kusafirisha upate wapi vibali vya kusafirishia. Sasa kuna mlolongo wa vibali kwenye nchi mbalimbali, hata kwenye nchi yetu unakuta kunakuwa na mlolongo wa vibali vingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni lazima tuweke one stop center ya certification ili mtu anapokwenda awe na one stop center ya certification. Anataka ku-export, haya hiyo Phytosanitary Certificate aipate pale pale ambapo ambapo anapata kibali cha ku-export, aipate pale pale ambapo anapatia leseni, hizi tunazozungumza hizi center ambazo ni sehemu moja na hizi za Phytosanitary ziwepo hapo ambapo tayari tumeshaanza kurahisisha. Isije ikawa tunatengeneza hii kikawa kikwazo sasa; mtu amefika kwenye One Stop Center anapata vibali vyote, anaambiwa sasa Phytosanitary huna, Sanitary Certificate huna, hiyo katafute Wizara ya Kilimo.

Kwa hiyo, ku-merge kwa sababu hiki ni kitu kipya, kuna importance ya ku-merge hiyo ili ije isababishe sasa ule urahisi uwepo. Pale palipowekwa zile One Stop Center; TRA, sijui nani, wote wale, naye awepo. Kama kuna haja ya kuangalia document mahali, iwe rahisi zaidi ili hii isije ikazalishwa kuwa barrier. Tusaini halafu baadaye iwe barrier wakati wa implementation.

Mheshimiwa Naibu Spika, yangu yalikuwa ni hayo. Nashukuru sana. (Makofi)