Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

MHE. OTHUMAN HIJA JUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Mwaka 2021/2022.

Pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu kwa namna alivyoanza kuonesha uwezo mkubwa wa kuliongoza Taifa letu. Namuombea kila la kheri katika maisha yake na tatu, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na hatimaye kuiwasilisha hotuba hii kwa ufanisi wa hali ya juu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kuhusu sera na mikakati ya kuongeza mapato; Mheshimiwa Waziri ametaja hatua kadhaa kama nane hivi ambazo kama tukizisimamia zitatuwezesha kufikia malengo ya Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hatua hizo bado kuna maeneo ambayo kama Serikali ikiziboresha zinaweza kutuongozea mapato ya ndani. Moja katika sehemu hizo ni sehemu ya bandari bubu. Bandar bubu ni moja kati ya sehemu nyeti sana ambazo kama zikiboreshwa zinaweza kutuongozea mapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu katika suali hili ni kuiomba Serikali kuziboresha kwa kuzipelekea wafanyakazi wa Mamlaka za Mapato wenye kutambulika na Serikali na wenye ujuzi wa kufanya kazi za ukusanyaji wa mapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili ni kuhusu Jeshi la Polisi; naipongeza sana Serikali kwa kuwaondoshea askari tatizo la ajira. Tatizo hili ni la muda mrefu sana na lilikuwa linawadhalilisha askari wetu. Lakini hatuba hii imeacha kuzungumzia makazi na vitendea kazi kwa askari wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya muda wa zaidi ya miaka hamsini bado kuna maeneo ambayo makazi ya askari wetu hayaridhishi, majengo ni mabovu sana ambayo hayastahili kutumika na askari wetu. Ushauri wangu katika jambo hili ni Serikali kulishughulikia kwa nguvu zake zote suala hili la makazi na vitendeya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu ni kuhusu wakulima wadogo wadogo; lazima tukubali kuwa katika nchi hii wakulima wetu wanafanya kazi kwa bidii kubwa lakini bado wanakwazwa na mambo kadhaa katika maisha yao ya kikazi. Wanakabiliwa na upatikanaji wa pembejeo kwa kiasi kikubwa sana. Bado mazingira ya utendaji wa kazi zao sio rafiki. Aidha, wakulima wetu wanakabiliwa na uwezo mdogo kifedha. Mabenki yanawapatia mikopo yenye riba kubwa sana ambayo yanawapelekea kufilisika kabisa. Ushauri wangu katika jambo hili kwa Serikali ni kuwatengenezea mazingira mazuri ya kupata mikopo yenye mashart nafuu ili waweze kujiendeleza na kazi zao hizi. Naunga mkono hoja.