Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili kuweza kuchangia katika bajeti hii ya Serikali. Pia nitumie nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya njema na kuniwezesha kufikia siku hii ya leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nipende kuungana na Wabunge wenzangu hasa akinamama kwa jinsi ambavyo tumeona hizi siku 100 za Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan, ambazo zimeonyesha kwamba nyota nzuri huonekana asubuhi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, alipotuita pale kwenye mkutano sisi akinamama kwa kweli alizungumza maneno ambayo yalitugusa akinamama wote kwa ujumla na pia Bunge waliona upweke walivyoona akinamama hatupo Bungeni. Kwa hiyo akajua kwamba akinamama ni watu muhimu katika jamii yoyote ile. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niongelee mambo ya TARURA, kuongeza ile Sh.100 kwenye kila lita ya mafuta ni jambo nzuri, lakini kama fedha hii haitakuwa ring fenced, kama fedha hii haitatumika specifically kwa ajili ya kutengeneza barabara za vijijini na mijini iliyoko under TARURA, dhambi hii haitamwacha salama Waziri Mwigulu Nchemba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunajua ni wazi kwamba kuongeza Sh.100 kwenye kila lita la mafuta itaongeza gharama za vitu mbalimbali ikiwepo usafiri wa malori ambayo yanabeba bidhaa mbalimbali kupeleka vijijini. Kwa hiyo, kama wananchi hawataona kwamba kweli zile barabara zimetengenezwa, watajua kwamba hapa Serikali ilikuwa inataka kuwatumia kwa kuwadanganya ili na sisi Wabunge tui-support hii measure iliyochukuliwa, halafu sijui hii lawama kama haitafanya kazi ile fedha hiyo iliyotegemewa, Bunge hili tutaficha wapi sura zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nina wazo moja tu au nina weza kutoa maoni kidogo. TARURA wamekuwa hata vijijini wakitumia contractors au wakandarasi. Hawa wakandarasi wanakuja kutengeneza barabara hizi wakati wa kiangazi ambayo kwa kweli tunategemea iwe hivyo, lakini wanachofanya yale ma- grader wanapitisha mara moja, mtu ukipita unaona barabara inatengenezwa, baada ya miezi miwili mvua ikinyesha, barabara hakuna.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tunaotoka sehemu za milimani tumeona pesa nyingi zimetumika sana kwa TARURA, lakini mifereji haitengenezwi, zile sehemu korofi hazitengenezwi imara, matokeo yake baada ya muda mfupi tu mvua ikinyesha mara moja, mara mbili barabara hazipitiki, mabasi hayaendi, malori hayaendi, balaa kubwa kwa wananchi wakati fedha za mlipakodi zimetumika kwa ujanja, ujanja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba nishauri kwamba wakati nafanya internship kule ILO - Geneva nakumbuka kwamba kazi kubwa ambayo ILO alikuwa anasisitiza ni labour intensive, activities hizi zitumie labour zaidi kuliko equipment na kwamba equipment itumike pale ambapo panaonekana kuna hali ngumu ambayo haitaweza kutumia wananchi. Kwa mfano, wakati huko nyuma tulikuwa tunaona kwamba kulikuwa na hizi zinaitwa PWD – Public Works Departments vimewekwa vibanda kila sehemu za barabara zetu na wale wafanyakazi walikuwa wanapewa vifaa kwamba wao wana-monitor, wakiona kuna sehemu ina shida wana-repair mapema.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nashauri, Serikali yetu hii izungumze na TARURA wajiongeze, wafundishe wanavijiji wetu, vijana wetu, kule kwenye vijiji, kwenye kata jinsi ya ku- repair kufanya periodical maintenance ya hizi barabara, wawape vifaa kama machepeo, wheelbarrows, mafyekeo, ambavyo wao baada ya contractor kuondoka wataendelea na ile maintenance ya zile barabara ili ziwe sustainable. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaweza kutumia ile kama wanavyotumia force account, kuwe na posho ya kuwalipa hawa vijana, kwanza wata-create employment; pili watahakikisha kwamba zile barabara zinapitika throughout the year. Halmashauri zetu kwa mfano halmashauri ya Wilaya ya Same hatuna hata grader, hatuna hata equipment, ukichukua grader la kutoka Moshi kupeleka kwenye vijiji vyetu unaambiwa ulipe kwanza milioni tatu la kuliondolea pale na kila siku unalipa laki tisa. Sasa hapo kwa fedha hizi ambazo naamini ni nyingi, naamini Serikali ikiwa na nia njema itaweza kusaidia Halmashauri zikapata hizi equipment, zikaongeza ma-engineer wa TARURA ambao wataweza ku-monitor hizi activities ambazo zinafanywa na vijana wetu ambao tutaweka hizi building brigades au road brigades. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hilo nataka nizungumzie pia vikundi vya ujasiriamali, ile ten percent inayotengwa kwenye halmashauri. Experience imenionyesha kwamba akinamama licha ya jinsi ambavyo Rais wetu alizungumzia kuhusu hela ndogo inayotolewa kwenye hivi vikundi, lakini once wakishapewa zile fedha mgogoro unaanzia pale, vikundi vinasambaratika, wanagawana zile fedha na kazi haifanyiki ile iliyotarajiwa. Fedha hizi zilikuwa zinatengwa ili ziwe revolving fund, ili ziwe zinarudishwa wengine wanapewa, lakini haionyeshi popote pale kwamba hizi fedha zimekuwa zikirudi na vikundi vingine kupewa fedha hizo hizo imekuwa kila mwaka Serikali inatoa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nashauri kwamba fedha hizi badala ya kutolewa cash, kuna Maafisa Maendeleo ya Jamii, kwa nini wasitumie hizi fedha kununua equipment wakawapa vile vikundi, maana wao ndio wana- mobilize vile vikundi, wakawapa na kuwasimamia kuhakikisha wanafanya ile kazi waliyoitarajia. Kwa hiyo ningeomba kwamba Serikali iliangalie hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo nataka kuzungumzia, napendekeza TRA fedha inayotengewa iwe ya kutosha ili iweze kuajiri wafanyakazi watakaoweza kukusanya kodi. Pia CAG nashauri kwamba apewe hela za kutosha, apewe ruhusa I do know you call it ruhusa ya kuajiri wafanyakazi, because ameongezewa kazi ya ku-audit miradi zaidi kwa ajili ya kuona kwamba fedha za umma zinatumika vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunataka CAG kama alivyosema afanye -real time auditing aweze ku-curb problems za kupotea kwa fedha kabla hazijawa zimetumika vibaya, halafu ndiyo aje kukagua. Kwa hiyo tungesema kwamba CAG akipewa hizi fedha mapema anaweza kufatilia jinsi ambavyo bajeti hii itatumika. Tumeona huko nyuma kwa mfano kuna Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori ambao ulipata bilioni nne kwa ajili ya kufanyia usanifu wa jingo. Tangu wamefanya usanifu huo ni miaka minane sasa lile jengo halijajengwa ambalo ni la Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori, bilioni nne zimepotea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna ndege ambayo imetengenezwa zimetumika karibu bilioni nne, lakini hiyo ndege haijawahi kunyanyuka chini, ni mbovu siku zote. Sasa tunachosema ni kwamba, laiti CAG angekuwa na fedha za kutosha akaajiri wafanyakazi wa kutosha, akawa anafanya real time auditing angeweza ku-curb hizi proliferation ya hizi fedha zinazopotea bure.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri pia nchi yetu iunde think tank la watu wenye busara, wenye hekima wa uchumi, wenye kujua mambo ya uchumi, ambao wanaweza kuishauri Serikali yetu jinsi ya kuweza kufanya ufuatiliaji wa yale ambayo yanawekwa kwenye bajeti na jinsi ambavyo fedha inatumika ili kusudi isiwe tunapanga hiki na kinachofanyika ni kingine. Naamini kwamba hii pia itafanya mambo ya monitoring na evaluation ili tujue kwamba kweli fedha ya umma inatumika jinsi ilivyopangwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)