Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Hon Haji Makame Mlenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chwaka

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na mimi kuweza kupata fursa hii ya kuweza kuchangia jioni hii. Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufika hapa nikiwa katika hali ya uzima. Pili, ninakishukuru Chama changu Cha Mapinduzi kwa kuweza kusimamia mpaka ikafika hapa kuletwa bajeti ambayo kila mtu anaiangalia kwa mtazamo chanya. Nakishukuru sana chama changu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi ninaipongeza sana bajeti hii hasa kwa sababu imeweza kutaja maeneo mengi ambayo yanaenda kuwagusa wananchi wa nchi hii. Mfano wa maeneo hayo ni kama vile elimu, barabara, maji michezo, wafanyakazi, bodaboda, nakadhalika. Haya yote inaonekana kwamba Serikali imekusudia kufanya na kuleta maendeleo makubwa katika kipindi hiki cha awamu ya sita. Kwa hiyo na mimi nitatoa mchango wangu mdogo ili tuweze kuona namna gani tunaenda kuboresha zaidi ili kuweza kufikia yale malengo ambayo tumeyakusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu wa mwanzo nitaanza kugusa kupitia mifugo. Najua kwamba Serikali imeshajidhatiti hasa kupitia Waziri anayehusika na sekta hii. Wakati bajeti yake ilipopitishwa alijidhatiti na kuona kwamba anaenda kuleta mabadiliko makubwa ili kuweza kutimiza zile haja za wananchi na Bunge hili ambalo michango yao wameitoa. Lakini niweze kusema kuna maeneo ambayo yanaweza yakagusa wananchi hasa wale wa chini, kama vile ambavyo tumesema katika mpango wetu, kwamba tunaenda kuangalia maendeleo ya watu. Niseme kwamba Serikali ikasimame zile benki zetu ili ziweze kurejesha riba za mikopo, kama ambavyo mama ameshauri, kwamba mikopo ipunguzwe riba.

Kwa hiyo ikipunguzwa riba kuna makundi ya vijana kina mama, walemavu tunaweza tukawapa elimu na wakaweza kusomeshwa ili kuweza kutimiza haja zao kwa kupitia mifugo kama vile kuku. Inaonekana kwamba soko la mifugo hii ya kuku bado lipo kwa sababu soko hili bado linakuja kutoka nje, kuna import kupitia kuku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kama tutaweza kufanya vizuri maana yake sisi tunaenda kujiwekeza zaidi ili tufanye export badala ku-import. Watu wana import kutoka mfano Brazil na maeneo mengine kuleta kuku nchini ilhali sisi tuna uwezo mkubwa wa kufanya ufugaji huu na baadaye sisi tukaweza ku-export. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije katika dhana nyingine ambayo katika kichwa changu inaniambia kwamba tukiweza kuifanya basi ile adhma yetu ya bajeti nzuri tunaweza tukaifikia. Watu wengi wanazungumzia miundombinu, lakini nataka kuzungumza kuhusu jambo kubwa la huduma ambalo linaweza likasababisha kuona yale matakwa yetu yanaweza kufikia kwa urahisi. Kwa sababu inaonekana tukishindwa kulitilia mkazo suala la huduma basi tunaweza kutapanga mambo mazuri lakini yakashindwa kutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano niseme tu, bajeti hii kila mtu anayekuja hapa anaisifu; lakini si hapa tu hata kwenye mitandao watu wote wanaisifu bajeti hii kutokana na uzuri wake. Sasa tukishindwa kutoa huduma iliyokuwa sahihi maana yake hii bajeti haitakuja na majibu; na kama itakuja bila majibu basi tutabakia na vitabu vyetu kuwa vizuri, lakini hatutapata kile ambacho tulikikusudia kukipata katika jambo hili. Kwa hivyo niseme kwamba tuboreshe huduma hili yale ambayo tumeyakusudia yaweze kupatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano TRA tumesema kwamba tunaenda kujenga viwanda vingi, lakini baada ya kujengwa kuna watu ambao tumewapa kazi kwa kila mwezi kuweza kuvipitia na kupata huduma katika maeneo haya. Kama huduma hizi hazitakuwa stahiki maana yake tunaweza tukapelekea wawekezaji kutokuridhika na kuweza kuondoka, yapo maeneo ambayo tulipita tukaona kwamba wawekezaji waliondoka kutokana na huduma tu kuwa si nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo jambo hili la kuweza kutoa huduma bora tulitilie mkazo mkubwa sana; na nipendekeze kwamba katika eneo hili tuwape elimu, hasa TRA ambao wanaenda kukutana na wafanyabiashara katika muda wote ambao wanakutana na wanazungumza na wanapanga ili wafanyabiashara waweze kulipa kodi. Kodi hii bila kulipa katika hali ya kirafiki maana yake tutaendelea kuhesabu kusema kwamba tuna watu milioni zaidi ya hamsini lakini wanaolipa kodi ni watu milioni 5. Lakini iwapo kama dhana hii ya kutoa huduma itakuwa ni rafiki maana yake tunaenda kuongeza walipa kodi, kwa sababu kila mtu atakuwa ana nia ya kwenda kuwekeza lakini pia kulipa kodi kwa sababu huduma anayoipata ni rafiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niseme jambo lingine; mfano wa bandarini. Tukiiona bandari yetu maana yake ina hudumia nchi nyingi lakini bado hatujafikia viwango. Watu wanalalamika kwa kuona kwamba watu wanaondoka kutoka bandari yetu wanaenda katika sehemu nyingine lakini ukizingatia mbali ya miundombinu je, huduma yetu tunayoitoa watu wanairidhia? Na kama hwawataridhika maana yake wataondoka. Kwa hivyo lazima tuboreshe suala la huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini sana Serikali kwa namna ambavyo imejidhazititi na suala hili litapewa kipaumbele kikubwa hili kuweza kufikia malengo ambayo tunayataka. Sasa nije katika suala ambalo mimi mwenyewe linanipata mtihani mkubwa, suala la ubinafsishwaji wa benki ya FBME. Kwanza hapa ni-declare interest. Miongoni mwa waathirika na mimi ni mmoja wao. Kwa kweli jambo hili tukishindwa kuliangalia vizuri, Serikali na kwa sababu Serikali ndiye mdhibiti wa benki hizi za biashara ambazo zinakuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo wanastahiki kuangalia zile dhima ambazo Serikali wamebeba kwa ajili ya kuwafanyia Watanzania ambao wameathirika. Mimi mwenyewe tarehe 8 Mei 2017 wakati naondoka zangu naenda benki nikiwa sina pesa mfukoni, naenda benki mlangoni nakutana na polisi. Lakini kwa sababu sikuwa jambazi wala sikwenda pale kwa jambo baya sikujishughulisha nao. Nataka kuingia ndani benki wakaniambia soma hapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikakuta kwamba benki imezuiwa huduma. Pale bado kidogo nichanganyikiwe kwa sababu mfukoni nilishamaliza na pesa zangu zote zilikuwa ziko benki. Kwa kweli nimeondoka pale nimejikaza, lakini niko barabarani akili nilikuwa sina. Kwa hiyo jambo hili ni kubwa sana, na hapa limezungumzwa mara nyingi lakini ufumbuzi wake unakuwa mgumu. Mimi mwenyewe nimeenda BOT mara mbili kusikiliza jambo hili. Cha kusikitisha sana ninapoenda BOT nakutana na wananibembeleza na kuniambia usiwe na shaka. Pesa benki hii inayoza kutosha mtalipwa nyote na pesa nyingine zitabakia lakini mpaka leo hatujalipwa. Kwa hiyo hata wakibeleza inakuwa ni bure tu lakini kama mimi niliumia nikiwa mfanyakazi wa Serikali baada ya mwezi mmoja nikalipwa pesa zangu angalau nikapata kujizuiwa je, wale wengine ambao walikuwa si wafanyakazi wakoje

Mheshimiwa Mwenyekiti, na hapa kuna watu wamepoteza maisha yao kutokana tu na kuathirika na kukosa haki yao na benki hii kama tumeambiwa ina fedha za kutosha kwa nini atulipwi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Fedha ndiye msimamizi mkuu kupitia BOT. Wale wadau kama kule Zanzibar walikaa pamoja kutafuta njia na kuona namna gani tufanye na wakajikusanya wakachagua viongozi na wakaona namna gani tufanye. Wakaandika barua ya kuweza kuonana na Wakuu wa BOT. Barua hii hapa, Waziri naomba hii barua nimkabidhi aone namna gani, lakini majibu yake mpaka leo hayajapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ndiyo tunayozungumza ili huduma, kwamba kama hatutatoa huduma inayostahiki, basi watu wengine wanaweza wakapata taabu kwa sababu ni jambo dogo tu hili la kuwajibu na kukaa nao, kuzungumza nao wakawabembeleza kama ambavyo nimebembelezwa mimi, lakini lilikosekana. Kwa hiyo naomba mhudumu aje uichukue barua hii umpe Waziri ilia one namna njema…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)