Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Fedha na Mipango

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Fedha na Mipango

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nikushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuchangia katika hotuba hii ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Spika, kwanza, nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri na timu yake yote kwa hotuba nzuri ambayo ameitoa. Pia na wasaidizi wake wote katika ofisi yake kwa kazi nzuri ambayo wamekuwa wanaifanya wakitusaidia katika kutekeleza Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi maana kwa sehemu kubwa wao ndio wawezeshaji wakubwa ambao wanatupatia pesa ili tuweze kutekeleza miradi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nimesimama hapa kwa mambo kama mawili; jambo la kwanza ni ku-share experience katika kitu ambacho nataka nichangie nikikiita protection ya local industries au viwanda vyetu vya ndani. Maana nimejaribu kupitia katika baadhi ya details nikaona kwamba iko haja ya kupanua wigo wa kodi kwa sababu nakumbuka siku Rais anahutubia Bunge alitamka hapa akasema tujaribu kupanua wigo wa kodi. Sasa najaribu kuangalia vyanzo vipya vya kodi ambavyo vinaweza vikatusaidia ili hatimaye tuweze kuongeza mapato kule ambapo tunahisi kwamba mapato yalikuwa hayakusanywi vizuri ili haya ambayo tumeyapanga kuyafanya yaweze kufanyika kwa wakati na pesa zikiwepo.

Mheshimiwa Spika, cha kwanza, nilijaribu kuangalia trend ya biashara katika nchi hii. Nikawa najaribu kuangalia viwanda vya ndani na tozo za kodi mbalimbali, hasa importation ya vitu ambavyo vinatolewa nje na tunavyoviingiza hapa kuna kitu tunaita import duty, nikawa najaribu kuangalia duties ya baadhi ya vitu na experience yangu ya shughuli zangu za nyuma nikaona liko jambo la kufanya.

Mheshimiwa Spika, cha kwanza, nilikuwa napitia manufactures wa trailers, haya ma-trailers ambayo tunatengeneza. Nadhani kuna Kiwanda cha Super Doll, Simba Trailers na M Trailers nilijaribu kufanya research pale nikawa naona trend yao ya uzalishaji nikaona kwamba as time goes on trend imekuwa inashuka haipandi na employment so far ni kama ime-stuck, lakini ina stuck kwa sababu kumekuwa na unfair competition kwenye importers wa trailers na manufacturers wa trailers.

Mheshimiwa Spika, nataka niliseme jambo hili kwa sababu kwanza nilijaribu kuangalia kitu kimoja nikawa nawaza aliyeleta sera ya kwamba tupitishe sheria trailer linatozwa 10% ya buying price halafu gari tu la kawaida IST ambalo unajua hapa hamna mtengenezaji wa IST nikileta hapa la kwangu la kutumia ni mstaafu ni nini, natozwa import duty 25%. Sasa nikawa naona tunapotafuta kulinda viwanda vya ndani, maana nimejaribu kufanya research si hapo na sehemu nyingine nitaelezea, wenzetu kwa mfano Uturuki na China unapofanya export ya trailer lolote lile kuna export levy wanapewa na nchi zao; 17% mpaka 20%.

Mheshimiwa Spika, sasa mtu ambaye ana-export akapewa levy ya 17% na 20% maana yake huyo mtu tayari ana kitu anachoki-save kwa asilimia 17 mpaka 20. Unapo- save asilimia 17 mpaka 20 ukaja hapa Tanzania bado unalipa kodi import duty kwa asilimia 10. Already yule mtu kuna kama asilimia 10 ambayo ameshai-save kule anaponunua. Tukumbuke materials nyingi ya hivi vitu tunaagiza kutoka kule nje. Sasa tumekuwa tunajikuta kwamba tunasaidia kutengeneza biashara na kujenga viwanda vya nchi nyingine wakati tukisahau ku-protect watu wa kwetu hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wa kwetu hapa tuna faida gani tunapojenga viwanda? Hiki kitu nimekuwa nakisema mara zote, cha kwanza kikubwa ambacho tunakuwa nacho ni transfer of technology yaani tunachokililia hapa ni watu wetu wapate ujuzi wa kuvifanya vitu vile. Hii ni kwa sababu vyuo vyetu vya Tanzania kwa sehemu kubwa tunasoma theories na practical kidogo ile ya miezi mingapi tunayoenda field kule tunarudi sasa tunapopata viwanda tukakaa kwenye viwanda na sisi tukaweza kujifunza maana yake tuna advantage kubwa zaidi ya kuja kugundua vitu vingine ambavyo vinafanyika kule nje, tukiweza kuvifanya hapa vitapunguza importation hatimaye tuweze kujenga ajira hapa. Tuna vijana wa Kitanzania tunapowatengenezea ajira wale vijana maana yake wanalipa Pay as You Earn, SDL na halikadhalika pesa inayopatikana inabaki hapahapa. Kwa sababu tunapeleka dola kununua vitu nje na wao hawaji kununua vitu hapa, hatu-export vitu vingi hivyo maana yake balance ya Mheshimiwa Waziri kwa sehemu kubwa tutakuja kujikuta kwamba tuna pesa nyingi za kigeni ambazo zimeenda nje huku stock yetu inakuwa ndogo baadaye tunapata shida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba chanzo kipya cha kodi, kama mtajaribu kuliangalia hili jambo, tuongeze kwenye upande wa importers wa trailers ili tulinde viwanda vya ndani. Nilikuwa nawaza tukiongeza hata yenyewe ikawa 25% kuna shida gani? Mtu anayeona kwamba ni ngumu kununua hapa ina maana atatuongezea 15% kwenye kodi ambayo tunaililia hapa. Kama hataongeza ile atanunulia hapa kwa sababu bado kuna Watanzania wengine wananunua haya ma-trailers hapahapa na wanayatumia. Sasa anayeenda kutoa kule nje kwa sababu anapata unafuu wa bei na haji kulipa kodi kubwa hapa ndiyo maana anafanya hivyo. Kwa hiyo, hili jambo nilikuwa naliomba ili kuweza kulinda viwanda vya ndani.

Mheshimiwa Spika, kitu kingine nilikuwa najaribu kupitia kwenye miradi ya maji Mheshimiwa Waziri. Kuna mambo ambayo yamekuwa yanafanyika hapa, kwa mfano nakumbuka Hayati Rais Magufuli aliwahi kuuliza kwa nini tuna- design miradi ya maji kwa kutumia vifaa ambavyo haviko kwenye nchi hii? Hilo jambo mimi ni shahidi, unakuta mtu ana- design Ductile Iron Pipe, unajiuliza bomba la DI linapatikana India na China lakini tuna kiwanda pale Ubungo kinatengeneza mabomba ya chuma. Hakuna kitu ambacho kinafanywa na DI hakiwezi kufanywa na bomba la chuma la kawaida, lakini kwa sababu ya mtu na interest zake yeye mwenyewe ana-design kitu ambacho hakipo hapa.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba hata hayo mabomba kwa sababu yamekuwa na 10% tuyaongezee yapate 25% tuone kama kuna mtu ataya-design hapa. Kwa sababu tunavyoyatoa kule India au China yatashindwa ku- compete na mabomba ya hapa maana yake mabomba ya hapa yatakuwa cheaper kuliko yale kwa sababu tumeongeza kodi. Matokeo yake ni kwamba watu wata-opt kununua ya hapa, atakayeamua kuyaleta atatulipa 25% again tumeongeza kodi. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri hili jambo mliangalie.

Mheshimiwa Spika, lakini kuna jambo moja mimi niende nalo mbali. Last time nilikuwa Zambia wale watu wanakuuliza unachotaka kukiuza hapa kwetu hakipo? Yaani the first thing uwaambie kwamba ulichoendanacho kama unafanya mauzo kwao hakipo? Kama kwao hakipo watakusikiliza lakini kama kipo inakuwa ngumu. Same applies hata Uganda, Uganda wana sera yao wazi kabisa wanakwambia buy Uganda build Uganda. Hicho kitu Waganda wanacho kabisa yaani anakwambia lazima anunue kitu cha kwao ili aweze kuijenga nchi yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niombe hata sisi kama kuna uwezekano tuje na sera ya ku-protect vitu vya kwetu hapa. Tutamke Watanzania wajue akinunua kanga ya Tanzania anaijenga Tanzania. Watanzania wajue wakivaa vitenge vya Tanzania wanajenga Tanzania. Tusigombane hapa kwamba ma-container ya vitenge yame-park bandarini wameshindwa kuyatoa wakati tungekuwa tumewahamasisha Watanzania wakanunua vitenge ambavyo vinatengenezewa hapa kuna faida fulani, kwanza wangependa vya kwao lakini pili kuna saving tunaifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwa kumalizia harakaharaka kwa sababu ya muda, mimi naomba ni-declare interest nina jambo moja hapa. Mimi nimekuwa staff wa Air Tanzania nikifanya kazi kama cabin crew pale na baada ya kumaliza chuo nilirudi Air Tanzania kama Development Engineer. Nakumbuka niliondoka pale mwaka 2012 lakini kuna jambo moja ambalo limekuwepo pale kwa sehemu kubwa limewaumiza sana waliokuwa wafanyakazi wa Air Tanzania.

Mheshimiwa Spika, nakumbuka kipindi kile kipindi shirika limekwama pesa za mishahara zilikuwa zinatoka Serikalini, lakini pale Air Tanzania tulikuwa na SACCOS yetu inaitwa Wanahewa SACCOS, tunakatwa mishahara kwa sababu ya SACCOS, lakini pia pesa yao ya pension. Nadhani Mheshimiwa Waziri analielewa na Serikali iko hapa inalielewa. Ningeomba basi, kwa heshima maana watu hawa nimefanya nao kazi na wamekuwa wananililia, wananiambia kijana wetu na wewe upo Bungeni kama mwakilishi na wewe jambo linakuhusu. Naomba muwaangalie wazee wale, wengi sana wamekufa, wazee wapo kwenye tabu, lakini fedha yao ipo kule. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali ilisikie hili jambo kupitia kiti chako, tuwaokoe wazee hawa kwa sababu wamelitumikia Taifa, fedha zao zilikatwa kama pension lakini hazikupelekwa, fedha zao zilikatwa kwa SACCOS ya Wanahewa lakini hazikupelekwa. Leo wamestaafu lakini hawana chochote na mbaya zaidi nyote tunajua, Watanzania wengi wanavyokuwa wanafanya kazi wanakuwa wapo kwenye bima, wanalipiwa bima. Wakishamaliza miaka 60 akastaafu hata bima tu hana, tena labda hata tuje tena na sera hata ya kuwa-protect hawa kwamba kama alikuwa mtumishi aendelee kulipiwa bima mpaka anakufa angalau hata tuweze kuwasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu leo wanalalamika, fedha zao zimezuiliwa hawajazipata na matokeo yake hata wanaoumwa tu hawawezi kujitibia. Naomba sana kupitia kiti chako tuliangalie hili ili wazee hawa ambao wametoka kwenye hili shirika kwa shida kabisa, tuweze kuwasaidia na mimi mwenyewe nikiwemo humo, najua za kwangu nazo bado zipo ili hata mimi niweze kupata haki yangu kupitia huko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, kwa leo ni hayo machache, naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)