Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Fedha na Mipango

Hon. Twaha Ally Mpembenwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibiti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Fedha na Mipango

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi kuweza kuchangia katika hotuba hii ya Waziri wetu wa Fedha ambao ni Wizara muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kabla sijaanza kuchangia, nilikuwa namba nichukue fursa hii kwanza kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri kwa utulivu mzuri sana walionao. Lakini cha kusikitisha tu kwa Mheshimiwa Waziri ni pale tu ambapo timu anayoi-support haiendani na utulivu alionao. Nilikuwa naomba tu kama ikiwezekana ajifikirie mara mbili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kabla sijaendelea mbali kuchangia hii, naomba tu niseme kwamba kutokana na hali ambayo wanayo watani wetu wa jadi na Mheshimiwa Waziri yeye ni mpenzi sana wa timu hiyo, basi nilikuwa namuomba sana Mheshimiwa Waziri afikirie, ikiwezekana lile goli alilokuwa amelifunga kijana wetu Morrison wakati anacheza na timu ya Namungo kule Ruangwa, basi lifanyiwe credit rating ili sasa liweze kuwasaidia jamaa zetu waweze kwenda kukopea katika financial institution waweze kuendeleza timu. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia katika Wizara hii kwenye kifungu Na. 50 na kifungu hiki nagusa tu katika ile sehemu ya TRA. Nitachangia kwenye point moja tu na point hii ni suala zima la tax administration. Ni masikitiko makubwa sana kwenye TRA pale Tax Administration yetu haiko vizuri, kuna leakage katika tax system yetu. Hii leakage inasababisha sisi kama Serikali kukosa mapato mengi sana na mfano wake uko wazi kabisa. Sisi badala ya kuchukua solution kwenye kufanya tax administration, tunakwenda kuchukua solution katika kuongeza tax. Hii inaleta shida sana, tunakuwa hatuwasaidii kwa ujumla wake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, in recent past kulikuwa kuna issue moja inahusiana na masuala mazima ya mafuta ya kupikia/ crude oil kutokana na common market tulikuwa tumekubaliana kwamba itakuwa zero rated. Sisi Tanzania ilikuwa zero rated, lakini katika mazingira ya kutatanisha kutokana na tax administration, kutokana na leakage iliyopo ndani ya mifumo tukajikuta kwamba tunakwenda kutoza asilimia 10. Hii ni kwa sababu kuna baadhi ya wafanyabiashara walikuwa hawako honest enough, wanakuwa wanaleta semi refined wakati huo huo wana- declare kwamba wameleta crude oil.

Mheshimiwa Spika, cha kusikitisha, pale kuna TRA, TBS, and by then kulikuwa na TFDA. Hawa wote walikuwa wanaidhinisha kwamba hii ni crude oil, lakini in the real sense mle ndani kulikuwa na semi refined. As a result, Serikali tukaona kwamba tunapoteza mapato. Tulifanya nini? Badala ya kuwa na control nzuri katika tax system, tulichokifanya tukaenda kuongeza tena tax, tukasema wataenda kulipa asilimia 25. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa angalia, anayeathirika hapa ni mwananchi na bahati mbaya sana wenzetu kule katika common market ndiyo, Uganda wao wanakwenda katika asilimia 10 lakini jirani zetu Kenya wao ni zero rated crude oil. As a result, viwanda vyetu vilivyokuwa ndani, vinashindwa ku-compete na viwanda ambavyo viko kule Kenya. Sasa hii, athari yake kubwa ni kwamba tunakwenda kuwakandamiza wananchi lakini hatufanyi solution iliyokuwa sahihi kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba katika tax administration, Mheshimiwa Waziri uangalie sana kwenye eneo hili ili sasa kwa namna moja ama nyingine tuweze kuona ni jinsi gani zile leakage tunaenda kwenda kuzi-control. Katika tax administration hiyo hiyo naomba vilevile nizungumzie suala zima la electronic stamp system.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge mmoja amelizungumza vizuri na dada yangu Mheshimiwa Halima Mdee naye akaenda kulikazia. Naomba niseme tu hapa tuna shida. Shida iliyopo ni kubwa sana. Katika mfumo ule, nasema uko vizuri zaidi, tunafanya vizuri, katika baadhi ya maeneo tunafanya vizuri lakini bado tunapaswa twende kuongeza katika maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, shida kubwa ambayo ninaiona pale ni kwamba vendor ambaye kazi yake ni very simple ni ku-scan tu zile chupa halafu at the same time anakwenda kulipa fedha. Kwa mfano, research niliyokuwa nimeifanya pale Cocacola, bottles ambazo zinakwenda kuwa scanned katika msimu wa mwaka jana zilikuwa almost milioni 600 na katika kila chupa moja inakuwa-charged shilingi 900. Hii shilingi 900 haiendi Serikalini, inakwenda kwa vendor. Cha kusikitisha, tunao watu wa TTCL, TCRA wapo na wao ndiyo wataalam katika mambo ya mtandao. Tunaweza vilevile tukawa-equip wao wakaweza kwenda kufanya kazi hiyo ili sasa zile fedha zinazoweza kupatikana zinakuwa zinazunguka ndani. Hii ni shida katika tax administration yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama hivyo haitoshi suala lingine la kusikitisha zaidi sisi Wabunge tunaishi sana kwa kupitia wadau hawa. Kwa hiyo, tunapenda sana kuandika andika paper hizi tunakwenda kwa wadau basi wakiangalia pale wanapoweza kwenda kusaidia kwenye masuala mazima ya corporate social responsibility wanafanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilikutwa na mtihani mkubwa sana baada ya kuwa nimeandika paper kwenda sehemu fulani na kule nilikokuwa nimekwenda yule bwana akanipigia simu akasema bwana tunakuhitaji njoo. Nikajua nakwenda nimefanikiwa. NIlipofika pale, nilisikitika; kutokana na taratibu za kanuni zetu naomba tu nihifadhi kampuni hiyo. Nilifika, nilisikitika akaniambia Mheshimiwa Mbunge tungependa kukusaidia, lakini tunadai sisi Serikalini hapa hii tax return inakuwa ni shida upande wetu. Kwa hiyo, hili ni tatizo katika suala zima la tax administration. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki ambacho sisi tunacho hivi sasa, ni muhimu sana Serikali tukaanza kufikiria katika suala zima la tax refund, input and output VAT basi twende tukawarudishie wale corporate citizens ili sasa kwa namna moja ama nyingine waweze kuzizungusha zile hela katika mfumo na mambo yaweze kwenda kuendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili ni jambo la msingi sana kwa sababu tunajua kutokana na masuala mazima ya Covid, crisis za kiuchumi ambazo zimejitokeza in recent past, sisi kama Serikali hatuna budi. Najua tunao uwezo wa kuweza kutumbukiza stimulus package lakini kabla hatujafika huko basi hivi vidogo ambavyo tunaweza tukavifanya katika tax administration twende turudishe fedha zile ile fedha zile zirudi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, cha kusikitisha katika kampuni moja tayari kuna watu wameshafanywa kuwa redundant almost 600 peoples, watu hawa Serikali tunakosa tax. Hii inasikitisha sana. Kwa hiyo, nilikuwa naomba nisisitize kwa Mheshimiwa Waziri aweze kuliangalia hili kwa mapana yake ili sasa kuweza kuona tunakwenda kuweka internal control nzuri katika suala zima la tax administration. Sio tu tunaongeza tax, lakini tujue kwamba tunavyokwenda kuongeza tax, wanaokuwa wanaathirika ni wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukiwa hapo hapo katika suala zima la tax administration, napata shida kidogo katika suala zima la ku-quantify vile vigezo katika Jimbo moja au Wilaya moja na Wilaya nyingine jinsi ya kuweza ku-meet target ya kuweza kukusanya.

Mheshimiwa Spika, pale kwangu Kibiti, nina shida, najua tunafanya kazi vizuri, tunashirikiana karibu zaidi na watu wa TRA, lakini wakati mwingine inakuwa ni husstle kwa wananchi hasa ninavyoona mama zangu wale, mama ntilie wanakwenda kuwa chased out ili kuanza kwenda kulipia kodi. Hii ni shida ya msingi sana.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilikuwa naomba sana Mheshimiwa Waziri tuweze kuliangalia hili ili sasa tuweze kuona vigezo vile ambavyo vinasababisha kuweza ku-meet target katika Jimbo au katika Wilaya moja na wilaya nyingine. Hili ni suala la msingi na haya yote yapo katika suala zima la tax administration. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama hiyo haitoshi, hapa hapa katika suala zima la tax administration ni ukweli ambao ulikuwa wazi huwezi kuingia peponi lazima ufe kwanza na ukifa hakuna atakayethibitisha kama unakwenda peponi au unakwenda motoni. Hatuwezi sisi kukusanya kama hatuwezi ku-spend. Lazima tuweze ku-employ enough people ili sasa tuweze kuona wanakwenda kutusaidia katika kuweza kufanya collection. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pale kwangu Kibiti tuna watumishi watatu wa TRA mbaya zaidi watumishi hao watatu wanahudumia vilevile Wilaya ya Rufiji. Sasa hapa mimi napata shida yaani ili tuweze ku-enjoy huwezi ukaenda peponi u-test kwanza kifo, toa fedha ajiri watu. Watu hao utakaoenda kuwaajiri ndiyo watakaoweza kwenda kukufanyia kazi ya kukusanya mapato. Kwa hiyo, nashauri sana hilo lifanyike. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba tu nirudi kwa Mheshimiwa Mbunge mwenzangu wa kule Ujiji. Yeye aliuliza, je, ni busara na mimi nauliza hivi ni busara kweli wilaya mbili zinahudumiwa na wafanyakazi watatu wa TRA halafu tunategemea tuwe na efficiency? We can not be able to move in this way. Kwa hiyo, naomba sana suala hili Mheshimiwa Waziri aweze kuliangalia kwa mapana yake ili sasa tuweze kuona kwa namna moja ama nyingine tunakwenda kuongeza mapato.

SPIKA: Kwa hiyo, Mheshimiwa Mpembenwe kwa kila Wilaya moja mtumishi mmoja na nusu?

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Spika, hiyo ndiyo hali halisi, halafu tunategemea tuwe na efficiency katika maeneo hayo, hii ni shida kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba sana Mheshimiwa Waziri anapokuja kufanya hitimisho lake basi tuweze kuangalia ni jinsi gani atakavyoweza kuajiri wafanyakazi waweze kwenda kutukusanyia kodi. Nasi tuweze kwenda kuzungumza kule kwa wananchi kodi zinazokusanywa zinakwenda kutumika katika mambo ya shule, TARURA na sehemu nyingine. Kelele hizi tunazozipiga sisi Waheshimiwa Wabunge TRA wasipoweza kufanya kazi nzuri ya kukusanya mapato hatuwezi tukafanikiwa kwa namna moja ama nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine la msingi zaidi ambalo naomba nilisisitize ni hapohapo kwenye suala zima la tax administration…

SPIKA: Haya, malizia basi nakupa dakika mbili.

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi narudi pale kwa Mheshimiwa Mbunge mwenzangu asubuhi alivyokuwa ameanza kuzungumzia suala zima la mambo ya interest rate. Hapa kuna tatizo kubwa sana la msingi na katika kifungu namba 50 vilevile central bank wanahusika. Why can’t we do our borrowing ikawa cheaper ili sasa tuweze kurahisisha maisha kwa watu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu kinachotokea borrowing is very expensive kwa wananchi wa kawaida, lakini vilevile kwa corporate citizen. Sasa hili jambo Mheshimiwa Waziri kaa na wataalam wako tuweze kuangalia jinsi gani tutakavyoweza kucheza na fiscal policy zetu, borrowing yetu ikawa cheaper ili sasa tuweze ku-stimulate uchumi wa ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima na unyenyekevu wa hali ya juu naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)