Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati

Hon. Salma Rashid Kikwete

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mchinga

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati

MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na wataalam wote wa Wizara kwa kazi nzuri ya kuwapatia Watanzania umeme takriban nchi nzima.

Mheshimiwa Spika, katika Jimbo letu la Mchinga, tuna maeneo kadhaa ambayo hayajafikiwa na umeme. Maeneo hayo ni Kijiji cha Ruvu (Kata ya Mchinga), Kijiji cha Dimba(Kata ya kilolambwani), Kijiji cha Matapwa(Kata ya Mipingo), Kijiji cha Mnyangara (Kata ya Mipingo), Kijiji cha Lihimilo (Kata ya Mipingo)na Kijiji cha Namkongo (Kataya Mipingo).

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.