Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia katika Wizara hii ya Viwanda na Biashara. Kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza sana Waziri wetu wa Viwanda na Biashara, Naibu Waziri na watendaji wote maana kazi kubwa wameifanya na hotuba nzuri imesomwa hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda nadhani nina dakika saba tu na vitu ni vingi nadhani niweze kwenda haraka haraka. Jambo langu la kwanza ambalo ninalo tuna hii issue ya Special Economic Zone, nilikuwa najaribu kupita nimeona tulijiandaa ni karibu kila mkoa uweze kutengeneza kongani kwa ajili ya viwanda, lakini sasa nikawa nawaza jambo moja, nimejaribu kuangalia katika research zangu nikawa naona viwanda vingi sana ambavyo vimejengwa katika wakati uliopita vimejengwa Mikoa ya Pwani na Mikoa ya Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikawaza nikasema kwanini viwanda vingi sana vimejengwa Pwani na Dar es Salaam wakati sikusema labda malighafi nyingi sana ziko pale, lakini kitu ambacho nimekiona viwanda vingi vilivyojengwa ni viwanda vya process, unakuta mtu analeta raw material kutoka nje ya nchi ana i-process akimaliza ku-process inakuwa product ambayo tunaitaka anaweza kuiuza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikawa nawaza sisi wa Mkoa wa Kagera, kilometa 1,400 kutoka bandari ya Dar es Salaam, watu wa Mara Kigoma kilometa 1500, tutakapo jenga viwanda ambapo tunaleta malighafi kutoka nje ya nchi tukaenda kujenga vile viwanda kwetu Kigoma, kwetu Kagera, sidhani kama tutaweza kuwa competitvetuweze kushindana na watu ambao wanajenga vile viwanda maeneo ya Pwani. Kwa sababu hakuna mfanyabiashara ambaye hatakuwa tayari kuja ku-invest Kagera na Kigoma at is the same incentiveambayo na mtu wa Dar es Salaam anapata na mtu wa Pwani anapata yeye aongeze kilometa zile aende kule aweke kiwanda, halafu kesho wakati wa kuuza mtu yule akashindane na mtu aliopo Dar es Salaam. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umeshaongeza cost of transportation container moja mpaka ulifikishe Kagera la forty feets ni milioni sita, ufikishe Kigoma ni milioni sita, kuja na kurudi kama ile product utakayouza Dar es Salaam ni milioni sita unaongea forty feets imeshaongeza milioni 12, wakati aliopo Dar es Salaam ka-clear kwa 350,000, mzigo unaingia sokoni. Sasa nilichokuwa naomba kwa Wizara ya Viwanda tujaribu kuweka mkakati maalumu wa kuona na sisi maeneo yetu ya huku tuweze kuweka uwekezaji yaani tuweze kuweka vivutio kwa ajili ya uwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama na sisi tunasema watu wakawekeze Kagera, wakawekeze Kigoma, wakawekeze mikoa mingine ya pembeni huku tuwe na incentive ambayo Serikali inatoa, waone kuna unafuu fulani kwao ili hata kama tukiwaambia wakaweke viwanda kule waweze kuja kuweka viwanda unless otherwise sasa viwanda hivi vitaendelea kubaki Dar es Salaam na Pwani tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kitu kimoja cha muhimu ambacho ninacho, mimi nina declear kwamba niko kwenye Kamati ya Viwanda na Biashara tulitembelea Ubungo pale EPZA, kuna watu pale wanazalisha jeans wanapeleka Marekani, lakini kitu ambacho niliona wakati wa ziara wanatoa material kutoka Pakistan wanaleta garments kabisa ambayo iko tayari kwa ajili ya kushona kinachofanyika pale ni kama fundi cherehani wanashona tu zile nguo, alafu wana export kwamba zimetoka hapa alafu wanapeleka Marekani, maana analeta under Special Economic Zone halipi kodi anamaliza pale tena ana export halipi kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nilichokuwa naomba ni kitu kimoja, amemaliza kuongea Mheshimiwa Nyongo hapa, mimi natoka Kanda ya ziwa katika Jimbo langu la Biharamulo tunalima pamba pia, wakulima wa pamba wako wengi sana hapa ni aibu kuona pamba inatolewa hapa, tuna export pamba inaenda nje ya nchi, wale jamaa wanaenda wana process wanatangeneza garments za kutengenezea jeans Pakistan halafu the same pamba ambayo tulipeleka sisi inatoka Pakistan inakuja Ubungo inashona, inamaliza kushona inapeleka Marekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokuwa nasema ni nini, viwanda hivi vya kimkakati ambavyo tunavyovipanga, tupange viwanda vya kimkakati ambavyo vitatumia raw materials ambazo ziko kwenye sehemu zetu. Sidhani kama kile kitu kinachofanyika Pakistan kinashindwa kufanyika hapa, maana tuna viwanda vingi ambavyo vina process vitu hapa na tumeonesha kwamba tunaweza kufanya vitu ambavyo vinafanyika nje vikaweza kufanyikia hapa. Nilichokuwa naomba kwa upande wa Wizara ya Viwanda sasa, maana ninyi ndiyo custodian wa suala la biashara na vitu vingine hapa, muende mkatusaidie mkae na TIC, mtusaidie, wawekezaji wanapokuja washaurini wawekezaji kwa sababu tayari tuna client anayetengeneza jeans hapa na ana export jeans nyingi sana. Sasa kwa sababu tuna client anaye export jeans hapa na pamba tunayo tutafute wawekezaji wa kwenda kuweka viwanda Kanda ya Ziwa tunapolima pamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakishaweka viwanda Kanda ya ziwa tutowe pamba sisi kwanza tukishatengeneza vile tutapata mashudu kwenye pamba, tutapata mafuta haya tunayo import kutoka nje, kutakuwa na advantage nyingi. Yule mtu akishamaliza kutengeneza garment tutoe pale tulete Ubungo pale tukamuuzie. Najua ipo shida maana katika maongezi na mtu mmoja aliniambia hatuna capacity hiyo, hakuna mtu ambaye yuko tayari kulima pamba hapa kwa shilingi 1,000; akakope pesa benki alafu pesa ifie kule wauze assets zake. Lakini kama soko liko pale Ubungo tuna hakika kwamba watu watalima pamba na kinachotakiwa anayekuja kuwekeza kwenye kile kiwanda hakishakuwa na shamba lake yeye mwenyewe la kulima pamba ni kwamba hata kile kiwanda chake hakitakufa, maana tumekuwa na shida moja sana Watanzania, unakuta mimi nimwekeza kwenye kiwanda, unapowekeza kwenye kiwanda hata kwa wenzetu wanachokifanya huwezi kutengeneza excavator tunaona caterpillar yale barabarani, kuna anaye muuzia engine, kuna anayemuuzia vitu vingine, kuna anayemuuzia ticks, inakuwa combination kiasi kwamba kabla ya kiwanda chako wewe kufa unayetengeneza caterpillar kuna stakeholders wengi sana huku nyuma yako wana feel uchungu kabla ya wewe kuweza kuathirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa shida yetu sisi utakuja kukuta kiwanda unacho wewe tu, raw material unatoa nje kwa hiyo hata kesho kiwanda kinakufa hakuna mtu anayeumia hapa, lakini tukiweza kutengeneza viwanda ambavyo ni feeders wa viwanda vingine ambavyo vipo hapa nina hakika hata vile viwanda vikubwa havitaweza kufa kwa sababu tayari kuna mtu ananufaika navyo pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kitu kingine ambacho ninacho kwenda kwa Serikali, kuna jambo moja ambalo nimekuwa najiuliza sana, mimi nimekuwa nafanya kazi ya sales naweza ni-declare interest, kitu kimoja ambacho watu tumehusika na maunzo sehemu nyingi tulipo, lazima usimame katikati, unasimama katikati kwa client na unasimama katikati kwa kampuni, unaangalia maslahi both sides. Sasa sehemu kubwa sana ya viwanda wafanyabiashara wamekuwa wanaachwa kama yatima, ninachoomba kwa Serikali hasa kupitia Wizara ya Viwanda wa Biashara tunapolia humu tukawa tunasema viwanda, viwanda, kazi yenu nyie kubwa ni mambo ya viwanda na wafanyabiashara. Simameni na wafanyabiashara maana mfanyabiashara anapokufa hebu feel kwamba kuna kitu mimi nimepoteza kwenye sehemu yangu ya kazi maana hawa watu wanakuwa wanalia kodi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka kipindi cha nyuma niliwahi kuelezea hapa tulivyoenda pale Ubungo mtu mmoja amefunga kiwanda anapeleka Uganda, wakati tunaongea pale tunaambiwa TRA. Sasa nikawa najiuliza hivi TRA ni nani? Maana mimi nakumbuka wakati nafanya kazi nilikuwa nagombana sana na wahasibu unaleta mteja pale mhasibu akija naye anakubalikia wakati unatafuta mteja mhasibu hayupo, lakini siku unamfikisha pale anasisimama anataka hiki anataka hiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mimi nikuombe Mheshimiwa Waziri hii kazi ya kutafuta wateja ni yako tunachotaka utuhakikishie kwamba unapoangaika kutafuta wateja huyu TRA wanajua unatumia nguvu kuwatafuta, sasa msimalize kuwapata watu wanajenga viwanda hapa, kesho mtu mwingine anaweka kikwazo hivi viwanda vinafungwa itakuwa ni aibu kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nina hakika direction yetu ni nzuri, tumemsikiliza Rais hapa alivyosema, kwa hiyo, nina hakika tukiji-tune katika kuhakikisha tunajenga mazingira mazuri ya kuwasikiliza wafanyabiashara, haiwezekani mtu akaweka bilioni 250 hapa halafu wewe huwezi kwenda kukaa naye mezani ukamuuliza ana matatizo gani? Akaweka bilioni 300 hapa huwezi kwenda kukaa naye mezani ukajua anamatatizo gani? Hizo atazipeleka Uganda, atazipeleka Kenya, atazipeleka Zambia na sehemu nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nadhani baada ya hayo kwa sababu ya muda nilitaka niongee issue ya Liganga na Mchuchuma lakini wenzangu wameshaongea ni sehemu ambayo itatusaidia sana sana, maana kama unaagiza mzigo China, ukiomba quotation ya product yoyote ya chuma China hawawezi kukupa quotation ya thirty days kwenda nje, sana sana ya siku kumi/siku saba kwa sababu bei ya chuma inabadilika kila wakati. Sasa suala la Linganga na Mchuchuma tulichukulie serious ni sehemu itakayotunyanyua sisi hapa maana product za chuma hata tunavyoziagiza huko nje ni very expensive na bei zinapanda kila siku. Nyote ni mashahidi kama kuna mtu anafanya biashara hapa tumesikia China juzi wameongeza 13 percent kwenye export zote. Kwa hiyo, kama hata kuna mzigo ulikuwa umeagiza China leo umeongezeka kwa asilimia 13 kwa sababu bei ya chuma ilivyo fractuate. (Makofi)

Kwa hiyo, niombe suala la Liganga na Mchuchuma Serikali ilichukulie serious ili sasa liweze kututoa hapa, tuunze chuma hapa kwa majirani zetu kama sisi tutashindwa kutumia hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuyasema hayo naomba niunge mkono hoja, ahsante sana.(Makofi)