Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo

Hon Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo

MHE. JUMANNE A. SAGINI: Mheshimiwa Spika, mchango wangu wa maandishi ni kama ifuatavyo:-

Kwanza, Serikali iongeze miradi ya umwagiliaji hasa kwenye Wilaya na Mikoa inayopakana na maziwa na mito ikiwemo Ziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa, Manyara, Eyasi na Rukwa. Hii itasaidia kupunguza utegemezi wa mvua hasa kipindi hiki chenye changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.

Pili, Serikali ifanye uamuzi wa makusudi wa kuajiri Maafisa Ugani wa kutosha kwenye Mikoa na Halmashauri ambazo kilimo cha mazao ndiyo shughuli yao kuu ya kiuchumi. Kwa kufanya hivyo, tutasaidia kuongeza kwa kasi tija katika kilimo cha mazao.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana na naunga mkono hoja.