Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii pia niweze kuchangia kwenye hotuba hii ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, nadhani nianze kwanza kwa kuipongeza Wizara kwa hotuba nzuri ambayo wameitoa, lakini pia niseme tu jambo moja, nitapenda zaidi kujikita kwenye sehemu ya mifugo hasa kwenye masuala ya ng’ombe kwa sababu mwenyewe historia yangu nimezaliwa kwa wafugaji, nimechunga sana ng’ombe nikiwa mdogo, kwa hiyo, kidogo ni kitu ambacho nakielewa na nimekiishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa haraka kuna jambo moja ambalo nimekuwa najiuliza alichangia mwenzangu bwana Maganga hapa tangu zamani hata kabla sijaingia kwenye siasa nimekuwa najiuliza kuhusu wafugaji wa Tanzania. Yaani wafugaji wa Tanzania wamekuwa kama yatima always ni watu ambao ni watu wa kufukuzwa fukuzwa, ni watu ambao wanaonekana wanakosea kosea kwenye vitu vyao vingi wanavyovifanya, sasa nikawa niwaza Wizara ya Mifugo mnajua kwamba mna mtoto ambaye ni mfugaji na bado anakimbikizwa kimbizwa, lakini bado hamchukui hatua ya kum-protect? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayasema haya kwa sababu wafugaji hawa sijui wanamakosa gani, kwa mfano kwa upande wa Biharamulo ni eneo ambalo tuna mifugo mingi sana na baada ya kuingia hasa wakati wa kampeni nimekuwa nikiuliza maelekezo ilikuwa ni kwamba tuna-ranch zimetengwa Karagwe, ranch zimetengwa Misenyi sasa nikawa najiuliza Mkoa mzima wa Kagera tutaenda kufugia Karagwe na Misenyi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba labda tusaidiane kwenye jambo moja, wafugaji wetu wa Kata ya Kaniha kuna Kijiji pale kinaitwa Kijiji cha Mpago, wiki mbili zilizopita bwana mmoja wamemkamata ng’ombe wake akatozwa faini shilingi milioni saba, mwingine naye akatozwa faini ya shilingi milioni tano, reason ng’ombe wameingia kwenye hifadhi ya TFS.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nikawa najiuliza swali moja wewe ni mfugaji, let say ni mfugaji, nafuga kule kwa sababu tumehamasishwa kufuga, nipo Bungeni hapa sasa hivi vijana wanaochunga ng’ombe wapo karibu na hifadhi ng’ombe wameingia mle, mtanzania yule anatozwa shilingi milioni saba at per kama hajatoa milioni saba ng’ombe wote sabini wanaondoka najiuliza hata Waheshimiwa Wabunge tumo ndani leo tukimnyanyua mtu milioni saba ambayo haikutegemea papo aitoe hapa sidhani kama kuna mtu yupo hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikumbukwe wale watu wapo maskini, wapo vijijini kule ni maskini kabisa, faini ya kumtoza mtu shilingi milioni saba mtu ambaye juzi Kijiji cha Mpago kamati iliyoundwa wamesogeza mipaka, hawajaweka alama TFS, lakini wafugaji wetu wameshaanza kukamatwa wanatozwa hela yote hiyo, lakini hawa ni Watanzania tunahamasisha kwamba ufugaji uendelee, mnalenga leo kutengeneza maziwa kutoka lita bilioni 2.7 mpaka lita bilioni 4.5 yatatoka wapi kama hawa watu wapo disturbed kiasi hiki na hawana sehemu ya kulishia ng’ombe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ilani ya CCM imeahidi ukurasa wa 51 kwamba tunataka tuongeze malisho, sehemu ya kulishia kutoka hekta milioni 2.7 mpaka hekta milioni sita. Sasa hizi hekta milioni 2.7 na hekta milioni sita kutoka hapo hiyo range tunaipata wapi? sisi wananchi tunaipata wapi kama siyo Wizara ya Mifugo ndiyo itabidi ifanye kazi hiyo ya kuitafuta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo maeneo ambayo mnataka muyaongeze nani anayamiliki, tungekuwa tunamiliki wananchi wenyewe tungepeana, lakini yanamilikiwa na Serikali kupitia TFS. Sasa tunachowaomba ndugu zangu wa mifugo, ninachowaomba kwa niaba ya wananchi wangu sisi tuna eneo kubwa sana Kata ya Nyantakara pale tunaomba mfunge safari mje Biharamulo muwaambie wafugaji wa Biharamulo kwamba eneo lipo hapa kaeni na TFS, maana Biharamulo kwa sehemu kubwa tumezungukwa na mapori, kwa nyuma huku tumezungukwa na hifadhi ya Burigi Chato ambayo off course tunashukuru Mungu watalii wataanza kuja tutapata fedha za kigeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo mengine yamehifadhiwa wananchi hatuwezi kwenda kuomba TFS hawatatuelewa ila wewe custodian wa mifugo ni kazi yako kuwatafutia wafugaji wako maeneo. Nyie mwende mkaongee na Serikali maana Serikali kwa Serikali mnashindwanaje? Ila wananchi huku wanaumia, nayaongea haya kwa uchungu kwa sababu wakazi wa Biharamulo tunajua tulivyoteseka na haya mapori. Sasa mnavyoyaacha mnataka wale jamaa warudi tena waanze kutuimbisha mtaji wa maskini nguvu zake mweyewe, tumeteseka mno tulikuwa tunashushwa kwenye magari usiku tunapigwa viboko, leo tumeshakaa vizuri sasa maeneo haya iyambieni TFS nyie watu wa mifugo wawakatie maeneo wafugaji wa Biharamulo wapate eneo la kufugia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina haja ya kushika shilingi, lakini ninachoomba sasa nyanyukeni mkae na wenzenu wa maliasili kwa sababu maliasili hatuwezi kuomba sisi, waombeni nyie watenge maeneo ili wakazi wa Biharamulo wapate maeneo ya kufugia, nina wafugaji wengi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa imekuwa ina-prompt watu maliasili wapo hapa, mwezi wa pili nadhani walikuja wakamfukuza mkuu wa TFS pale na viongozi wengine, wafugaji wa Biharamulo wamekuwa wanalipa pesa, wanachanga, pesa nyingi mpaka milioni 50 wanawalipa viongozi, viongozi halafu wanawaruhusu wanaingiza ng’ombe, angalia mfugaji huyu anavyodhulumika, kwamba hana eneo la kuchungia inabidi amlipe mtu wa TFS amruhusu aingie yaani Mtanzania mwenyewe hata eneo la kuchungia ng’ombe unanunua, lakini bado Serikali ipo hapa inasema inataka ikuze ufugaji, kwa hiyo naomba hili jambo mliangalie nyanyukeni mkatusaidie na hapo. Sina haja ya kuendelea sana kwenye masuala hayo nadhani mmenielewa, rafiki yangu Mheshimiwa Ulega unaniangalia umenielewa vizuri njoo unisadie ili wakazi hawa wa Biharamulo wapate eneo la kufugia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lipo jambo moja nimekuwa naliangalia kuhusu ufugaji wa Samaki, kwangu kule mwanzo watu walihamasishwa wafuge samaki, watu wengi sana wamechimba mabwawa kwa ajili ya kufuga samaki mabwawa yale yamekauka hayana maji na watu wengi sana wamepata hasara, sasa ameongea sana bwana Mheshimiwa Mwijage hapa asubuhi Mheshimiwa Mwijage ni mtaalam sana wa mambo ya samaki kwa sababu mpaka anaandaa na vyakula issue ya kufuga kwa kutumia cage, lakini si kila mtu yupo karibu na ziwa, kutoka kwangu Biharamulo mpaka nifike Chato ziwani ni kilometa 50 siwezi kuwaambia wakazi wote wa Biharamulo sasa washuke Chato kwenda kufuga cage fifty kilometers unaenda ukaweke cage pale ukatafute eneo its difficult.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba sana Serikali mnisikilize katika hili bado tunaingiza Samaki all most fifty-eight billion tunaingiza value, lakini kwenye Ilani ya CCM ukurasa wa 55 tumesema tunataka tuongeze idadi ya vifaranga vinavyofugwa katika vituo vyenu vile vinne vya Ruvuma, Iringa, Morogoro na Tabora ifike vifaranga milioni tatu, sasa hao vifaranga milioni tatu tunamuuzia nani kama watu wanajenga mabwawa, wakishajenga mabwawa maua yanakauka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokuwa naomba nataka nitolee mfano, kwa mfano Biharamulo tulikuwa na mradi mkubwa wa maji ambao umekuwa design kwa ajili ya kutuhudumia pale kwa sababu tupo mbali na ziwa na hatuna access ya maji. Mwanzoni walikuwa wame-design wachimbe bwawa kubwa ambalo bwawa litakuwa linakusanya maji ya mvua kwa mwaka mzima, lakini bahati nzuri tutapata maji ya maziwa ambayo yatakuja kama Ilani ilivyoahidi, kwa hiyo mpango wa bwawa umeisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikaja na hii idea; Don Consult ndiyo wali-design ile kitu. Sasa nilitaka mfanye pilot project kwa kuanzia kwangu. Mje mwombe pesa, ongeeni na Don mchimbe lile bwawa pale kwetu Biharamulo. Bwawa lile litumike kwa ufugaji. Watu waliokuwa wanataka kufuga kwa kutumia vizimba sasa kule ziwani waje wafugie pale, then you will be charging them. Kwa sababu, kukuza wale vifaranga mnakosema, mtapata wateja pale. Is a business mind, mnaweza mkaja pale mkachimba lile bwawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkishachimba bwawa, maji yanaingia pale; watu wa kufuga kwa cage waje, lakini mtawa-charge kadri mnavyowakatia maeneo. Watafuga pale, mtakapokusanya fedha mnahamia sehemu nyingine, mnatengeneza bwawa lingine, maana yake tunatengeneza samaki fresh, hata mtu asiyekuwa karibu na ziwa aweze kupata samaki fresh, siyo wa kwenye friji. Maana samaki wanasaidia hata kukuza brain za watoto. Wote ni mashahidi hapa, kwa wenzangu wanaotoka Ukerewe kwa Kanda ya Ziwa, waliozaliwa mle visiwani, huwa tunasema kwa Kanda ya Ziwa watu wa Ukerewe wana ma-professor wengi sana. Kwa sababu gani? Samaki wanaoishi nao mle ziwani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba hili jambo mliangalie, mtusaidie, mje mjenge mabwawa. Mabwawa muwakodishe wafugaji, ambao watafuga na watakuwa wanalipa as time goes on huku mkikusanya fedha mnapeleka sehemu nyingine. Tunafungua watu kibiashara na vile vile tunapunguza fedha ambazo tunaagiza sato na samaki wengine kuwatoa nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuyasema hayo, kwa sasa yalikuwa ni hayo mawili, niseme kwamba naunga mkono hoja. Nategemea haya ambayo nimeyasema, tutapata majibu sahihi na ya uhakika ili wananchi hawa walioniagiza mambo ya ufugaji wapate solution kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na naunga mkono hoja. (Makofi)