Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Hon. David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa fursa hii ambayo umenipatia. Nitaongea kwa kifupi na mambo machache; ukiacha kupongeza kazi kubwa inayofanywa na Wizara hii mpya pamoja na wataalam, lakini niongee kwenye angle mbili tu. Angle ya kwanza, mara kadhaa nimezungumza na Mheshimiwa Waziri pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano juu ya changamoto kubwa sana ya mawasiliano kwenye eneo letu la Mufindi Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati fulani waliwahi kuniahidi kwamba wangeleta hiyo minara, niwaombe tu sasa wafanye utekelezaji. Tunayo changamoto kubwa sana kwenye Kata ya Idete ambako wananchi wanabidi wapande kwenye miti ndiyo afanye mawasiliano. Kwa mfano, ukiende pale Idete, utakuta kuna sehemu maalum kama center, zimewekwa Kamba pale kuna mtu anakodisha unapeleka simu yako pale halafu unaweka ukimaliza kuzungumza unarudi nyumbani. Hii si sawa kwa nchi ya level ya maendeleo ambayo tumefikia mpaka sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niwaombe wenzetu, walishaanza kufanyia kazi tayari pale lakini ziko kata jirani ambazo zina changamoto kubwa especially Kata ya Maduma, Idunda, Makungu, Kiyowela pamoja na maeneo mengine machache ambayo yameainishwa. Kwa hiyo niwaombe sana Mheshimiwa Waziri na timu yake watusaidie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nataka pia kutazama eneo moja. Tuna mfumo mzuri ambao tumeuanzisha sasa hivi especially kwa kuanzisha masomo ya computer mashuleni. Hata hivyo, naishauri Wizara wakae chini, watafakari ni namna gani tunaweza kuwafanya vijana wetu wakawa competent. Mambo mawili; moja masomo yale wanayosoma yawe na uhalisia, yawe ya kivitendo zaidi. Wapo vijana wanamaliza mpaka Vyuo Vikuu lakini pengine hata kutengeneza simu hawezi wa masomo ya IT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni changamoto kubwa sana. Hivyo, niwaombe waitazame vizuri mitaala yetu, ni namna gani vijana wanaosoma pengine wako Vyuo Vikuu kama ni ma-IT kama ni ma-engineer wapo kwenye mifumo ya habari, namna gani sasa wakimaliza wanaweza kuja kusaidia huku mtaani ambako kuna changamoto kubwa sana kwenye eneo hili. Kila kitu tunasema sasa hivi kinakwenda kiteknolojia na vijana wako mtaani hawana kazi, kwa hiyo ni changamoto kubwa sana. Namba mbili, tutazame namna ya kutengeneza centers kama hubs, baadhi ya nchi zilizoendelea waliandaa technological hubs kama zamani tulivyokuwa tunafanya maktaba. Unakwenda pale Dodoma Mjini kuna maktaba, vijana wanakwenda pale wanasoma, wanajifunza na kadhalika. Tunaweza kufanya hivyo hivyo kwa maeneo yetu kwenye level ya halmashauri, vijana walio mashuleni na wasio mashuleni wenye uelewa na uelewa mdogo, wakawa wanakutana inasaidia ku-exchange yale mawazo na ku- develop pengine mifumo mbalimbali ya ki-computer, matokeo yake tukaongeza confidence kubwa kwa vijana wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nilitaka tu niongee mambo hayo mafupi. Naunga mkono hoja. (Makofi)