Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Hon. Bakar Hamad Bakar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii kuweza kuchangia hotuba hii ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi. Tangia asubuhi leo hapa zinazungumzwa barabara tu hapa, lakini bahati nzuri nitahama kwenye eneo hilo la barabara nitakwenda kuchangia kuanzia haya ya 225 mpaka haya ya 227 ambapo inazungumzwa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge la kumi na moja lilipitisha Sheria Na. 2 ya mwaka 2019 Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, ni matarajio ya Bunge hili pamoja na Taifa kuona kwamba sheria ile inakwenda kuleta tija kwa Taifa lakini tija kwa mamlaka hii ya hali ya hewa Tanzania. Naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri tangia kupitishwa kwa sheria ile Sheria Na. 2 je ni mafanikiko gani yaliyopatikana kwa Taifa ama kwa mamlaka hii mpaka leo hii 2021? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nazungumza haya kwa sababu kwenye sheria ile Na. 2 wapo wadau mbalimbali ambao wametajwa kwenye sheria ile bandari ni mdau wa hali ya hewa aviation ni mdau wa hali ya hewa mazingira, viwanda watu wa nishati barabara majanga kilimo afya sayansi na teknolojia wote hawa ni wadau wa hali ya hewa hasa namuomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja atuambie je wanaitumiaje wadau hawa sheria ili Na. 2 ya mamlaka hii ya hali ya hewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu kwamba sheria haiwezi kutumika ipasavyo kama haijatengenezewa kanuni, lakini tangia mwaka huo ambapo sheria hii ilipitishwa lakini mpaka leo hakuna kanuni ambazo zinaiongoza kuifanya sheria ile iende ikatumike inavyopaswa. Sasa tunamuomba Mheshimwa Waziri atakapokuja atueleze je kanuni za Sheria Na. 2 ya mwaka 2019 imefikia wapi? imekwamwa wapi? tatizo ni nini kwamba mpaka leo kanuni zile hazijapatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania tuna bahati tumepata bahati ya kuwa na chuo kinachotoa taaluma ya hali ya hewa kwa nchi za Afrika ni nchi chache sana zenye bahati zenye vyuo ambavyo vinatoa taalum hii. Kwa nchi za Afrika nchi za SADC na hasa nchi za Afrika Mashariki ni nchi chache sana tulitegemea sana kwamba chuo hiki kingeweza kuitangaza Tanzania, lakini kingeweza pia kuongeza mapato ya mamlaka lakini pia kuitangaza Tanzania kupitia taaluma hii ya hali ya hewa. Lakini hatuoni kwamba kuna mikakati ipi ya kukifanya chuo hiki kuwa tija na kuitangaza Tanzania kuongeza mapato ya nchi yetu lakini kuongezea mapato ya mamlaka ya hali Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, endapo tutakiwezesha chuo hiki kimiundombinu naamini kwamba mapato ya mamlaka ya hali ya hewa yataboreka na maslahi yatakuwa mapana zaidi na tija kwa Taifa itakuwa pia itaongezeka. Namuomba waziri atakapokuja atuambie ni mikakati ipi aliyonayo kwenye kukiboresha chuo hiki cha mamlaka ya hali ya hewa ambapo kipo pale Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, utakubaliana nami kwamba kipindi hiki tulichonacho ni miaka ijayo ambapo majanga yanatokana na hali mbaya ya hewa taasisi hii ya mamlaka ya hali ya hewa ni taasisi muhimu sana kwa Taifa letu na kwa dunia. Umuhimu wa taasisi hii umeonekana zaidi hata hapa kipindi cha karibuni niipongeze sana Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia niipongeze mamlaka hii kipindi cha jaribio cha kimbunga cha jobo walikuwa wanatuhabarisha mara kwa mara bila ya habari zile nchi ingekuwa ipo katika wasiwasi sana watu walikuwa na wasiwasi na mali zao lakini watu walikuwa na wasiwasi na maisha yao lakini kupitia mamlaka hii tulikuwa tunapata taarifa za mara kwa mara na ile presha ilikuwa inashuka kila time ambapo ilikuwa inakuja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunamuomba sana Mheshimiwa Waziri atueleze ana mikakati gani ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi hili wafanyakazi wale waweze kufanya kazi zao kwa utulivu na moyo zaidi wa kujitolea. Sasa hivi kumekuwa na wafanyakazi wengi wa mamlaka hii wanatoroka kwa maana wanakimbia wanakimbilia sehemu nyingine ambazo taasisi ambazo zina maslahi zaidi. Lakini pia kuna wafanyakazi ambao wamepewa barua za kupandishwa madaraja tangia 2016 mpaka leo hii 2021 barua zile zinabakia kuwa ni hewa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunamuomba waziri atakapokuja atueleze ni kwa nini na lini maslahi ya wafanyakazi ni lini madaraja ya wafanyakazi pale ambao wana muda mrefu awajapandishwa madaraja ni lini sasa watapandishwa madaraja lakini ni lini barua zile zitajibiwa tangia 2016 mapaka leo 2021 watu wamepewa barua ya kupandishwa madaraja lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia tunafahamu taasisi hii ni taasisi ya muungano kama ilivyo sasa namuomba sana Mheshimiwa Waziri naiomba pia Serikali inapoajiri ajira hizi za taasisi ya muungano iangalie zaidi pande zote mbili, za muungano ile ratio ya 79 kwa 21 ianze kutekelezwa hasa kwenye taasisi hizo za muungano. Sasa hivi tunazungumza kwamba kuna ratio 79 kwa 21 maana zile ajira za muungano kwa Tanzania bara zitakuwa ni 79 asilimia lakini kwa Tanzania visiwani itakuwa ni asilimia 21 naomba sana tutakapo ajiri taasisi hizi za muungano basi tutumie hii ratio ili kuweza kuweka usawa kwenye ajira za taasisi zetu za muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mara baada ya kusema hayo nikushukuru sana ahsante sana. (Makofi)