Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji

Hon. Twaha Ally Mpembenwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibiti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ili kuweza kuchangia katika Wizara hii muhimu sana. Awali ya yote nichukue fursa hii kwanza kabisa kumpongeza ndugu yangu Juma Aweso, Waziri, kwa kazi kubwa na nzuri ambayo anaifanya katika WIzara hii. Sambamba na hilo, niseme tu unyenyekevu aliokuwa nao, mabega yake kuwa chini, basi aendelee kuwa hivyo hivyo. Nasema haya kwa sababu japokuwa mimi ni mgeni hapa Bungeni, sijwahi kusikia hata siku moja Mbunge yeyote akisema kwamba Aweso hapatikani kwenye simu, Aweso hana ushirikiano. Hivyo, nampongezahukuru sana Mheshimiwa Aweso kwa kazi yake hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhila vile vile, Mheshimiwa Naibu Waziri anafanya kazi nzuri sana. Tangu nifike hapa, kila Mbunge ambaye anamwomba kwenda nae katika Jimbo lake kuzungumza kero za wananchi analifanya hilo. Ni mategemeo yangu vile vile nitamwomba Kiti kikiridhia ili niweze kwenda nae kule Kibiti twende tukazungumze na wananchi wale kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichangia katika Wizara hii jambo moja tu la Kitaifa la msingi. Nalo ni kuweza kuwa na timu maalum katika Kanda hizi ili ziweze kufuatilia miradi mikubwa mikubwa. Tukifanya hivyo, tafsiri yake ni kwamba tutakuwa tunakwenda kurahisha mzigo mkubwa ambao Mheshimiwa Waziri anakuwa nao kila wakati. Yeye atakuwa anapokea zile taarifa, akiwa anakwenda kule tayari ana taarifa in advance. Kwa hiyo, tukifanya hivyo itamsaidia sana Mheshimiwa Waziri katika kuweza kui-control hii miradi mikubwa mikubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba nizungumze pale Jimboni kwangu. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri, katika bajeti ambayo ilikuwa imetengwa mwaka 2020/2021 tuna miradi takriban kama minne. Kuna mradi mmoja uko kule Mtunda takriban shilingi milioni 736, mradi ule mpaka hivi sasa bado haujaanza na fedha bado haijapelekwa. Kuna mradi mwingine uko kule katika Kata ya Mahege, takriban shilingi milioni 402, fedha bado hazijapelekwa nayo ilikuwa ni bajeti ya mwaka 2020/2021. Lakini kama haitoshi, kuna mradi ambao uko katika Kata ya Mjao shilingi milioni 486, bado vile vile fedha hazijapelekwa, nayo ni bajeti ya mwaka uliokuwa umepita.

Mheshimiwa Naibu Spika, pale anapotoka Mbunge kabisa katika Kata ya Mtawanya, kuna mradi wa shilingi milioni 61. Chonde, chonde Mheshimiwa Waziri, sitaki kuamini akili yangu kwamba fedha hizi hazitokwenda kwa sababu anakujua. Uchapakazi aliokuwanao Waziri, mambo makubwa ambayo anaendelea kuyafanya katika sekta hii, naamini tu kwamba ni kiasi cha kusema muda utafika, fedha hizi zitakwenda. Kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri tuweze kwenda kufanya taratibu za msingi kupeleka fedha hizi ili sasa miradi ile iweze kwenda kutekelezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimwambie Mheshimiwa Waziri tu kama mambo yatakuwa mazuri ukipata ruhusa kule Tanga. Miradi hii itakapokuwa imekamilika, nataka nimhakikishie Waziri, sisi watu wa Kibiti tuna zawadi tumemwandalia pale. Atakapokuja kama atakuwa
amepata ruhusa kuna zawadi ya mathna tunaweza tukampatia ili sasa kwa namna moja au nyingine mambo mazuri yaendelee kufanyika na wananchi wale waweze kunufaika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumze jambo moja la msingi kubwa sana ambalo limewagusa sana watu wa Kibiti pamoja na Wajomba zangu wa Rufiji pale. Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri amesema kwamba upembuzi yakinifu unaweza ukaenda kufanyika katika Bonde la Mto Rufiji. Nataka nimwambie, hii kauli ni kauli ya matumaini makubwa sana kwa wajomba zangu wa Rufiji na sisi vile vile watu wa Kibiti.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka Mheshimiwa Waziri, aamini hili, katika Jimbo la Kibiti kuna kata tangu jimbo lile lianzishwe hazijawahi kuwa na bomba. Kuna Kata ya Kiongoroni, kuna Kata ya Mbuchi, kuna Kata ya Maporoni, kuna Kata ya Msala, hizi kata hazijawahi kuona bomba la maji likiwa linafunguliwa. Kwa hiyo, uanzishaji wa mradi ule utakapokuwa umefanikiwa, nimhakikishie Waziri kwamba, tutamwongeza zawadi nyingine. Tutakwenda sasa katika mambo ya wathulatha sio tu mathna.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima na taadhima na unyenyekevu wa hali ya juu sana, naomba niunge mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)